#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

Hii ni campaign,kama wewe umekubali kufanyiwa majaribio ni wewe,sisi wengine hatupo tayari.
 
Bora hayo, ila nyie subirini kuwa mazombi na kuzaa mapredector
 
6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiiana

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi

8. Nilitoa mbegu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiiana

😂 😂 😂
 
Chanjo hazikufanyiwa majaribio kwa watoto haijulikani ina effect gani kwa watoto.
 
Chanjo hazikufanyiwa majaribio kwa watoto haijulikani ina effect gani kwa watoto.
Na bado hakuna aliyepinga chanjo za watoto.
Mtoto wa Tanzania hadi akifika miaka 5 ana chanjo zaidi ya 5.
Na hakuna aliyehoji hadi Leo.
 
Na bado hakuna aliyepinga chanjo za watoto.
Mtoto wa Tanzania hadi akifika miaka 5 ana chanjo zaidi ya 5.
Na hakuna aliyehoji hadi Leo.
Unazungumzia chanjo za watoto ila mimi nazungumzia chanjo za corona kuwa hazikufanyiwa majaribio kwa watoto, chanjo huwa zinajaribiwa kwa rika tofauti tofauti kwahiyo siku kusudia hizo chanjo ambazo ni kwa ajiri ya watoto.
 

WHO wameipitisha, au na hilo hulijui? kama una ufahamu fulani basi utakuwa unafahamu maana ya crisis management and namna ya contain epidemics/pandemics. unaposafiri na gari likakuharibikia njiani na porini utang'ang'ania upate chakula cha biriani? nyoka akiingia ghafla chumbani kwako utachagua cha kumpiga nacho? mtengenezaji na WHO walijiridhisha kuwa chanjo inaweza kutoa kinga dhidi ya corona kwa zaidi ya asilimia 70, yaani inaweza kupunguza idadi ya wanaokufa sasa, wanaougua sasa, waliojilock down sasa kwa zaidi ya 70%, wewe na wenzio mnasema hapana tuwaache hawa wafe tu kwakuwa hiyo chanjo pamoja na kupunguza kufa kwa zaidi ya 70% lakini haijulikani madhara yake ya muda mrefu. Tungekuwa na watu wanaofikiri kama hivi dunia ingeangamia yote siku nyingi, maana mpaka leo ziko dawa ambazo mwanzo zilionekana zinafaa lakini baadae zikaonekana hazifai na kupigwa marufuku kutumiwa na binadamu wote au makundi fulani ya watu kama watoto, wajawazito, wanaonyonyesha au wenye afya za aina fulani. Hata hizi chanjo zitaendelea kuboreshwa kadiri watu wanavyozitumia kama ulazima utakuwepo. Na chanjo nyingine bora zaidi zinaweza kutengenezwa, kama zilivyo antibiotics
 
wewe ni sheikh wa mkoa wa daresalaam?
 
Tugawane hio hela ulipewa ndipo nikusupport
 

Hakukuwa na mjadala. Kwa milongo kadhaa watu wanachanjwa ila leo kila mmoja amegeuka mwana sayansi. Nimechanja na kupata dalili za hapo juu. Kuhusu kuongezeka nguvu sijui ila najikuta nasukumwa wiki hii kusafiri kumfuata wa kumtima wangu nikampe yote ninayojisikia mwilini na moyoni.
 
Mlinganisho huo na wa polio surua haviendani mkuu sababu ilichukua muda mrefu kupatikana chanjo yake ila hii imekuja very soon yaani testing yake inafanyika directly ndio maana hata uchanjwe bado uko hatarini na zinapingwa kwa sehemu kubwa sana

Ilichukua muda kwa sababu teknolojia ilikuwa haijakua. Usilinganishe. Pia urgency ni kubwa kwa huu UVIKO-19.
 
Amka toka ndotoni utajikojolea bure.
 
