Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ajabu nami nikawa nahisi anaweza kuwa ndio yeye amekuja kivingineParabola
Watanzania kwanini huwa mnakuwa wakali mkiambiwa ukweli.Limbukeni akioneshwa mwezi hujidai yeye ndiye mwanzilishi wa kuona mwanga; ulichokielezea kinasadifu na laiti kama mzazi wako anakaa kijijini akisoma hiki alichokiandika hawezi kukuruhusu kurudi hata kuona kaburi lake ABADI.
Ni bora upotelee huko huko ulikolowea kuliko kubagaza taifa lako. Usiache mbachao kwa msala upitao. Huna mfano boara wa kuigwa na yeyote anayetafuta kutoka katika maisha yaliyojaa changamoto.
Wanaokutumia kwa kukulipa pesa ambazo hujui zimetokana na nini ndio waliokujaza kiburi ambacho kabla hujarejea ukimbizini utarejea kwenye jukwaa hili kuomba msamaha.............
Wabongo tukiambiwa ukweli tunalialia Sana.Duuu!! Acha ujinga tulipoachiwa na wakoloni wasomi na matajiri wale unspajua?. Ni wapi???
Wewe hapo umefanya nini kwenu. Tuanzie kumjengea babako??
Weka picha!!! Siyo unasema sema tuu!!
Kwani sisi lazima tuwe km ulaya? Dar yetu Bongo land haivunjwi na tutarudi tu kutoka huku tuliko ndo tulivo ukome kuisemasema!!!
Kwenu tu bado mnalalia nyumba za tembe!!! maskin bana???! Umeotea kisafari unaleta za kuleta hapa.!!!
Mtuache. Mfugale si mchezo? Kigamboni weee!
Kampala zipo, zaidi ya 15, ukitaka kuziona usiingie katikati ya jiji ukiwa unatokea Masaka, nenda moja kwa kwa njia ya pembeni ukiwa unaelekea Namboole Mandela Stadium.Ni mawazo mazuri, lakini mkuu Hivi Kampala kuna Flyovers? Kuna sehemu umesema ile ya Kijazi kwa Kampala ni kichekesho!
Nairobi nimekaa miezi 3. Napajua kila kitu. DSM kwa Nairobi inabidi tujipange. Huu ndiyo ukweli japo ni mchungu sana.Mtoa mada unachekesha yaan kwenye hii Africa Kampala na Nairobi ndo za kutolea mfano? kwanza unaijua nairobi wew huwa ukisikia kibera haraka haraka unafikiria ni kongo
Huna unalojua kilaxa wewe.
====
Huyo rafiki yako muonyeshe hizi clip kwa kuanzia.
Kuna wakati nilikuwa na jamaa waliotoka Ulaya. Tulikuwa kwenye chopa iliyokodiwa toka South Africa. Wale bwana ilikuwa mara ya kwanza kutembelea nchi ya Afrika, nje ya Afrika Kusini.Kuna rafiki yangu mmarekani aliwahi kaniambia Mnawezaje kuishi sehemu mko congested namna hii
Kwanini tunapiga kelele kwa vijiendeleo kidogo tunavyovishuhudia katika nchi yetu? Tunafanya hivyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watanzania (na waafrika kwa ujumla) tumezoea kusikiliza negative publicity kuhusu nchi zetu, watu wetu na maisha yetu kwa ujumla.U
Unajua sie Watz huwa hatupendi mtu anaejaribu kushauri au kuwaambia ukweli, matokeo yake huwa ni kuishia siku zote kutukana au kurusha ngumi...mie sijaona sehemu ambayo jamaa kaikana nchi yake bali maoni yake, ni kujaribu kufanya comparison kati ya home country Tz Vs nchi nyingine alizotembelea, na kujaribu kukumbusha kwamba, bado tuna safari ndefu, na vitu tunavyoona kama tumefanya wonders, ni vitu vya kawaida sana kwa nchi za wenzetu, na wala hatuhitaji kupiga makelele mengi wakati tunafanya hayo.
