Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilipomaliza chuo nilizunguka sana kutafuta AJIRA hasa kwenye majiji makubwa kama mwanza, Dodoma na na Daressalam huko kote niliambulia holaaaa, nilikaa nikafikiria sana nikaona sehemu pekee ya kwenda kutafuta maisha ni mikoa ambayo haijaendelea kwa sababu ushindani katika sekta ya ajira unakuwa ni mdogo na uhitaji unakuwa ni mkubwa pia, nikaona Bora niende tabora huko nilifanikiwa kupata ajira japo nilikuwa nalipwa mshahara mdogo sana..Mimi ni mtaalamu wa Afya ya binadamu japo kwa sasa najishughulisha na biashara niliisha Toka huko....soko la ajira aliliharibu zaidi magufuri likawa gumu balaa......Mtu mzima na akili zako timamu unawezaje kuishi tabora?
Akaanza kunipigia na ule ukuni sehemu za mabegani huku mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea
Tunafuata Quran na Sunna kama mtume Muhammad alivyotufundishaMaulamaa huwa wana complicate sana vitu,si unaona kukojoa tu mpaka akunje suruali
Hii sentensi iliniumiza kiasi ndio maana sikuweza kuipotezeaUmeharibu ulipoelezea kuwa polic walikuambia wewe ni mrembo,,,,, ni sawa pengine uliambiwa hivo, haka ka -segment ungekaruka ili kulinda uanaume wako ,,, !! Hongera Shombe
Usichokijua ni sawa na usiku wa Giza....pale nilikuwa kwenye himaya ya watu ningejifanya ngarambe wangeniuwa.....Huyu mwanamke ilitakiwa umchape ngumi mbili tatu, na mtama mmoja matata sana in the act of self defense...
Haiwezekani mtu anakushambulia then unajitetea kizembe...
Kasome kwenye google sifa za mtu mwenye" obsessive personal behavior."..Dah nmecheka sana 😂
Vitu vidogo tuu wanaenda na maandiko bc n sahihi kabisa kuitwa mwizi
Huyo mama aliyekuita mwizi hukumtafuta?Ni miaka 15 sasa imepita tangu ninusurike kuuawa na walimwengu. Nilikuwa nikiishi Tabora, na jioni moja, nilikuwa natembea mjini Tabora. Wakati natembea, nikajihisi kubanwa haja ndogo, nikawa nakatiza mtaa wa Salimini. Kwa wale wenyeji wa Tabora, mnafahamu ule mtaa ulivyo wa Kiswahili. Nikawaona niingie kwenye nyumba moja mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo (chooni).
Nje ya nyumba ile alikuwa amesimama kijana mwenye umri wa miaka 18 au 19, nilimuomba na akaniielekeza nipite kwenye korido niende mpaka uwani. Wakati napita kwenye korido, nilikutana na mwanamke na mwanaume wakiwa wanazungumza. Niliwasalimia, na mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea uwani. Nilipofika uwani, kabla ya kuingia chooni, nikawa ninakunja suruali yangu mpaka ukaribu na magotini (kawaida yetu Waislamu huwa tunafanya hivi ili utakapokuwa unajisaidia haja ndogo, zile cheche za mikojo zisirukie nguo). Ghafla nilisikia sauti ya mwanamke ikitokea nyuma ikiita "mwiziiiiii, mwiziiiiii."
Ile kugeuka, namuona yule mwanamke niliemuona kwenye korido anakuja mbio huku akakamata kuni. Akaanza kunipigia na ule ukuni sehemu za mabegani huku mimi nikihangaika kupangua kile kipigo na kujitetea kuwa mimi sio mwizi. Yule mwanamke alipoona ananipiga na ukuni na mimi sianguki, akabeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto ili animwagie usoni. Dah, lahaula! Akatokea yule mwanaume aliyekuwa nae akamuambia "achaaaaa!" Kujinusuru, nilibidi nirukie kwenye korido nitokee mlango wa mbele ili nikimbie (hapa nilifanya kosa kubwa). Nilianza kukimbia barabarani huku yule mwanamke akiendelea kuita "mwiziiii, mwiziiiiii."
