Watu hawajaanza kukataa chanjo tu bali walishagomea hata kuchukua tahadhari za kujikinga na hiyo corona yenyewe, pamoja na yote yanayozungumzwa kuhusu corona kuanzia kifo cha rais na viongozi, uhitaji wa mitungi ya oksijeni n.k ila bado watu wamegoma kuvaa barakoa,wamegoma level seat,wamegoma kunawa mikono, wamegoma social distance yani kwa kifupi watu wanaendelea na maisha kama hawajawahi kusikia kuhusu corona hata serikali imefeli katika hili.
Sasa sijui hapo mkuu unafikiri ni kipi ambacho kinafanya ufikiri kuwa itafika muda watu hao hao ambao wamegoma kuchukua tahadhari za kujikinga na corona watahitaji kuchanjwa?