#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

Sisi tumeletewa Johnson ambayo ni single dose ili tusipate tabu kufuatilia dose ya pili.
Kosa lilifanyika mwanzoni ambapo tuliembrace uongo na mambo ya ajabu kwasababu za kisiasa.
Idadi kubwa ya watanzania bado wana zile taarifa ambazo zilikuwa against njia za kitaalamu dhidi ya covid. Elimu iendelee kutolewa kwani watu wanaelewa japo taratibu sana.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ni suala la msimamo tu wa mtu maana hata hao wanaochanjwa wengi hawana elimu kuhusu hizo chanjo zenyewe,siku moja nimepanda daladala kulikuwa na mama ndio ametoka kuchanja kaingia kwenye daladala hana hata barakoa na anajipongeza kwa kuchukua uamuzi wa kwenda kuchanjwa, sasa nikajiuliza huyu mama baada ya kutoka kuchanjwa muda huo huo ndio keshaona amepata kinga dhidi ya corona ndio maana hakuona haja ya kuvaa barakoa au kwamba hakuona tu umuhimu wa barakoa kama walivyo wengine.
 
Ni kwasababu bado idadi ya walio na elimu angalau ya form four na kuendelea bado ni wachache sana kulinganisha na ambao wako chini ya hapo.
Hata elimu inayotolewa haieleweki, kazi ipo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
[emoji16][emoji16]hatuchanji
sema sichanji, hata mimi mke wangu alinikataza kwenda kuchanjwa, lakini nilichanjwa bila kumwambia, nilimwambia baada ya wiki moja kupita. Hii iko hata kwenye kupanga uzazi. wanaume wanawakataza wake zao kutumia njia za kupanga uzazi, lakini wanawake wanaenda kisirisiri kuchomwa sindano au kuwekewa vipandikizi bila waume zao kujua. Ulofa wako usiwe janga kwa mwenzio. Gwajiboy anataka msimamo wake uwe ndio msimamo wa waumini wake pia, ujinga wake uwe ndio ujinga wa waumini wake pia as if amewachukua ndondocha.
 

Kua kidogo basi, kwani Papa si Binadamu? Huo u papa ni cheo tu ila ubinadamu na hulka zote za kibinadamu ni zilezile.
Hakuna mkamilifu chini ya jua sote tumepungukiwa
 
Mzee umelipwa dolla ngapi kwa hili Tangazo
 
Kua kidogo basi, kwani Papa si Binadamu? Huo u papa ni cheo tu ila ubinadamu na hulka zote za kibinadamu ni zilezile.
Hakuna mkamilifu chini ya jua sote tumepungukiwa
Huwezi kuwa mcatholic mzuri kuliko Pope. Thamani ya Pope ni kubwa kulikoni ya mkatholic yeyoye duniani. Wasingekubali achanjwe kwa kubahatisha TU
 
Mzee umelipwa dolla ngapi kwa hili Tangazo
dunia imekubaliana kuchanja kama njia ya kukabiliana na covid-19, inawezekana imekosea au imepatia, na sio suala la kulipwa dolla. Wewe unahitaji kulipwa hela ili uchimbe choo na kukitumia? kuna watu walichimbiwa vyoo vya msaada lakini wakagoma kuvitumia, kuna uzi mwembamba sana unaotenganisha kati watu hawa wanaokataa kutumia vyoo vya msaada kuzuia kipindupindu na wewe unaekataa chanjo ya msaada kuzuia covid.
 
Tangu nichanje sijapata hata kikohozi, nadhani ambao hawachanji hawana hoja ya msingi.
 
Surua chanjo moja maisha yote na surua utaisikia redioni.
Ndui chanjo moja miaka yote na Ndui utaisikia redioni.
Manjano chanjo moja miaka yote! Na manjano utaisikia redioni.
Homa ya INI chanjo moja miaka yote na ugonjwa utausikia redioni.
Chanjo zote ni hivyo!
Tunauliza hii ya corona mbona wanasema hata ukichanjwa bado kunauwezekano wa kuambukizwa? Pia tunataka kujua inadumu muda gani?
Jiandae Ku boost mkuu!
 