Watu wakaanza kunikimbiza. Kadiri nilivyokuwa nakimbia, watu walizidi kuongezeka, huku wengine wakiwa wamebeba mapanga. Niliingiwa na fikra za haraka za kuingia kwenye nyumba ya mtu ili ninusuru maisha yangu. Bahati nzuri, nyumba ile niliyoingia ilikuwa ya mjumbe wa serikali ya mtaa. Alichokifanya yule mjumbe (mwanamke wa makamo) aliniambia niingie nijifiche chumbani na yeye akafunga mlango. Lile kundi la watu wenye mapanga walifika kwenye nyumba ile niliyokuwa nimejificha na wakaanza kumlazimisha yule mjumbe anitoe nje huku wakiimba "tunamtaka mwizi weeetúu."
Yule mjumbe alisimama mlangoni na kuwaambia wale watu, "Simtoi nje huyu kijana, ila nitakachofanya, napiga simu polisi waje wamchukue, mtamkuta kituoni." Hii ndiyo ilikuwa salama yangu. Haikupita masaa mawili, walikuja polisi na kunichukua kwenye gari lao. Polisi mmoja alinipiga vibao huku akisema, "Kumbe jamaa mwenyewe mrembo!" (Mimi nina asili ya ushombe shombe kwa mbali).
Nilipofikishwa kituoni, nilijieleza kwa ufasaha na pia nikatoa vitambulisho vyangu ili viwe ni uthibitisho wa kile nilichokizungumza. Bahati nzuri, mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja, nikatoa 30,000/- nikawapa wale askari, wakawa wameniachia niende nyumbani usiku ule na kesho yake niende kuripoti. Kesho yake niliripoti polisi, na askari walinikabidhi vitambulisho na kuniambia hakuna kesi. Nikaendelea na majukumu yangu.
Afu inawezekana hapo ulipo unakula kitimoto, unakula wake za watu, unabet, unashabikia mpira 😂Tunafuata Quran na Sunna kama mtume Muhammad alivyotufundisha
Mambo yasiwe mengi, nambie wwKasome kwenye google sifa za mtu mwenye" obsessive personal behavior."..
Acha uvivu mkuu...hiyo simu yako ukiwa na bando lako la internet unakuwa na kila kituMambo yasiwe mengi, nambie ww
Usichokijua ni sawa na usiku wa Giza....pale nilikuwa kwenye himaya ya watu ningejifanya ngarambe wangeniuwa.....
Huko kote niliishapita....naishi maisha ya kumcha munguAfu inawezekana hapo ulipo unakula kitimoto, unakula wake za watu, unabet, unashabikia mpira 😂
Sina bandoAcha uvivu mkuu...hiyo simu yako ukiwa na bando lako la internet unakuwa na kila kitu
Ukiwa nje ya uwanja ni rahisi sana kuyaona makosa ya mchezaji.....ingia wewe uwanjani ndio inakuwa kimbembe😁Kulikuwa na watu wawili tu walioleta ukuda, ujasiri wako ungewatia uoga...
Pia umetaja kwamba uliingia ndani ya nyumba hiyo kwa kuomba, hivyo kungekuwa na watu wa kukutetwa...
Unamkata huyo mwanamke ngumi ya shingo, na pua, mtama ukimsindikiza na maneno "***** mimi sio mwizi nimeomba kuja kutumia choo"...
Kamata huo ukuni mtishie kumchoma mdomo wake kama akiendelea kuleta zogo...
Mtaa wa Salmin ambao Rc Mwanri aliuita Toronto na weekend ukawa unafungwa kuruhusu wachuuzi kufanya biashara.Ni miaka 15 sasa imepita tangu ninusurike kuuawa na walimwengu. Nilikuwa nikiishi Tabora, na jioni moja, nilikuwa natembea mjini Tabora. Wakati natembea, nikajihisi kubanwa haja ndogo, nikawa nakatiza mtaa wa Salimini. Kwa wale wenyeji wa Tabora, mnafahamu ule mtaa ulivyo wa Kiswahili. Nikawaona niingie kwenye nyumba moja mtaani hapo ili niombe sehemu ya kujisaidia haja ndogo (chooni).