Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Mleta mada ungetuletea na picha za ulivyo pabadilisha huko kwenu Mwanza nasi tukaifata nyayo zako zako ungekua umefanya la maana sana.
 
Sio lazima kuishi kama wao inawezekana tunavyoishi kwa msongamano ni kivutio tosha kwa nchi nyingine kuiga wakidhani ndo utamaduni wetu

Tunakubali ni kweli tunamapungufu yetu lakini pamoja na yote bado tunaona sio sawa na tulipokua,ITOSHE KUSEMA TANZANIA NI YETU NA SISI NDO WATANZANIA WENYEWE KUA MZALENDO PENDA TAIFA LAKO

Kwa hyo Tanzania ni yetu sote hta kama kuna mapungufu tusiseme?

Kwa hyo unakubaliana na Hali ya uchafu na ujenzi holela uliopo kwenye miji yetu?
 
Mkuu, hiyo miji uliyoitembelea na kuweza kuona ubora wa mpangilio wa majengo na miundombinu yake haikufanyika kwa muda mfupi. Ilikuwa ni kupitia jitihada kubwa na kwa karne kadhaa ndipo yote hayo uliyoyaona yaliweza kufanyika.

Muda wa miaka minne uliyoishi ughaibuni haikupi "justification" ya kuponda maendeleo hata kama ni madogo ya nchi yetu yalipofikia. Ni lazima tujifunze kuthamini vya kwetu, kwa kuwa maendeleo ni kama zoezi la kupanda ngazi, ili ufike juu ni lazima uanzie chini.
 
Vip kijijini kwenu?kukaa ulaya miaka minne unatukoromea wakati inawezekana kijijini kwenu Bibi ako anaishi kwenye msongee
 
Tatizo hujawahi kufika Marekani ,ungemuuliza na Harlem,Manhattan je
huko nasikia ni balaa si ndio lile poem la landlord landlord.my roof has l
sprung a leak.
mshair langhston hughes anaonesha namna maisha mabov ya black s huko.
huyu jaamaa limbuken kabisa ina mana anashindwa kulala et dawa ya.mbu.asa alitegemea nin katila nchi za ukanda wa kitropik.huku joto sio sawa na huko virginia maryland.jinga
 
Ni ukweli mtupu ukisoma kwenye history 2,, vitu vinavyofanyika sasa hivi ni vya mwaka 1870 ndiyo tunafanya sasa,, nashangaa viongozi wanashindwa hata kukopi huko nje wenzetu wanavyofanya,, tumebaki tukiwalaumu eti wapinzani walituchelewesha, wakati Uhuru mpaka sasa kinaongoza chama kile kile,,
 
Labda kwa sababu ya ugeni tu ungekuwa unajua ungesafiri moja kwa moja mpaka Chato International Airport hakuna tofauti na ule wa Dubai baada ya hapo ungeingia mji kama Ulaya ungejikuta uko nyumbani kabisa tofauti wenyeji ni Wasukuma. Siku nyingine ukija toka utokako nenda moja kwa moja mpaka Chato International Airport baada ya hapo ukatalii Burigi National Park, utapata mengi ya kusimulia ukirudi kwenu.
 
huko nasikia ni balaa si ndio lile poem la landlord landlord.my roof has l
sprung a leak.
mshair langhston hughes anaonesha namna maisha mabov ya black s huko.
huyu jaamaa limbuken kabisa ina mana anashindwa kulala et dawa ya.mbu.asa alitegemea nin katila nchi za ukanda wa kitropik.huku joto sio sawa na huko virginia maryland.jinga
Waafrica ukweli huwa hatutaki kuambiwa, tunataka tusifiwe kinafiki
 
Kwa hyo Tanzania ni yetu sote hta kama kuna mapungufu tusiseme?

