#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

Sasa Mnataka Watanzania wote tuchanjwe. Je, kama Chanjo inashida kwahyo Tanzania nzima tuumwe?
Nyie wengine Chanjeni na Wengne tusichanje ili kukiwa na Shida sisi tuwape msaada.
 
Shida inakuja hizo chanjo za surua, ndui, nk tulichoma mara moja tu. Mliochanjwa wala msiwe na shaka tunasubiri majibu kutoka kwenu baada ya miaka miwili au mitatu zen na cc ndiyo tutaamua tuchanje ama la, ni kama ndui tu na chanjo zingine kuna baadhi ya watu walizikataa lkn matokeo yake yakawa mazuri basi jamii ikazikubali, so wala msihofu na kutuona wajinga cz wasi wasi ndo akili mkuu.
 
Tumeshasema, hatuko tayari kufanyiwa majaribio, hizi mbini uchwara hazitasaidia, ifike mahala mtuelewe jamani
Jisemee mwenyewe mkuu (kivyako), kila mtu atakufa kivyake kwa sababu zake.
 
Aisee hukusikia dalili zozote za uzombi mkuu tuambie ukweli tu
 
Tumeshasema, hatuko tayari kufanyiwa majaribio, hizi mbini uchwara hazitasaidia, ifike mahala mtuelewe jamani
Kuna msela alikuwa mbishi balaa.Zilipokuja hiz chanjo za serikali alidengua dengua.Kilichotokea sijui ila nasikia anaingia wiki ya 2 sasa bado yuko hospitali flan ya private kwenye mitambo ya hewa.Nasikia kumbe hata Bima haitumiki kutibu covid na mitungi ya gesi.

litapita bakula la kuomba msaada soon
 
Wanasema ukichanja bado uvae barakoa, uepuke mikusanyiko, unadhani ni kwanini?
 
hapo kwenye nguvu za kiume, utatukamata wengi.
 
Mwenyewe chanjo imeningezea nguvu kupita maelezo nisiwe mnafiki
 
Hutupati hata useme inaongeza nguvu za kiume
 
Nakubaliana na wewe, ndio maana inatubidi tupate chanjo ili kuepuka severe infection. Labda hukuelewa comment yangu ya awali.
Kweli aombe Mungu ndugu zake kijijini wasipate corona
 
Maswali kadhaa kwako Mkuu
1.ULIPIMWA KWANZA KUJUA KAMA TAYARI UMESHA AMBUKIZWA NDIPO UKACHANJWA? AU ULICHANJWA TU ?
2. NA JE IKIWA TAYARI UNA MAAMBUKIZI UNACHANJWA AU HUCHANJWI?
3. NA JE UKICHANJWAN UKIWA TAYARI ULISHAPATA MAAMBUKIZI NINI KINATOKEA??
 
Haha, hata mimi sikumwambia ndugu yangu yeyote kama nimechanja hadi ilipopita wiki moja na kujiona niko fit sana, yaani hata concentration yangu imeongezeka sana, hata ninapoendesha gari najisikia niko focused kuliko mwanzo. Niliendesha gari Toka Arusha hadi Dar bila kuchoka Wala kuhama barabarani. Yaani siku 3 za kwanza nilijisikia viungo vyote vinaguswa na chanjo kuanzia ubongo, UTI wa mgongo, kiuno, utumbo, ini, nk. Hii chanjo Ina uwezekano wa kutibu magonjwa mengine pia bila kukusudia.
 
Sasa Mnataka Watanzania wote tuchanjwe. Je, kama Chanjo inashida kwahyo Tanzania nzima tuumwe?
Nyie wengine Chanjeni na Wengne tusichanje ili kukiwa na Shida sisi tuwape msaada.
Ukibaki hai peke yako utakuwa na faida gani?; Hapo ulipo walikuchanja machanjo kibao, hata ukichomwa na msumari utakimbilia chanjo ya tetanus, watakupata TU kama wakikukusudia
 
Mama Yetu, Rais na Amri Jeshi Mkuu Mama Samia kasema kuchanja ni hiari, na yeye kasema hawezi kuleta kitu cha kuua raia wake (ingawa hapa kidogo kapotoka maana hizi dawa ni za majaribio kwa 100%).
 
Kwa jinsi ulivyoelezea umenishtua sana haishindikani badae kutokea side effects zingine ni Bora zikawa positive zikiwa negative je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…