#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

Ndy maana over 40 na kuendelea kinga muhimu sana.

Hivi MKUU Mara ya mwisho ni lini kufanya fully body check up ?
Na kujuwa huna tatizo lolote?
Ni kwamba hayo maradhi uliyotaja ni baadhi tu ya vitu vye kushusha kinga za mwili kwa maana yapo mambo mengine yenye kufanya kinga zetu kuwa dhaifu, kwahiyo nachokiona hapo si suala la umri au kuwa na hayo magonjwa bali ni issue ya kinga za mtu husika, ndio maana nikauliza watot wadogo kinga zao ndio imara sana?
 
Yaani uzoefu wako ni kupanda bus la Lay-land lililochukua masaa 10 kutoka Dar-Moro, ukiambiwa siku hizi kuna yanayochukua masaa 3 tu hutaki. Ukiambiwa siku hizi kuna ndege inakwenda USA moja kwa moja bila kutuwa Amsterdam hutaki, hiyo ni sayansi?
Sidhani mkuu kama umefuatilia hizo hoja za kisayansi za wenye kupinga hizi chanjo, kuna mambo mengi zaidi ya hayo ya muda, kuna mambo hadi ya jinsi hayo majaribio yenyewe ya hizi chanjo hadi jinsi chanjo zilifikia kuruhusiwa kutumika kwa watu wote na mengineyo.
 
Mume wangu mtarajiwa kama huko humu usidanganyike na hizi nguvu za kiume zinazoletwa na chanjo.baki hivyo hivyo tutavumiliana
 
Kuna walikuwa wakimtanguliza Mungu katika kila jambo na wameondoka kwa corona, na wengine walikuwa na makanisa kabisa. acha kumjaribu mungu wako bure.
Wewe kachanje. Achana na mimi. Mungu wangu sio korona wala chanjo, tumeelewana?
Hata nikifa leo, inakuhusu? Wewe kachanje, wachanje na familia yako, hapo ndio wigo wako unaishia. Achana na familia zisizokuhusu. Huo ndio uungwana!
 
Sidhani mkuu kama umefuatilia hizo hoja za kisayansi za wenye kupinga hizi chanjo, kuna mambo mengi zaidi ya hayo ya muda, kuna mambo hadi ya jinsi hayo majaribio yenyewe ya hizi chanjo hadi jinsi chanjo zilifikia kuruhusiwa kutumika kwa watu wote na mengineyo.
Kwenye swala la muda wa kufanya maribio hiyo ni sawa lakini hiyo siyo sayansi, huo ni uzoefu tu ambao hauwezi kujibu swali kuhusu chanjo ina madhara au haina, inakinga au haikingi. Kusema chanjo haifai kwakuwa imetengenezwa na kutumika kwa muda mfupi haihalalishi kuwa na hitimisho la chanjo ni mbaya.

Chanjo hii imekuja kwa hati ya dharura kwakuwa wakubwa ndio wanaokufa kwa wingi, wamejifungia ndani na uchumi wao kushuka, wamechanganyikiwa. Binafsi kutoka kwenye moyo wangu ni kwamba, kama una uhakika kuwa hutaugua corona kali kiasi cha kupoteza uhai wako basi usichanje ili usubiri uone waliochanja wamepatwa na balaa gani. Lakini kama unadhani uko kwenye hatari ya kuugua corona na kufa na kuwaacha watoto wako, mke/mume wako, wazazi wako, nyumba yako, shamba lako au suti zako, ni heri uchanje tu ili usogeze mbele muda wako wa kufa ili kulipia karo za watoto wako leo. Tusidanganyane, kila mtu anazosababu zake za kuchanja au kutochanja, ni vibaya sana kufuata mkumbo wa kuchanja au kutokuchanja.

Hata mungu kuna wanaosema yupo na wako wanaosema hayupo, ni heri ya anaeamini kuwa yupo ili asipokuwepo hapati hasara. Chanjo hii ni hiari na inapaswa kuwa hiari kwelikweli. Kazi ya uzi huu ni kuwaunganisha wale ambao tumechanja tayari kupeana ushuhuda na uzoefu tunaokutana nao baada ya kuchanja. Hatumaanishi kuwa kuna udalali au kushawishi wengine wachanje, HAPANA. Tumia akili na utashi wako kuchanja au kuacha.
 