Kwa hyo unakubaliana na Hali ya uchafu na ujenzi holela uliopo kwenye miji yetu?
mtoa mada amejigamba kwa kutoa kasoro nyingi zenye dhihaka ndani yake ukiwa kama mtanzania mwenye uzalendo wa kweli chukua changamoto tulizonazo tuzibadilishe kua fursa inawezekana mmoja akija na idea ya kutatua kero za uchafu tulionao na serikali ikatoa surport kwa sehemu inapobidi ingewezekana kabisa tungeondoa tatizo,na sio kutupiana mipira

usipowajibika ww kwa kuona changamoto na ukadai wengine ndo walitakiwa kufanya uon kama umejikita kwenye malalamishi na sio suluhu

TANZANIA NI YA KWETU USIMTUPIE MPIRA MWINGINE AUCHEZE VIZURI WAKATI WW UNATOA PASI ZA OVYO
 
Wakati mwingine ujitahidi pia kutembelea stendi yetu mpya ya kimataifa ya Mbezi! Tumelazimishwa kuiita stendi ya magufuli! Utajionea mwenewe wanyonge wanavyo fanya biashara ndani ya hiyo stendi bila bughudha!

Hutokuja uuone huo utaratibu sehemu yoyote ile duniani zaidi ya huku kwenye nchi yetu ya wanyonge.
Kwa suala la bus station nadhani waTanzania tuko vizuri, sijatembelea hiyo, lakini kama imejengwa kwa ubora unaotakiwa basi tutakuwa tunazizidi nchi za ulaya kwenye eneo la Bus station maana huku sijaona bus station ya maana. Hata ile ya Paris bado hawatufikii ukilinganisha na yetu.

Nadhani Ulaya bus station za masafa marefu hazipewi umuhimu sana kama ilivyo Tanzania.

Hiyo ya Mbezi NAIONA KWENYE PICHA TU.
 
mtoa mada amejigamba kwa kutoa kasoro nyingi zenye dhihaka ndani yake ukiwa kama mtanzania mwenye uzalendo wa kweli chukua changamoto tulizonazo tuzibadilishe kua fursa inawezekana mmoja akija na idea ya kutatua kero za uchafu tulionao na serikali ikatoa surport kwa sehemu inapobidi ingewezekana kabisa tungeondoa tatizo,na sio kutupiana mipira

usipowajibika ww kwa kuona changamoto na ukadai wengine ndo walitakiwa kufanya uon kama umejikita kwenye malalamishi na sio suluhu

TANZANIA NI YA KWETU USIMTUPIE MPIRA MWINGINE AUCHEZE VIZURI WAKATI WW UNATOA PASI ZA OVYO
Mimi nadhani nimewajibika kutoa tathmini ya maendeleo ya nchi yetu kipindi mimi niko nje.

Ukisoma vema mada yangu utaona nimeponda, lakini pia nimesifia nilipoona panastahiri.

Wenye mamlaka wachukue kama changamoto ili kupanga miji yetu.

TUTAFIKA
 
Ni mawazo mazuri, lakini mkuu Hivi Kampala kuna Flyovers? Kuna sehemu umesema ile ya Kijazi kwa Kampala ni kichekesho!
 
Ndugu unasifia miji ya Ulaya iliyojengwa na wanaume wenzako? Rudi bongo ushiriki kujenga nchi yako.

Ni kweli miji ya Tanzania haikupangwa vizuri, nyumba zake si za kisasa, na kadhalika na kadhalika. Lakini ndio hivyo tulikotoka ni mbali na bado tunasonga mbele kivyetu vyetu. Siku hizi tunae kiongozi anaetufundisha kwa mfano wake mwenyewe kupitia kutosafiri nchi yoyote ya Ulaya: kwamba penda vya kwenu, sifia vya kwenu, acha kusifia vya wanaume wenzako.
 
Hongera kwa kuishi Ulaya na kuiona Tanzania haifai. Kwanza umeanza kupondea hotel uliyoichagua mwenyewe. Hakuna alie kulazimisha. Unapofanya booking ktk hotel siku hizi ktk mtandao utaoneshwa vyumba na mazingira ya hotel. Hii inaonesha japo waishi Ulaya hujui namna ya kupata hotel zilizo na huduma safi. Tanzania kama ilivyo pia Ulaya swala la hotel ni fedha yako. Ungeweza kufikia hotel zilizopo mazingira mazuri yaufukweni upate hewa nzuri. Ni fedha yako tu.