Kampala zipo, zaidi ya 15, ukitaka kuziona usiingie katikati ya jiji ukiwa unatokea Masaka, nenda moja kwa kwa njia ya pembeni ukiwa unaelekea Namboole Mandela Stadium.
Au ukiwa unaenda Entebbe airport basi nenda na Express Road from city centre.
Nairobi nimekaa miezi 3. Napajua kila kitu. DSM kwa Nairobi inabidi tujipange. Huu ndiyo ukweli japo ni mchungu sana.
Duh, hiyo ni miaka minne tu ya kukaa ulaya unakuja na maneno ya shombo kiasi hicho!? Hivi nani aliyekuroga wweee mwana usi kwenu!Shalom,
Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.
Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa Ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya Ujerumani. Pia ili kukidhi haja ya moyo wangu nimetembelea karibu miji yote mikubwa na midogo ya nchi ninayoishi. Pia nilibahatika kutembelea Tel Aviv na Jerusalem nchini Israel. Kwa ujumla matembezi yangu yameniwezesha kujionea landmarks muhimu karibu yote kwenye nchi nilizotembelea. Pia kwa kuwa, mbali na safari ya London, Oslo na nchini Israel ambapo nilipanda ndege miji yote iliyobaki nilisafiri kwa bus ambapo nilipata furasa ya kuiona Ulaya kwa undani zaidi hasa highways. KWA UFUPI ULAYA IMEUNGANISHWA NA BARABARA NZURI SANA NA ZENYE UBORA WA HALI YA JUU KABISA. KUNA RAHA YAKE KUSAFIRI NCHI ZA ULAYA KWA KUTUMIA BARABARA.
Baada ya utangulizi sasa naeleza nilivyoiona Tanzania baada ya kutua Dar es Salaam.
1. Kwa kuwa tulitua usiku, haikuwa ajabu sana kuiona Dar es Salaam mfano wa nyota za angani ambazo huwa hazina mpangilio maalum maana naijua vema na hata kabla sijaondoka kwenda ng'ambo nilitua na kupaa mara kadhaa kwa safari za ndani, nilijua DSM ina mipango miji mibovu inayofanya nyumba kujengwa bila mpangilio na hivyo usiku kuonesha taa zilizozagaa kama nyota angani. TOFAUTI KABISA NA UNAVYOSHUKA USIKU KWENYE MIJI MINGINE DUNIANI AMBAPO UTAONA NAMNA BARABARA ZA MITAA NA HIGHWAYS ZILIVYOPANGWA, NA HATA TAA ZA MJI KUWA KWENYE MPANGILIO MAALUM. Tofauti na nilivyouacha uwanja wa ndege. WALAU MARA HII TERMINAL 3 KWA MBALI SANA NILIKIRI INAONDOA AIBU TULIYOKUWA NAYO, LAKINI HATA HIVYO NILIONA KAMA BADO NI NDOGO SANA.
2. Baada ya kutua na kuvuka SECURITY control nilitoka nje na kukutana na dereva wa "hotel' niliyofanya booking kwa njia ya simu baada ya kuiona kwenye booking.com, haiko mbali sana na airport, nikili wazi njia nzima kuelekea hotelini, nikiwa na picha ya miji ya Ulaya kichwani, niliona mji kuwa ni masikini na mchafu kupindukia. Hotel yenyewe niliyolipia laki moja ambayo kiukweli ni hela ndogo sana kwa Euro niliikuta ni ya hovyo, chumbani nilikuta kuna neti ya mbu hiki nacho kilinistua maana Ulaya sikuwahi kulala na neti, pia nilikuta chumba kimepuliziwa dawa ya mbu. PALINISHINDA ILIBIDI NITAFUTE SEHEMU NYINGINE YA KULALA.