Ufafanuzi wa hii...
Ninajifahamu mwenyewe na hata mwenzangu kuwa kama nimeendesha gari kwa masaa 12 mfululizo nikifika nyumbani kazi zangu ni kuoga, kula na kulala kwanza, lakini baada ya chanjo naweza kusafiri bila kujisikia uchovu sana kiasi cha kushindwa kwichikwichi hotae x 2 kwa mpigo tena kwa mke wangu wa maisha ya miaka 25 iliyopita
 
Kwenye swala la muda wa kufanya maribio hiyo ni sawa lakini hiyo siyo sayansi, huo ni uzoefu tu ambao hauwezi kujibu swali kuhusu chanjo ina madhara au haina, inakinga au haikingi. Kusema chanjo haifai kwakuwa imetengenezwa na kutumika kwa muda mfupi haihalalishi kuwa na hitimisho la chanjo ni mbaya.

Chanjo hii imekuja kwa hati ya dharura kwakuwa wakubwa ndio wanaokufa kwa wingi, wamejifungia ndani na uchumi wao kushuka, wamechanganyikiwa. Binafsi kutoka kwenye moyo wangu ni kwamba, kama una uhakika kuwa hutaugua corona kali kiasi cha kupoteza uhai wako basi usichanje ili usubiri uone waliochanja wamepatwa na balaa gani. Lakini kama unadhani uko kwenye hatari ya kuugua corona na kufa na kuwaacha watoto wako, mke/mume wako, wazazi wako, nyumba yako, shamba lako au suti zako, ni heri uchanje tu ili usogeze mbele muda wako wa kufa ili kulipia karo za watoto wako leo. Tusidanganyane, kila mtu anazosababu zake za kuchanja au kutochanja, ni vibaya sana kufuata mkumbo wa kuchanja au kutokuchanja.

Hata mungu kuna wanaosema yupo na wako wanaosema hayupo, ni heri ya anaeamini kuwa yupo ili asipokuwepo hapati hasara. Chanjo hii ni hiari na inapaswa kuwa hiari kwelikweli. Kazi ya uzi huu ni kuwaunganisha wale ambao tumechanja tayari kupeana ushuhuda na uzoefu tunaokutana nao baada ya kuchanja. Hatumaanishi kuwa kuna udalali au kushawishi wengine wachanje, HAPANA. Tumia akili na utashi wako kuchanja au kuacha.
Ulikuwa unanijibu mimi au mtu mwengine? mbona unajibu ambavyo mimi sijavizungumza, mimi sijazungumzia issue ya muda.
 
Wewe kachanje. Achana na mimi. Mungu wangu sio korona wala chanjo, tumeelewana?
Hata nikifa leo, inakuhusu? Wewe kachanje, wachanje na familia yako, hapo ndio wigo wako unaishia. Achana na familia zisizokuhusu. Huo ndio uungwana!
Usipotumia choo kujisaidia hutaachwa hivihivi eti kwakuwa ni hiari yako na familia yako; wewe ni mali ya serikali ndio maana unalindwa na kuhudumiwa na serikali. Unalindwa na kuhudumiwa kwasababu tatu tu ambazo ni nguvu kazi yako, kulipa kodi kwa serikali na kuzaa ili wafanyakazi na walipakodi wasipungue. Ndiyo maana Hata leo hii kama ukijaribu kutaka kujinyonga na serikali ikakuona itakukamata na kukupa adhabu. Kuacha kuchanja ni sawa na kutaka kujiua, serikali inaweza isikubembeleze kuchanja kama itajiridhisha kuwa unataka kujiua au unataka kuua walipakodi wake wengine kwa kueneza corona. Ndio maana serikali inaweza kupiga marufuku na kumwaga vyakula vya akina mamalishe kama mtaani kuna hatari ya kipindupindu ili kuilinda nguvukazi yake na walipakodi wake wasife kwa kipundupindu.

Hivi kaka hata akili ndogo kama hii huna? Hiari yako inaishia pale hiari ya wengine inapoanzia. Haiwezekani serikali ipote nguvukazi yake na walipakodi wake kwaajili yako.
 
