Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Nilivyoyaona maendeleo ya Tanzania baada ya kuwa Ulaya kwa zaidi ya miaka minne

Ok. Nitajie zote ulizotaja na mwaka kila nchi ilipata uhuru, vingenevyo nitajua hujui kitu kabisa
Nchi zote hpo tulipata nao Uhuru almost Sawa kasoro China sa sijui unatka nn??

Unatetea nchi kuwa chafu na ujenzi holela kwa kisingizio cha umaskini ?
 
Uwezo wako wa kufikiri ni wa kati... Wenye uwezo angalau wa kueleweka wanakuja na mapendekezo baada ya kuonyesha tatizo hawaji na ukosoaji na kebehi pekee...

Nchi kama Tanzania hakuna kisichokuwa kipaumbele ndio maana huijui historia ya nchi yetu na hutaki kujifunza... Hatua za maboresho ya miundo mbinu, mazingira, afya, uzalishaji, usafirishaji, elimu, ajira na huduma za jamii zinahitaji fedha kununua teknolojia, ujuzi na mitambo, tafiti, kulipa ujira nk...

Ukiwa na hali tuliyonayo kama nchi unawezaje kubeza tulichonacho... Anza kujiuliza wewe mpaka sasa umechangia kiasi gani kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yako...nini mchango wako ...anzia ndani ya familia yako anzia hapo Mwanza alipo mama na baba yako umechangia kipi kuleta mabadiliko chanya kwa exposure uliyopata nje ya nchi... Umewezaje ku transform kilichopo kuwa bora kama ulichojifunza ulaya?
Ikiwa unaponda tu bila mapendekezo basi huitambui nafasi yako katika nchi na jamii in general.

Nitakupa mfano mdogo sana jiji la Dar (sasa Ilala) na zamani Mzizima kabla ya Sultan Seyyid Majid wa Zanzibar kuibatiza Mzizima jina jipya la Dar es salaam ni moja ya mji mkongwe... then 1891 Ujerumani walifanya mji mkuu wa kibiashara mpaka walipojenga reli ya kati 1904 Dar-Kigoma waliushikilia mpaka waliposhindwa vita 1940s then uingereza ika takeover mpaka 1961 ....maana yangu ni nini muda wote huo mji ulikuwa unaendelea kuongezeka wakazi na makazi kwa kasi kiasi kwamba uwezo wa serikali ya kiraia kuuhudumia mji ulikuwa mdogo... Sasa leo hii ndio hizo pangua pangua, bomoa bomoa zinakuja kutokana na jiographia ya Dar kumekuwa hakuna mbadala kwa baadhi ya maeneo kuruhusu ujenzi wa kisasa unao utaka... Madaraja ya coco nk nikatika kuufungua mji na kupunguza compessision cost, kupunguza relocation endapo utawatoa watu katika maeneo yao.... Utaona mifumo ya maji safi na taka ilivyozidiwa [iliundwa kuhudumia watu laki 4.5 leo wapo 6m+] na sasa inaboreshwa na kuanzisha mipya...

Walau umekiona ulichokiona na ukaweza kufanya mlinganyo kuliko kisingekuwepo kabisa...

Anyway ulitoa mawazo yako nimekuelewa hata kama sikukubaliana nawe. Maana kumwelewa mtu kunasaidia kujua uwezo wake.
Mimi nimekosoa. Wewe njoo na suluhisho. Huwezi nifundisha namna ya kuandika. JIBU HOJA
 
Ukweli uambatane na ushauri namna ya kufikia hicho kiwango mnachokiona huko ng'ambo! Ukweli huku unachombeza kwa lugha zisizo na staha, tunarudi kwenye lugha za kuudhi.
Kwani mtu kujua hili si sawa ni lazima ajue sawa ni lipi?
 
Ukweli uambatane na ushauri namna ya kufikia hicho kiwango mnachokiona huko ng'ambo! Ukweli huku unachombeza kwa lugha zisizo na staha, tunarudi kwenye lugha za kuudhi.
Watanzania wengi hatujui umuhimu wa criticism. Sioni mtu wa kushiriki hard talk mfano wa ile ya BBC. Hatupendi ukweli.
 