3. Kesho yake asubuhi nilisafiri kuelekea Mwanza. Baada ya kutua nilendelea kuona umasikini kama niliouona DSM, nyumba za kimasikini zisizopangiliwa vema. Airport mtu anakubebea mzigo kwa vile vigari mpaka kwenye taxi, lakini baadaye anakuomba hela wakati haukukubaliana naye. Sintoongelea sana Mwanza.
4. Siku zangu zilivyokaribia za kurejea Ulaya, nilirudi DSM siku 2 kabla, lengo likiwa ni kuona mechi ya timu ya Taifa. Nakumbuka kulipokucha na baada ya breakfast nilimwambia dereva taxi anizungushe DSM niione kwa ukaribu, hasa miundombinu inayoongelewa sana kwamba imeifanya DSM kuwa kama Ulaya. Lengo lilikuwa baada ya kuzunguka mimi na dereva taxi tukaone mechi. Nilikubali kumlipa kwa ujumla. Nilimtaka anipeleke TFF maana kulikuwa na dada mmoja nilitaka kukutana naye ili aniuzie jezi za timu ya Taifa, DARAJA LA MFUGALE, DARAJA UBUNGO, KISHA TWENDE MLIMANI CITY KWA AJILI YA CHAKULA, KISHA DARAJA LA SELANDAR, BAADAYE TWENDE KIGAMBONI KUPITIA DARAJA LA NYERERE.
- DARAJA LA MFUGALE - SINA MENGI ILA NILIONA NI KAMA KITUTA FULANI TU KILICHOJAA UMASIKINI - HAKUNA LA MAANA LA KUPIGA KELELE NYINGI
- TFF - LICHA YA HELA ZOTE WAZIPATAZO NILISIKITIKA KUIKUTA KAMA NILIVYOIACHA, INATIA AIBU
- DARAJA LA KIJAZI - HAKUNA KITU, KAMPALA TU MBALI NA KUIHUSISHA NAIROBI TUNATIA AIBU KWA KELELE TUZIPIGAZO, MAANA WENZETU WA EAST AFRICA WAKO MBALI SANA KWENYE MAMBO YA FLYOVERS
- MLIMANI CITY-LICHA YA KUWA NAPAFAHAMU SANA, NILIONA KUNA ULAZIMA WA KUJENGA MALLS KUBWA ZAIDI KAMA ILIVYO KWA NAIROBI NA MIJI YA SOUTH AFRICA
- DARAJA LA BAHARINI SELANDAR
NILIONA KAMA TUNAJIPIGA WENYEWE, KIUKWELI SIKUONA UMUHIMU WA LILE DARAJA, MAANA KIJIOGRAPHIA NILIONA KAMA LIMELAZIMISHWA, NADHANI LINALENDA KUWARAHISISHIA MABALOZI NA WATU WAKUBWA WAKAAO MAENEO YA MBEZI BEACH, OYSETRBAY NA KWINGINEKO KUFIKIA OFISI ZAO KIURAHISI.- MAENEO YOTE YA UPANGA NA HATA IKULU NILIONA NI PA HOVYO SANA, UCHAFU NI MWINGI MNO, PENGINE NIMEATHIRIWA NA KUISHI MIJI AMBAYO ENEO LOTE LA MJI LIMEWEKEWA TILES.
- BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI NILIONA KUNA MAJENGO YAMECHOMOKA KIDOGO YALIUPENDEZESHA MJI, MAANA KIUKWELI WATANZANIA TUKO obsessed OBSSESSED SANA NA MAGHOROFA PENGINE KULIKO MIUNDOMBINU MUHIMU IKIWAMO MAJI TAKA NA MAJI SAFI NA UMEME, HIVYO KIUREFU WA MAJENGO TU, DSM INAYAZIDI MAJIJI YOTE NILIYOTEMBELEA, LABDA KWA UIMARA YANAWEZA KUWA CHINI YA KIWANGO ILA SI HABA.
- Hatukubahatika kuliona daraja la Nyerere maana muda wa mechi ulikuwa umefika.