Hapo kwenye nguvu za kiume, umenifanya nicheke mpaka nilio karibu nao wanahitaji kujua nacheka nini!?

Ila sio kwa promo hilo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Usipotumia choo kujisaidia hutaachwa hivihivi eti kwakuwa ni hiari yako na familia yako; wewe ni mali ya serikali ndio maana unalindwa na kuhudumiwa na serikali. Unalindwa na kuhudumiwa kwasababu tatu tu ambazo ni nguvu kazi yako, kulipa kodi kwa serikali na kuzaa ili wafanyakazi na walipakodi wasipungue. Ndiyo maana Hata leo hii kama ukijaribu kutaka kujinyonga na serikali ikakuona itakukamata na kukupa adhabu. Kuacha kuchanja ni sawa na kutaka kujiua, serikali inaweza isikubembeleze kuchanja kama itajiridhisha kuwa unataka kujiua au unataka kuua walipakodi wake wengine kwa kueneza corona. Ndio maana serikali inaweza kupiga marufuku na kumwaga vyakula vya akina mamalishe kama mtaani kuna hatari ya kipindupindu ili kuilinda nguvukazi yake na walipakodi wake wasife kwa kipundupindu.

Hivi kaka hata akili ndogo kama hii huna? Hiari yako inaishia pale hiari ya wengine inapoanzia. Haiwezekani serikali ipote nguvukazi yake na walipakodi wake kwaajili yako.
Acha ujinga basi!
Hivi kabisa na akili zako timamu unalinganisha essential service kama choo na chanjo ambazo watengenezaji wenyewe wanasema ziko kwenye clinical trial? Hivi akili huwa mnaziweka wapi inapokuja suala la chanjo?

Nakuwekea hii fact sheet ya mtengenezaji wa chanjo hii. Soma halafu ukome kutoushughulisha ubongo wako. Yaani akili unaweka likizo kisa ni chanjo?

Hizi ni baadhi ya nukuu:

- "The Janssen COVID-19 Vaccine may prevent you from getting COVID-19. There is no U.S. Food and Drug Administration (FDA) approved vaccine to prevent COVID-19"

Hi chanjo haijawa approved kwa sababu hawajaweza ku ascertain usalama wake. Hawa ndio wenye teknolojia na ndio nchi iliyotengeneza chanjo. Sasa kama ni salama kama unavyodaio, kwa nini hawajipitisha? Unadhani unaijua chanjo kuliko wao? Ukiweza kupunguza kiherehere, ukaamua kuutumia ubongo wako kufikiri, utaelewa sababu!

- "The Janssen COVID-19 Vaccine may not protect everyone."
Okay mjuaji wa yote umeisoma hiyo? Sasa niambie unajuaje kama yupi itaweza kumlinda na yupi haitamlinda? Unadhani unajua sana chanjo kuliko walioitengeneza? Kama sio kiherehere ni nini? Ni ngebe tu, hamna unalojua!

- "The Janssen COVID-19 Vaccine has not undergone the same type of review as an FDA-approved or cleared product. FDA may issue an EUA when certain criteria are met, which includes that there are no adequate, approved, and available alternatives"

Umeelewa hiyo mjuaji wa chanjo? Hii chanjo haijapitishwa kwa sababu haijapitia hatua ambazo dawa na chanjo nyingine ambazo huwa mnazifanya kichaka chenu zimepitia. Kwa hiyo haiwezi kuwa salama kwa sababu hakuna anayejua juu ya usalama wake!

- "The Janssen COVID-19 Vaccine is an unapproved vaccine. In an ongoing clinical trial, 21,895 individuals 18 years of age and older have received the Janssen COVID-19 Vaccine"

Bwana/Bibi mjuaji umeisoma hiyo? Kama data anazo refer ni za ongoing trial, huoni kama hili linaloendelea pia ni sehemu ya hiyo trial? Maana hakuna aliposema trial imefikia mwisho. Kwa hiyo kwa akili zako, dawa iliyo kwenye majaribio inafaa kuwa mandated na serikali? Hivi hizo akili umepewa urembo ama? Yaani kabisa unalinganisha choo ambacho usalama wake tunaujua na hii chanjo ambayo wenyewe walioitengeneza wanakwambia kabisa iko kwenye majaribio yanayoendelea? Are you that dumb in any other area?

