Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Tusijidharau kiasi hicho. kikubwa tujue historia. Tanganyika baada ya vita ya kwanza kumalizika ilikabidhiwa kwa waingereza ili waishikirie mpaka tutapo weza jitawala. Hivyo hatukuwa koloni la mwingereza.Kwa ijumla miji ya Tanzania kimpangilio, ni ovyo sana.
DSM, sijui utailinganisha na mji gani!!
Achilia mbali miji ya Ulaya, hata ukilinganisha na miji ya Afrika tu, DSM si lolote, si chochote.
Hayo madaraja yanayoitwa flyovers, si chochote. Nilienda wakati fulani Bamako, Mali, nchi ambayo karibia robo tatu ni jangwa, ina mpangikio mzuri, mara 10 zaidi ya Dar. Flyovers wala siyo kitu cha kuongelea, ni kitu cha kawaida, na sijui zipo ngapi!!
Ukienda tu hapo Maputo, mji umejengeka na kupangwa hasa, japo pembeni kabisa huko, ni takataka. Lakini kati kati ya mji, ni mji hasa. Tunajisifu na daraja la Nyerere, letu ni fupi kuliko la Maputo.
Nenda Harare, Dar ni takataka.
Sisi tatizo letu, mafanikio kidogo, kelele ni nyingi sana.
Tulikuwa under (British Protectorate) Hii ilimfanya Mwingereza hasifanye maendeleo yoyote ya maana. Kwani alijua kabisa ipo siku anaondoka. Hakuweza kuwekeza kama ilivyokuwa kwa mjerumani. Japo Mjerumani alikaa kwa muda mfupi. Ndo maana wakati wa uhuru Nyerere alienda Umoja wa Mataifa kudai Uhuru kuwambia tuko tayari kujitawala.
Hii ni tofauti na nchi ambazo zilikuwa makoloni kama Zimbabwe, Kenya na zinginezo. Hizi nchi wazungu walikuwa Settlers, walifanya makazi ya kudumu kama ilivyo Maputo. Walijenga na kupangilia miji kama ilivyo Ulaya. Hii ni tofauti na Dar ambayo wewe na mimi tunapata vimishahara vyetu tunajijengea nyumba kulingana na uwezo wetu.
Tembelea nchi ambazo hazikuwa na ma settlers miji yao haijapangika na kuna nyumba nyingi za hali ya chini. Mfano Ethiopia, ni mji mzuri lakini tembea mitaani utajua. Nenda Somalia pia. Ni baadhi tu. Tusijidharau Dar imepiga hatua, Dar ya mika ya 90 haikuwa hii ya leo. Nakumbuka Kariakoo kulikuwa na nyumba za makuti. Nyumba za Miti na tope zikaezekwa kwa mabati chakavu.
Kuna wakati upepo ulivuma na kuondoa paa kadhaa na kuleta maafa. Hiyo ilikuwa 1993. Kariakoo hakukuwa na barabara za lami. Ilikuwa Vumbi. barabara ya kunduchi, Tegeta mwenge balaa ilikuwa unapanda mabasi kama ya mikoani yanaanzia kariakoo, tena ya kusubiria. Mwenge kulikuwa na chai maharage.
Tegeta ndo ilikuwa mwisho wa mji. Huko Boko, Bunju ilikuwa ni kijijini, watu wanalima.
Tujipongeze hata kwa hivi vichache tulivyovipata kwa nguvu zetu. Kubeza haisaidii, kuwa proud na ulichonacho.