MWISHO - SIYO KWAMBA NAPACHUKIA NYUMBANI LENGO LA UZI HUU NI KUTAKA TUBADILIKE NA IKIWA TUNATAKA MAENDELEO YA KWELI YA MIJI YETU NI LAZIMA TUKUBALI KUJIFUNZA NA KUONA WENZETU WANAFANYAJE. ILI DSM YETU IWE NA HADHI YA KIDUNIA NI LAZIMA (UKWELI MCHUNGU) KUBOMOLEWA UPYA, LABDA KUACHA MAENEO MACHACHE SANA, NA KUJENGWA UPYA (NI HASARA LAKINI BAADA YA KUJENGWA UPYA FAIDA YAKE NI KUBWA SANA)
NAWAOMBA VIONGOZI WETU WATEMBEE, WAJIFUNZE JINSI MIJI INAVYOJENGWA KUNA FAIDA KUBWA SANA KWA KUFANYA HIVYO
Kuna majitu ni mapumbavu na tatizo kubwa la Tanzania ni raia wake hawana exposure. Jitu mpaka limeota mvi halijawahi kuwa na Passport au halijawahi hata kutembelea walau nchi moja aone Wenzetu wanavyoishi.Kuna wakati nilikuwa na jamaa waliotoka Ulaya. Tulikuwa kwenye chopa iliyokodiwa toka South Africa. Wale bwana ilikuwa mara ya kwanza kutembelea nchi ya Afrika, nje ya Afrika Kusini.
Tulitua eneo moja mkoani Tabora. Nikawaona wameduwaa. Nikawauliza kuna nini? Wakasema, hawa watu maisha haya wanaoyishi, nikisoma vitabu vya historia kule kwetu, inaonekana ni aheri maisha ya karne ya 18 Ulaya.
Ndiyo maana wenye akili wakimsikia mtu akisema kuwa Tanzania ni tajiri, tupo vizuri - hawawezi kuelewa kama huyo mtu ni mzima kabisa!!
Mimi sijidunishi. Naipenda nchi yangu. Nimekuja huku chumbani, japokuwa kuna wa mataifa mengine wanaweza kusoma, kuteta ili ikiwa kuna viongozi basi wachukue hatua. NAIPENDA SANA TANZANIA MPAKA KUNA KIPINDI NATOA MACHOZI YA WIVU NIKIONA MIJI YA LEVEL YA KIDUNIA INAVYOPENDEZA ILI HALI SISI TUKIWA NYUMAKwanini tunapiga kelele kwa vijiendeleo kidogo tunavyovishuhudia katika nchi yetu? Tunafanya hivyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watanzania (na waafrika kwa ujumla) tumezoea kusikiliza negative publicity kuhusu nchi zetu, watu wetu na maisha yetu kwa ujumla.
Siku zote wazungu kupitia vyombo vya habari vyao wamekuwa wakiitaja Afrika kama "dark continent", "poorest continent", n.k, n.k. Juzi juzi mke wa Bill Gate hadi aliitabiria Afrika kuwa maiti zitakuwa zikiokotwa barabarani kwa sababu ya corona.
Unaweza kudhani hizo negative publicity hazina lengo. Zina lengo, na lengo lake kubwa ni kutengeneza mazingira ya kinyonge kwa waafrika, na sisi kuendelea kuzidi kujiona duni, na utu wetu kudharirika. Mtu ajionavyo mwishowe huwa hivyo.