Jamaa mzushi tu,wengine tunaishi kwa watu toka 2005 na tukirudi nyumbani unaona kuna kijihatua kimepigwa,shida ya dar uchafu tu na vile vibanda vya wafanyabiashara vilivyozagaa bila mpangilio kila mahali ndio vimeharibu
We utakuwa unafikiaga osterbay na masaki , ukirudi bongo nenda katembelee chanika na gomz uone jinsi ujenzi wa slum ulivyoshika chati
 
Ungeongelea na kijini kwenu ulipozaliwa wewe au mzazi/wazazi wako pakoje kidogo ningesema hujatumwa,ila mbona hiyo sehemu hujaiongelea? Tuachane na kote huko nadhani umeona nyumba za huko ulaya zilivyo watu wanapoishi.

Hebu ungetuonyesha na nyumba anayoishi mzazi/wazazi wako hapa bongo tuone vina utofauti na maandishi yako hapo juu,Mkuu hapa ndio kwenu hata ukipakataa Ukifa utapandshwa pipa utarudi kufukiwa huku huku kwa maskini.
 
Watanzania wengi hatujui umuhimu wa criticism. Sioni mtu wa kushiriki hard talk mfano wa ile ya BBC. Hatupendi ukweli.
Steve wa HD hatumii lugha za kuudhi bali uhoji kwa staha ingawa wakati mwingine u-provock muhojiwa kwa maswali tatanishi. Na mwisho wa kipindi kama mahojiano yameenda vyema utoa furusa kwa muhojiwa kutoa ushauri kwa jambo husika!
 
Ungeongelea na kijini kwenu ulipozaliwa wewe au mzazi/wazazi wako pakoje kidogo ningesema hujatumwa,ila mbona hiyo sehemu hujaiongelea? Tuachane na kote huko nadhani umeona nyumba za huko ulaya zilivyo watu wanapoishi.

Hebu ungetuonyesha na nyumba anayoishi mzazi/wazazi wako hapa bongo tuone vina utofauti na maandishi yako hapo juu,Mkuu hapa ndio kwenu hata ukipakataa Ukifa utapandshwa pipa utarudi kufukiwa huku huku kwa maskini.
ZERO BRAIN, Topic ni maendeleo ya Tanzania, siyo maendeleo yangu binafsi.
 
Steve wa HD hatumii lugha za kuudhi bali uhoji kwa staha ingawa wakati mwingine u-provock muhojiwa kwa maswali tatanishi. Na mwisho wa kipindi kama mahojiano yameenda vyema utoa furusa kwa muhojiwa kutoa ushauri kwa jambo husika!
Lugha ya maudhi na isiyo na maudhi ni ipi? Kuna uongo kwenye nilichokiandika?
 
Unajua hizo nchi unazozisifia zilipata Uhuru lini? Na tz ilipata Uhuru lini? Ukijua Hilo utaelewa kitu

Swali la kitoto, kama hutaweza kutuambia inahitaji miaka mingapi kufikia hatua yao!! Kuna nchi kama Malaysia, Singapore na Vietnam. Miaka ya 1970s zilikuwa kama sisi. Je leo ziko sawa na sisi???

Kazi yetu sisi kupiga mdomo tu!
 
Kwetu Mwanza. Nitapaongelea siku ingine. Lengo siyo kujionesha, ama kwamba napachukia nyumbani. TANZANIA NI KWETU. LENGO LANGU NI KWAMBA TUNATAKIWA KUJITATHMINI. KUDHANI TUMEFIKA KUNATUPOTOSHA.
Una miaka 4 tu Ulaya unasahau neti? Niko miaka 20 na nathamini kwetu Bongo. Kila sehemu inao uzuri na ubaya wake hata hiyo Colon yako.
 
Shalom,

Baada ya kuwa Ulaya kwa miaka zaidi ya minne, hatimaye mwezi wa tisa mwaka 2020 niliamua kurejea nyumbani ili kumjulia hali baba yangu mzazi pamoja na ndugu zangu.

Kwa kawaida mimi napenda sana kutembea, zaidi napenda kufurahia na kujifunza namna miji duniani kote ilivyojengwa. Hivyo nikiwa ulaya mbali na nchi ninayoishi niliamua kutembelea mara kadhaa Brussels, Paris, Berlin, Colon, Dortmund, London, Oslo na miji mingi midogo ya ujerumani.
Huo mji wa colon uko wapi?
 
Leo ndo nimemuelewa JPM kuhusu watoto wetu kuijua historia ya nchi yao.... Ukijua mmetoka wapi, mkoa wapi na mnaenda wapi unaweza kuja na uzi tofauti na huu.
Tumetoka nchi ilikuwa na viwanda lukuki

Ova
 
Back
Top Bottom