Nilivunja urafiki na kumshushia heshima Mjomba wangu baada ya kugundua ni mtu mwenye tabia ya kuingilia faragha yangu

Nilivunja urafiki na kumshushia heshima Mjomba wangu baada ya kugundua ni mtu mwenye tabia ya kuingilia faragha yangu

Kawaida mjomba ni mtu wa heshima sasa akishakuwa na maswali ya hovyo sidhani kama ataheshimika tena
Yeye ameacha mke nyumbani yupo mjini
Wewe kabila gani?
Ninavyojua katika watu ambao hawajiheshimu basi ni wajomba kwa wapwa zao.!!
Mjomba anaweza kuongea pumba zozote kwa mpwa wake na isiwe big issue….

Mimi anko wangu bhana ashawahi kutusuluhisha ugomvi na mpz wangu kisha akamwambia muombe game ili tujue km kweli kakusamehe 😹😹😹

Naye lilivyo jinga likaja kunisimulia nikabaki nasikitika.!! Huyo mjomba wako anakuzingua km mtani wake wala hamaanishi..!!
 
Kwani sijaoa, mchumba wangu wa kwanza wao ndio waliomfitini mpaka tukaachana nilipopata huyu wa pili sikutaka tena kushirikisha mtu kila mtu afe na maisha yake
😹😹😹
Huyo mjomba bila shaka type ya kina Shaban Madobe.
Mwambie aache unaa, ila na wewe si ungemwambia nishaoa
 
😹😹😹
Huyo mjomba bila shaka type ya kina Shaban Madobe.
Mwambie aache unaa, ila na wewe si ungemwambia nishaoa
Nilipowaeleza kipindi nipo na mchumba wa kwanza ndipo mahusiano yetu yalivunjika
 
Hapana, ilikuwa ni utashi wa kawaida wa wazazi wengi wa Kiafrika tu.

By the way mimi si punga ila kuwa punga ni haki ya kibinadamu tu, ni lifestyle ya mtu tu, si kitu cha kushikia bango kihiivyo kwa watu wanaoelewa dunia.

Ni huko tu kwa Watalibani mnakoona kuwa punga ni jambo la kushikia bango hivyo.

Yani mtu anayetaka kuwa punga ana haki ya kuwa punga kama wewe usiyetaka kuwa punga ulivyo na haki ya kutokuwa punga.

Na ukiingilia haki yake hiyo ya kuwa punga unafungua mlango na wewe usiyetaka kuwa punga ulazimishwe kuwa punga.
Kiranga A.K.A mchicha mwiba. Pole!
 
Hapo ndipo akili yako ilipoishia, huwezi kujadili hoja unaleta viroja.
Hoja zipi wakati utaanza kutumia tumia viswahili na hoja hujibu chochote tunakujua aisee. Hoja ngapi huwa unakimbia hewani kwa kutumia kivuli cha kutumia viswahili visivyo na msingi?
 
Hoja zipi wakati utaanza kutumia tumia viswahili na hoja hujibu chochote tunakujua aisee. Hoja ngapi huwa unakimbia hewani kwa kutumia kivuli cha kutumia viswahili visivyo na msingi?
Basi niweke ignore list usione ninachoandika tena maana sina hoja.

Mimi nakuweka ignore list kuanzia hapa sitaona unachoandika maana naona huna hoja.

Naondoa mzozo usio na muelekeo, maana wala tija.
 
Basi niweke ignore list usione ninachoandika tena maana sina hoja.

Mimi nakuweka ignore list kuanzia hapa sitaona unachoandika.
Usinipangie nini cha kufanya wewe kama unaweka hiyo ignore list weka.
 
Mjomba kuuliza umeoa si jambo la kukasirika. Na kuhusu wanaume kuolewa Kuna kitu amesoma kwako utakua unakaa kiupinde upinde
 
Mjomba kuuliza umeoa si jambo la kukasirika. Na kuhusu wanaume kuolewa Kuna kitu amesoma kwako utakua unakaa kiupinde upinde
Hana lolote mwehu tu yule ni mwanaume wa hovyo kwasababu ana chokochoko wanaume hawako hivyo
Mjomba ni mtu wa heshima sana yeye hajui maana ya heshima
 
Huyo mjomba hakuona jambo lingine zaidi ya kuowa na kuolewa? Lakini mjomba ni Mama.
 