Nimefanya kazi na wazungu -- kitu kimoja nimejifunza kwao huwa hawakiri udhaifu hata kidogo hata kama wana udhaifu. Labda nikupe mfano labda utanielewa. Nilipata kufanya kazi katika taasisi fulani ya elimu ya juu nchi fulani ya wazungu (sitaitaja) katika taasisi fulani ya elimu ya juu (sitaitaja). Mi nilienda huko na mindset kwamba kwa vile wazungu wapo juu basi kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza kwao kuliko wao kujifunza kwangu. Ila baada ya kukaa nao kwa muda kama mwezi nikagundua kumbe kuna mambo mengi waliyohitaji kujifunza kwangu kutokana na ujuzi na uzoefu wangu wa awali, kwa aina ya projects tulizokuwa tunazifanya. Sasa tabu ikaja pale walipokuwa wanahitaji kupata solution ya kitu fulani, ila hawataki kujionyesha kwa mtu mweusi (mimi) kuwa hawawezi niwasaidie. Mi nilikuwa nawacheki tu jinsi wanavyojizungusha maana maisha yao yote wamezoeshwa kujiona wao wapo juu na mweusi chini, but this time around on their nose kuna mweusi yupo juu na wao wapo chini. Anyway, long stori short ni kwamba hata siku moja hawakuwahi kunitamkia wazi kwamba hawawezi. Lengo ni kumaintain image yao waliyoicultivate kwa miaka mingi ya invincibility of white man mbele ya mtu mweusi hata kama ukweli upo wazi kwamba hata wao wana madhaifu yao mengi.
Sasa wewe endelea kujidunisha eti tu kwa vile unaishi katika nchi isiyo na nyumba nzuri kama za ulaya, na kujitamkia udhaifu. Kuna takataka moja ishawahi kuimba eti "bongo bahati mbaya". Stupid!
Wabongo acheni upumbavu kwani unataka sote tuwe na mtazamo sawa.Kwanini tunapiga kelele kwa vijiendeleo kidogo tunavyovishuhudia katika nchi yetu? Tunafanya hivyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watanzania (na waafrika kwa ujumla) tumezoea kusikiliza negative publicity kuhusu nchi zetu, watu wetu na maisha yetu kwa ujumla.
Siku zote wazungu kupitia vyombo vya habari vyao wamekuwa wakiitaja Afrika kama "dark continent", "poorest continent", n.k, n.k. Juzi juzi mke wa Bill Gate hadi aliitabiria Afrika kuwa maiti zitakuwa zikiokotwa barabarani kwa sababu ya corona.
Unaweza kudhani hizo negative publicity hazina lengo. Zina lengo, na lengo lake kubwa ni kutengeneza mazingira ya kinyonge kwa waafrika, na sisi kuendelea kuzidi kujiona duni, na utu wetu kudharirika. Mtu ajionavyo mwishowe huwa hivyo.
Nimefanya kazi na wazungu -- kitu kimoja nimejifunza kwao huwa hawakiri udhaifu hata kidogo hata kama wana udhaifu. Labda nikupe mfano labda utanielewa. Nilipata kufanya kazi katika taasisi fulani ya elimu ya juu nchi fulani ya wazungu (sitaitaja). Mi nilienda huko na mindset kwamba kwa vile wazungu wapo juu basi kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza kwao kuliko wao kujifunza kwangu. Ila baada ya kukaa nao kwa muda kama mwezi nikagundua kumbe kuna mambo mengi waliyohitaji kujifunza kwangu kutokana na ujuzi na uzoefu wangu wa awali, kwa aina ya projects tulizokuwa tunazifanya. Sasa tabu ikaja pale walipokuwa wanahitaji kupata solution ya kitu fulani, ila hawataki kujionyesha kwa mtu mweusi (mimi) kuwa hawawezi niwasaidie. Mi nilikuwa nawacheki tu jinsi wanavyojizungusha maana maisha yao yote wamezoeshwa kujiona wao wapo juu na mweusi chini, but this time around on their nose kuna mweusi yupo juu na wao wapo chini. Anyway, long stori short ni kwamba hata siku moja hawakuwahi kunitamkia wazi kwamba hawawezi. Lengo ni kumaintain image yao waliyoicultivate kwa miaka mingi ya invincibility of white man mbele ya mtu mweusi hata kama ukweli upo wazi kwamba hata wao wana madhaifu yao mengi.
Sasa wewe endelea kujidunisha eti tu kwa vile unaishi katika nchi isiyo na nyumba nzuri kama za ulaya, na kujitamkia udhaifu. Kuna takataka moja ishawahi kuimba eti "bongo bahati mbaya". Stupid!