-"Blood clots involving blood vessels in the brain, lungs, abdomen, and legs along with low levels of platelets (blood cells that help your body stop bleeding), have occurred in some people who have received the Janssen COVID-19 Vaccine"

Kama una akili timamu mpaka hapa unapaswa kuwa mdogo kama dawa za mafua. Unajua athari ya damu kuganda kwenye mishipa ya Ubongo wewe? Au unadhani haya ni mambo ya ushabiki? Ukiona tunawaambia nyie kachanjeni tuacheni tulivyo, sisi sio vichaa!

- "Guillain Barré syndrome (a neurological disorder in which the body’s immune system damages nerve cells, causing muscle weakness and sometimes paralysis) has occurred in some people who have received the Janssen COVID-19 Vaccine. In most of these people, symptoms began within 42 days following receipt of the Janssen COVID-19 Vaccine"

Kausome huu ugonjwa halafu uje uniambie nani yuko tayari ku risk hii kitu kwa sababu ya Covid ambayo tumeumwa na kupona! Yaani nipate ulemavu wa kudumu kwa sababu ya chanjo? No way! Wewe kachanje tu bibi/bwana mjuaji, ila tuache kama tulivyo. Na hayo ni madhara waliyoyajua baada ya watu kuchanja ndani ya siku 42. Unajua madhara yake miaka 10 ijayo wewe? Aun una kiherehere tu kama kuku wa mdonde?

-"In an ongoing clinical trial, the Janssen COVID-19 Vaccine has been shown to prevent COVID-19 following a single dose. The duration of protection against COVID-19 is currently unknown."

Mpaka hapo kama una akili timamu unajua kwamba mko mnafanyiwa majaribio. Tunawashukuru kwa kuwa sehemu ya majaribio. Pengine mbeleni tutapata chanjo bora au mtaishia kupata madhara, hakuna anayejua. Lakini msilazimishe wengine tusioitaka hiyo chanjo. Na hapo wamekwambia kabisa hiyo chanjo inakukinga muda gani, hawajui. Sasa wewe ndugu kiherehere umeandika as if hiyo chanjo ni absolute protection, una akili kweli? Yaani aliyeitengeneza anasema hajui inakukinga kwa muda gani, halafu wewe chakujua ambaye hata maabara hujawahi ingia unaongea pumba tu.

Halafu unajifanya hujui kwa ni serikali imeifanya hiyari?

Kiufupi wewe na madiketa wenzako mnaoishauri serikali ilazimishe chanjo ni weupe kabisa kichwani. Msidhani sisi tulioamua kutochanja ni mazwazwa na wapumbavu. Tunawaangalia tu mnavyoropoka tunacheka. Kwa sababu muda mwingi hata mnachokisema hakina akili.

Serikali imeamua hii issue ni hiyari, nami naipongeza. Iendelee kuwapeni mnaoitaka chanjo na iendelee kuilinda hii hiyari ili tusioitaka tupewe uhuru wetu. Naiomba serikali iachane na vilaza wa aina yako wanaoishauri wakiwa hata hawajasoma walichoandika watengenezaji wa hizi chanjo. Hawa wakisikilizwa watalea chaos ambazo hazina msingi. Serikali isimamie hapo: Chanjo ni hiyari na anayetaka akachukue. Serikali isiingie kwenye mtego wa kulazimisha hizi chanjo. Naamini watakuwa wanafuatilia yanayoendelea duniani.

Tuna kazi ngumu ya kuujenga uchumi wetu, isikubali hii issue ya chanjo ituondoe huko!

Siku njema mjua yote!
 
Mimi nilichanja last Monday. Nilihakikisha mama yangu na mimi tunapata.

Hatukuhitaji process yoyote kufanya kwaajili ya kuchoma chanjo. Pako poa na hakuna msongamano kikawaida. Hivyo ilikua poa. Vitambulisho vyetu vya NIDA ndo vilikua muhimu tu.