Na pia nakushangaa hujui hata mazingira ya kijografia baina ya Ulaya na Tanzania. Tanzania kama zilivyo nchi za tropik kuna mbu tena wanao eneza malaria ndo maana katika maeneo yenye mbu wengi yaliyo na msongamano kama huko ulikofikia hutumia net au chandarua.
Ulaya hakuna net kwa sababu ni nchi za baridi uwezi kuta mbu. Hata hivyo wakati wa Summer uwa kunakuwa na wadudu na mbu wasio na malaria baadhi ya maeneo ya Ulaya. Hii ulazimika watu kupakaa dawa za kuzuia wadudu wasizuru mwili.

Inaonesha ulivyo fika hapa kwa uchumi wa kubana na kukaa maeneo ya uswahilini. Tena umefikia karibu na uwanja wa ndege ili upunguze gharama ya tax kuliko ungefikia hotel za Masaki. Nambie Huko Ulaya kwenu, na hotel zetu za ufukweni ni hotel gani zina madhari nzuri na white sand beaches? Hotel nyingi za Ulaya kwa nje hazina mvuto kabisa. Unakuta ni jengo tu lipolipo mpaka uingie kwa ndani ndo unajua hii ni hotel kali.

Umeenda kijijini kwenu, je huko kukoje? Ni mchango ngani umetoa kuboresha hata nyumbani kwenu. Mtu unapojidharau mwenyewe utadharauliwa. Usidhani Ulaya watakuona wewe si Mtanzania. Bado wanakuona weye ni mweusi ulietoka Afrika kwenye dhiki.

Kikubwa ulitakiwa kutoa maoni si kuanza kukashifu. Kusema umasikini umejaa. Wewe mwenyewe masikini kwenda kulala vijihotel vya hali ya chini, ukiacha hotel kubwa zenye hadhi. Nenda huko Serengeti kaangalie Hotels zenye hadhi ambapo watu mashuhuri duniani kama akina Bill Gates, Will Smith, Barak Obama na wengine wengi ufikia.

Tanzania ni nchi inayoendelea uwezi linganisha kabisa na Ulaya ambako maendeleo yalianza toka karne kadhaa zilizopita. Tanzania ni ya miaka ya 60. Tutajivuna kwa vichache. Ningekuwa mimi ni wewe ningetembelea baadhi ya halmashauri na kukutana na viongozi na kutoa mawazo napia kama nimekaa Ulaya kipindi hicho chote ningekarabati hata darasa moja. Kama wafanyavyo mwanamitindo Flavian Matata, na pia hata Miriam Odemba.

Karibu tena Tanzania uje utushauri kwa vitendo. Na acha kufikia Uswahilini. Ukitaka ufahari fikia hata pale Kunduchi Beach hotel, au Ramada Resort huko hakuna net ndugu yangu. NAIPENDA NCHI YANGU NITABAKI KUJIVUNIA NCHI YANGU TANZANIA. Mkataa kwao ni mtumwa.
 
U
Akuache wewe na nani, sisi pia umechoka na hizo kalele za viongozi kumbe hata Kenya hatuwafikii sasa kwetu mbona kelele hivi? Mbona Kenya hatuyasikii haya, Asante sana Baharia kwa kututowa tongotongo
Unajua sie Watz huwa hatupendi mtu anaejaribu kushauri au kuwaambia ukweli, matokeo yake huwa ni kuishia siku zote kutukana au kurusha ngumi...mie sijaona sehemu ambayo jamaa kaikana nchi yake bali maoni yake, ni kujaribu kufanya comparison kati ya home country Tz Vs nchi nyingine alizotembelea, na kujaribu kukumbusha kwamba, bado tuna safari ndefu, na vitu tunavyoona kama tumefanya wonders, ni vitu vya kawaida sana kwa nchi za wenzetu, na wala hatuhitaji kupiga makelele mengi wakati tunafanya hayo.
 
Kwa suala la bus station nadhani waTanzania tuko vizuri, sijatembelea hiyo, lakini kama imejengwa kwa ubora unaotakiwa basi tutakuwa tunazizidi nchi za ulaya kwenye eneo la Bus station maana huku sijaona bus station ya maana. Hata ile ya Paris bado hawatufikii ukilinganisha na yetu.

Nadhani Ulaya bus station za masafa marefu hazipewi umuhimu sana kama ilivyo Tanzania.

Hiyo ya Mbezi NAIONA KWENYE PICHA TU.
Bus station za nini sasa kama hapo Mbezi. Stand tunapita tu. Ulaya wanafikiria mbali.
 
Back
Top Bottom