Nilivyogundua tu Mwanamke ana gari, nikaona huyu siyo Level zangu

bora kuombwa hela ya wese kuliko kuombwa hela ya gas ya kupikia imeisha
 
Mimi nilimsemesha mama mmoja akaniambia twende tukaongelee kwenye gari Yako.Ilibidi nikachekee choooni.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ulimuachaje hapo sasa?
 
Ni kama vile umeingia zile hoteli zina menu haijaandikwa bei halafu kuna mziki wa taratibu unapigwa
Have you ever experienced a menu without prices of different dishes? Binafsi sijawahi ona kwakweli, embu nitajie hata moja mkuu.
 
Watu wanatofautiana.. kuna vijana wa kiume wengine hawapo confident kwenye mahusiano ya namna hio..

Sema issue umeiweka sana kwenye kukojozana kitu ambacho ni kidogo kwenye mahusiano kwa ujumla..

Kuna ile hali ya kujihisi hautoshi kwake , yaani we mwenyewe kama mwanaume unajiona you are not enough.. automatically... unajihisi financial freedom uliyonayo haitoshi ku keep nae hata kama huna shida ndogondogo..

Mwanamke anafanya expensive trips, anakwenda expensive vacations na anatembelea expensive restaurants/hotels ...

Mnafika hotel hio mzee, ile mmemaliza kula/kunywa unajitia kama unatoa wallet unataka kulipa bill hadi manzi anakuuliza 'are you sure?' Yaani anaelewa kipengele..

Ku keep up na mwanamke wa namna hio ni ngumu...

Maana hata humu jf tunaona vijana wanashauriana 'mwanamke asikuzidi hata kimo' kuna ukweli flani ndani yake..
 
Mkuu umefanya vizuri, mambo ya kuanza kujaza mafuta kwenye magari ya Wanaume wenzako umejiongeza
 
huna uthubutu. angekuwa Robert Heriel Mtibeli yaani huyo alikuwa chakula kabisa..
 
Sema ukiwa hujalewa unashushaga nondo sana

Hongera sana kwa madini
 
Raver 4 zinatengenezwa mwezini? Kweli una haki ya kumuogopa
 
Mwanaume anayejiamini ni Yule anayejua limit yake, sio kuhamia Tu na mwisho wa siku unaharibu Brand yako
Ni kweli mkuu..

Yaani unalazimisha mahusiano hadi mwanamke anakuambia ana wish uwe na financial freedom zaidi.. unaanza kuwaza na kuona amekutukana wakati kakuambia kwa upendo tu.. unaona amekudharau kumbe sio type yako...

We umemkuta mtu anakula Kempinski unaanza ushauri 'unatumia gharama kubwa sana' kumbe wewe ndiye huna hio pesa...

Issue ni kwamba huyo si type yako... just move on.. tafuta wa level zako mfanye maisha...

Na katika visa vingi mwanamke mwenye uwezo wa kifedha kuliko mwanaume huishia kuja kukuacha na kuendelea na mwenye uwezo zaidi yake ama wanalingana....nasisitiza katika visa vingi..
 
Nime date na wanawake wa aina hiyo wapatao watatu sasa na wote nimekaa nao kwenye mahusiano sio chini ya miaka 2 bila shida yeyote, bahati mbaya kati ya hao, wawili walikuwa wake za watu (nami nipo kwenye ndoa uchwara) na tumesitisha mahusiano kwasababu za umbali wa kimaisha, ila nikirudi walipo naendelea nao bila shida, na mmoja hakuwa na ndoa ila amesafiri kwasasa zaidi ya mwaka hayupo.
Mnajua wanawake wanapenda mwanaume anaye jiamini na mwenye akili na mwanaume anayeweza kumuonesha misimamo.
Mimi huwa nashangaa mwanaume unaenda sehemu expensive halafu mwanamke wako ndio anatoa pesa kukulipia (hilo ni kosa kubwa) maana yake umeshindwa kuonesha kujiamini na huna akili ya kuchallenge au kum control kisaikolojia. KIMSINGI MWANAMKE AKIGUNDUA UNAMZIDI AKILI NA UNAJIAMINI BASI ATAKUPA PESA USHIKE WEWE ILI MNAPOTOKA OUT BILLS ZOTE ULIPE WEWE.
Sasa ukishindwa kuonesha unajiamini na una akili za ziada hakika hawezi kukupa hata mia mbovu, kwahio mwanamke kukupa ushike pesa zake ili mkazitumie ni ISHARA YA YEYE KUONESHA AMEJI SUBMIT KWAKO NA AMEKIRI YOUR THE BEST.
Mimi napenda ku date na wanawake walionizidi uwezo kiuchumi kwasababu wananipanua akili sana, na nina kiri kwamba mafanikio yangu niliyonayo na juhudi za maisha nilizonazo ni kwasababu ya ku date na wanawake walionizidi kiuchumi. Mimi sipo vibaya kiuchumi angalau namudu kumtoa mwanamke tukatumia hata 100k na nisiijutie, ila miaka ya nyuma hata kulipia lodge ilikuwa kipengele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…