Tulipumzika baada ya km dk 10 hivi tukaondoka.

Usiku mnene sana kichwa kiliuma mno. Lakini nilikumbuka zile reactions tulizoelekezwa hivyo sikuogopa. Ila kile kichwa hata panadol hakikua kinasikia. Asubuhi kulipokucha mdogomdogo nikaenda dukani kununua diclopar. Nilipomeza kikapoa. Nilimeza na kingine. Hakikuuma tena. Nikajisemea kwakua mamangu ana presha nisiongee kama kichwa kimeniuma sana usiku ili asije kuogopa.
Heh, tumekaa kidogo nikamsikia amesema kichwa kimeniuma usiku na hata sada ila hakiuma sanaa[emoji28][emoji28] nikacheka sana. Nami nikameambia hakika changu hata panadol hakikusikia. Basi tukapeana moyo ni zile reactions za chanjo.

Hakika kichwa kiliuma siku 2 tu. Baada ya hapo sina tena uoga. Nimekua balozi mzuri sana wa hili. Nasubiri nianze keenda moshi sasa nihudhurie kila msiba na kuhakikisha bibi yangu anachanjwa maana kuna vibarua wanapendaga kuja dowea bia kwa msheku sana wasiniulie msheku wangu maana hiyo delta hapo kenya wanaisomba mno hapo boda. Watu wasiogope wakachome.

Sitakufa leo nimechagua kufa kesho. Hata hiyo miaka 10 wewe una uhakika wa kufika?
 
Ni kwamba hayo maradhi uliyotaja ni baadhi tu ya vitu vye kushusha kinga za mwili kwa maana yapo mambo mengine yenye kufanya kinga zetu kuwa dhaifu, kwahiyo nachokiona hapo si suala la umri au kuwa na hayo magonjwa bali ni issue ya kinga za mtu husika, ndio maana nikauliza watot wadogo kinga zao ndio imara sana?

Kinga za mtoto haziwezi kuwa sawa na Mzee.
Ndy maana hata jua Kali la saa 7 mchana ,,Mzee atavaa koti la baridi.
Na hapo haumwi ila anahisi baridi..

Hivyo umri ni tatizo tosha kwamba covid inapenya kwa urahisi sana
Mambo mengine mm sio mtaalam na kujuwa zaidi.
Ila mm nawaamini scientists japo kuwa sio scientist.
 
Mimi ni miongoni watu waliochanjwa chanjo ya COVID-19 Johnson And Johnson siku ya pili tu baada ya zoezi la kuchanja kuzinduliwa na Rais

Nilijisikia yafuatayo:
1. Nilichanjwa kwenye bega la kushoto, sehemu niliyochanjwa nijisikia maumivu ya sindano kwa siku kama 3 hivi

2. Baada ya kuchanjwa nilijisikia kama kichwa kizito kidogo kwa siku kama 3 hivi

3. Nilijisikia kutaka kupumzika nyumbani nisifanye kazi kwa siku kama tatu hivi

4. Sikutamani kufanya tendo la ndoa kwa siku kama 5 hivi

5. Baada ya wiki moja kupita nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida na zaidi

6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiiana

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi

8. Nilitoa mbegu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiiana

9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo.

10. Tangu nichanjwe sijawahi kupata kikohozi, mafua

11. Kama Koo likinikereketa ilikuwa lazima nimung'unye lozenges au nimeze antibiotics ili nipone lakini juzi koo linikereketa likatulia lenyewe bila kutumia dawa yoyote.

12. Umakini (concentration yangu na busara zangu nahisi kama vimeongezeka kuliko awali.

Nadhani chanjo Iko pia, unaweza kuja kujutia kama chanjo zitaisha bila wewe kuchanjwa. Maana mwenye foleni tulikuwa na watu raia wa Ulaya na Asia wanahitaji kuchanjwa.
Mkuu mimi ijumaa nilichajwa juzi kati. Siku hiyo kuanzia jioni nilijuwa na homa the whole night lakini asubuhi yake ikaanza kupungua. Hadi jioni nikawa bie! Sasa hivi mimi na barakoa plus kitakasa mfukoni.
 
Back
Top Bottom