shida zipo na hazitakwisha hadi ulimwengu utakapoisha, na Mungu ndiye mponyaji mkuu. Wanachokifanya wanasayansi ni kujaribu kupunguza adha kwako. Lakini, hata surua kuna wakati watoto na watu wazima waliochanjwa surua wanapata surua tena. corona ni ugonjwa mpya sana hivyo hata majibu yake ni machache kuliko maswali, Lakini waliochanja wameonyesha matumaini makubwa sana, hawajutii kuchanjwa. Wanasayansi wasiwe na hasira kuona wako watu hawapendi kuchanjwa covid kwakuwa hadi leo wako watu ambao wamekataa kutumia vyoo. Wamekataa vyoo sembuse chanjo!!! Tutaenda nao polepole mwisho watakubali tu, hata idadi ya kaya zenye vyoo imepanda polepole sana
 
Endelea kuamini hata visivyoaminika.
 
Hata wanasayansi walivyogundua kuvaa chupi ndani kuna watu walibisha mpaka leo hawavai chupi, lakini dunia inasonga mbele, ndiyo
Chupi yako aligundua mwanasayansi gani mkuu?
 
Ni kwasababu bado idadi ya walio na elimu angalau ya form four na kuendelea bado ni wachache sana kulinganisha na ambao wako chini ya hapo.
Hata elimu inayotolewa haieleweki, kazi ipo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Watu tunajichanganya TU na chanjo hii moja TU. Miaka yote na siku wapo watu ambao tunawaamini wanaofanya maamuzi kwa niaba yetu. Mfano, wako watu waliamua kwaajili yetu kuhusu chanjo za surua, polio, tetanus, TB, homa za manjano na ini pamoja na dawa za kutinbu magonjwa mbalimbali.

Hakuna mtu aliyehoji kwanini mwanawe anachomwa sindano ya kuzuia surua, je, watu walikuwa na elimu kuhusu hizo chanjo? Wanafahamu ni watoto wangapi waliopotea/kufa kwa kuchanjwa hizo chanjo?

mara hii kumetokea nini kiasi Cha kutowaamini watu walewale walioidhinisha kwetu chanjo na dawa tunazotumia tangu utotoni?
 
Siasa tu ndugu yangu. Kuna watu wanakomaa na legacy ndio wapanda miiba.
 
Siasa tu ndugu yangu. Kuna watu wanakomaa na legacy ndio wapanda miiba.
Hawa wanaosita kuchanja tunahitaji kufanya utafiti juu yao ili kufahamu shida yao ni nini, haiwezekani ulaya na marekani wamechanja watu wao kwa zaidi ya 60% wakati sisi hata zile dozi 1.5mil bado hazijapata watu zote kwenye taifa la watu 60 mil. Hii ni kuonyesha kuwa ama

1. elimu yetu haitoshi kwa kiwango kikubwa bado watu ni wajinga hata kama wamesoma, kama shida ni hii mitaala na walimu viangaliwe upya, au
2. Wananchi hawawaamini tena viongozi wao wa serikali kabisa baada ya kuwadanganya wananchi kwa muda mrefu kwa mambo mengi. kama shida ni hii serikali lazima ijitathimini, au
3. Wananchi wengi bado hawafuati hata njia nyingine za kuzuia maradhi kama vile kutoa vyoo, kuchemsha maji ya kunywa, kutumia kondom, kufanya mazoezi, kupanga uzazi, au
4. Elimu ya chanjo hii na ugonjwa huu haijatolewa vya kutosha, au
5. Serikali amekosea sana kuficha ukubwa wa covid kwenye jamii na kuwaruhusu wananchi wawasafirishe na kuwazika hata waliokufa kwa covid kwa njia za kawaida tu, hivyo wananchi wanashindwa kuhusianisha (clue) vifo kwenye familia, ukoo na mitaani na covid 19. Kama shida ni hii serikali imekosea sana kuruhusu maziko ya waliokufa kwa covid kufanyika kwa njia za kawaida.

Hatuoni aibu kukutana na viongozi au kwenda kwenye mataifa ambayo viongozi wao wamewachanja wananchi wao kwa zaidi 60% wakati sisi hata dose 1,500,000 hazijakwisha bado. Viongozi wetu wanashindwa hata kusafisha mitaa ya miji na kuachia machinga wanachafua kila pahala, wanaogopa kuwaondoa sehemu walizovamia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…