Amka toka ndotoni utajikojolea bure.
Unatumia moyo badala ya ubongo kufikiri. Una faida gani hadi uogope kufa kwa chanjo? Hata upewe miaka 159 kuishi una nini Cha maana unafanya? Shetype
 
Hakika mkuu ,,,hii chanjo ni salama na hakuna madhara yeyote.
,tena haya mambo kufata mkumbo unaweza kuharibu maisha yako yote.

Jambo lolote kabla ya kulifanya kwanza unapaswa ulipime.

Wapo watu fulani waliambiwa kupata chanjo au kazi basi..
Wao waliamua kuacha kazi yenye maslahi kisa kukubali kuchanja.
 
Unazungumzia chanjo za watoto ila mimi nazungumzia chanjo za corona kuwa hazikufanyiwa majaribio kwa watoto, chanjo huwa zinajaribiwa kwa rika tofauti tofauti kwahiyo siku kusudia hizo chanjo ambazo ni kwa ajiri ya watoto.
Hebu tuambie namna chanjo ya polio, pertussis, Diphtheria, Tetanus, surua, na flu ambazo umeshachanjwa kabla hujafikisha umri wa mwaka mmoja zilivyotengenezwa na kilichomo kwenye chanjo hizo na madhara yake. Au unakariri kama kasuku tu.
 
Kaka nimeshaona watu wengi ambao mwanzo walisita kuchanja sasa wananiuliza wapi wakachanje bila kukutana na foleni. Hawa ni wale waliokuwa wakisubiri damu za waliochanja zigande na kufa, lakini wanawaona wanadunda mitaani tena kwa furaha zaidi na kujiamini kuliko wao. Hata hawa wanaopinga humu jf wana wasiwasi kubwa mioyoni mwao kama wachanje au wasichanje, hasa baada ya kuona misululu ya watu wanaochanja wakiwemo watu muhimu kuliko wao kama Marais wa dunia, mawaziri, matajiri, wanajeshi wa marekani na NATO wote, wachezaji wote wa EPL, VPL (simba na yanga wote kabisa), Series A, LaLiga, Bunde na hata Messi. Wao wana thamani gani hata iwaogopeshe kuchanja, lazima wanakosa raha na amani kwenye nafsi zao.

Sisi bwana tumechanja, na tunaongozwa na misemo ya "Sayansi haidanganyi" na "kifo cha wengi harusi" na "kila nafsi itaonja umauti"
 
Hakika mkuu,,
Mimi nilipata moyo baada ya kuona hata wazungu wnyewe wanalazimishwa kuchanja.
Nikasema jinsi wazungu wanavyopenda raia wao,
Kweli watakubali wauwe watu wao?
Kwl watakubali kuwapa sumu watoto na jàmaa zao wafe?
Nikaona hapana..

Hii ni salama zaidi.
Hakuna chanjo ya majaribio ikapigwa dunia nzima..
Tena itafika wakati watachanjwa kwa pesa hapo ..
Wewe subiri tu.
Ngoja chanjo iwaingie akilini.
 
Kaka mtu huwezi kuishi kwa kubahatisha, huwezi kufikiria negative ukafika mbali, huwezi ukapinga na kushawishi watu kwakutumia dhana, eti eti eti. Bibi yangu alikufa hajapanda gari kwa kuogopa ajali barabarani, ingawa ni kweli magari yanasababisha ajali lakini ni kweli kila anaepanda gari atapata ajali? je, ni kweli kila gari barabarani litapata ajari?. Hivi huyo mtengeneza chanjo ana akili gani kushinda watu wote na taasisi zote (WHO, UNICEF, CDC, FDA, FBI, CIA, TAKUKURU) hadi aipe sumu dunia nzima kwa chanjo zake bila kugunduliwa?. Kweli wajinga hawaishi hadi dunia iishe. Yuko mtu mpaka leo yuko tayari kutii maagizo ya mganga apeleke kuku mwenye manyoa ya rangi tatu ili akatibiwe TB. Na kila taifa linao wajinga wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…