Nilivyopata pesa nyingi nilipokuwa askari wa TANAPA

Nilivyopata pesa nyingi nilipokuwa askari wa TANAPA

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello

Nilivyomaliza kidato cha 6 kulingana na hali yangu ilinilazimu nikatae na kusitisha mipango ya kusoma chuo kikuu.

Target yangu ni kufukuzia ajira za uhamiaji, TISS au PCCB. Yaani nilikuwa naota taasisi hizo tu. Sasa kulingana na maisha ya kifukara na uyatima (Mimi si yatima kabisa nina wazazi wote ila hawakuwa na msaada kwangu). Nikajikuta nimekimbilia ajira ya TANAPA kama Askari wa wanyama (game ranger).

Nikapangiwa kazi Kambi moja iko Porini kwenye hifadhi ya Serengeti karibu na uwanja wa ndege ambao unatumika kuleta watalii, sometimes hata wafanyakazi wa hotel zile nzuri nzuri za maporini huutumia kupanda ndege.

Sasa tulikuwa na shift ya mwezi kwenda kulinda hoteli zilizopo kwenye ile hifadhi. Sasa nilipangiwa Four seasons hotel (Bilila) ikawa kazi kubwa ni kuchukua SMG yangu na kuwapa escort matajiri Wazungu kwenda kufanya sherehe zao maporini. Mara nyingi zilikuwa Sherehe za harusi. Wengine walifungia harusi angani ndani ya balloon wengine chini tu.

Sasa nilikuwa nawavizia saa 12 kasoro jioni nawapa taarifa kuwa muda umeisha wajiandae kurudi hotelini.
Ikitimia saa 12 kamili nawaambia time is over chukua chako twende. Basi hapo napewa dolari nawapa time wamalizie sherehe zao za ulevi.

Sasa mkirudi hotelini wale Wazungu ni kama niliwatupia uchawi hivi kumbe ni neema tu za Mungu. Wakiniona wananipa much respect na kufinyiwa midola.

Nilikuwa nikimaliza 30 days ile posho yangu ya laki 6 naiona chamtoto tu na karibu yote nilikuwa nawarushia ndugu na marafiki.

Nilikuwa natoka na milioni zaidi ya kumi kwa mwezi game likikubali. Sasa nikawa na pesa nyingi, sina mke, sina mtoto, account ya ziada (ya siri ikawa ina milioni 48 ) ndani ya miaka 2.

Nikaacha kazi.

Hii ilikuwa kati ya 2013-2015.
 
Back
Top Bottom