Ndugu zangu kuishi Afrika lazima uweze kuvumilia kero za watu lasivyo patakushinda
Kero kubwa ya Afrika ni watu kutaka kujua siri zako na mambo binafsi yanayohusiana na faragha

Labda nianze kwa kujielezea kiasi, mimi ni baba wa watoto wawili wa kwanza ana miaka mitano wa pili miaka miwili ninaishi kwangu na mke na watoto

Mimi ni mtu ninayependa sana faragha na ni mtu ninayeheshimu kila mtu lakini kwa sharti moja, huwa sipotezi muda na siheshimu mtu yeyote asiyeniheshimu

Mimi ni mtu nisiyependa uchokozi wa aina yeyote na huwa sipendi kuchokozwa inapotokea reaction yangu inakuwa mbaya sana na mtu huyo anaweza kujuta kwa uamuzi nitakaochukua

Maisha yangu yapo katika faragha na huwa sipendi kabisa umbea kuwa na urafiki na mtu mwenye kidomodomo, mtu wa kusema mambo, kaulimbiu yangu utakachokiona hapa kiishie hapa hapa nisisikie kwa mtu

Baada ya kugundua tabia mbaya za ndugu zangu za midomo mirefu wamekuwa ni watu wasiofahamu maisha yangu kwao imekuwa ni fumbo

Mimi nina wajomba wanne, hawa wajomba wanne nawaheshimu sana tangu nazaliwa, hawa watatu kila mmoja ana maisha yake natangu niwafahamu hawajawahi kunikwaza wala sijawahi kuwakwaza

Huyu mmoja ana familia kijijini lakini anaishi mjini kwa dada yake
Kwa dada yake yupo yeye na mama yao ambaye ni bibi yangu pamoja na yeye. Dada yake alimpeleka kwake ili afanye kazi ana kama miaka 50

Huwa mara kwa mara ninapotembelea huo mkoa lazima nimsalimie dada yake ambaye ni mama mdogo wangu kwenye hiyo familia yao

Tangu zamani nikienda kwenye hiyo familia na chochote mkononi wanafurahi sana isipokuwa yeye anaishia kunikata jicho la wivu

Safari mbili za mwisho kwenda pale alinitazama vibaya sana kwa macho ya wivu
Nilipoondoka akathubutu kunipigia simu akiniuliza kama nimeoa,
Sikumjibu chochote kwasababu sipendi umbea nachukia sana maswali ya kimbea

Safari ya mwisho kwenda pale baada ya kuondoka akanipigia simu akanambia nizae watoto kwasababu dunia ya leo imeharibika sana wanaume wanaolewa
Baada ya maneno hayo machafu sikujibu

Nilipokata simu nikajiuliza huyu mtu mbona kama amekuwa wa hasidi katika maisha yangu?
Watu kuharibika inahusiana nini na maisha yangu?
Mke wangu ninayemuoa mimi kwa faida zangu anamhusu nini yeye?
Anayetunza mke wangu ni mimi au yeye?
Watoto wangu wanamuhusu nini mtu mwingine?
Mbona ni maisha yangu binafsi?
Mbona wanaume hatuna tabia za chokochoko?

Nikagundua huyu ni mtu wa chokochoko

Baada ya hapo nikamlima Block ya nguvu naendeleza urafiki na wale tunaoheshimiana
Mjomba ni mama.

Mjomba wako ana mashaka na yas yako
 
Ndugu hukunelewa vizuri, mm ni mtu ninayechukia sana umbea sikuchukia maswali bali ni umbea hata mke wangu ananifahamu mambo yangu na familia yangu hayamhusu mtu mwingine kila mtu afe na yake
Basi mjomba yako hajui kama Una Mke teyari...
Mpotezee na hifadhi heshima yake..
 
Kufanya hivyo amenikosea adabu kwasababu umri wangu sio mtu wa kuniuliza maswali hayo, afe na maisha yake na mimi ni deal na yangu chokochoko kwa wanaume hazifai, hayo maswali akaulize watoto wake
Relaax😄
Sikuhizi wanajibu 'sijaoa ila pia sijaolewa'
 
Oy mkuu haya maisha unayachukulia siriazi sana. Maisha hayataki usiriazi kihivyo. Kula vizuri, Kunywa maji mengi, fanya mazoezi na hakikisha huchukulii Kila jambo Kwa usiriazi.
Tofauti na hapo utakuwa unahisi Kila mtu anakufuatilia.
Nb
Umri unavyozidi kwenda one day utakuja kugundua hats hakuna aliyekuwa anakufuatilia
 
Oy mkuu haya maisha unayachukulia siriazi sana. Maisha hayataki usiriazi kihivyo. Kula vizuri, Kunywa maji mengi, fanya mazoezi na hakikisha huchukulii Kila jambo Kwa usiriazi.
Tofauti na hapo utakuwa unahisi Kila mtu anakufuatilia.
Nb
Umri unavyozidi kwenda one day utakuja kugundua hats hakuna aliyekuwa anakufuatilia
Inatafakarisha sana
 
Back
Top Bottom