Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Ukiitwa mpumbavu au msukule utasema umetukanwa!!?
Matokeo ya Urais yanahojiwa mahakama gani huko Tanzania!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu iwe nini? Watu wanaeleza walichokiona kwa experience yao, kama unajikuta TISS kafatilie lile begi la kura Boss.
Swali zuri "Halafu iwe nini?", nadhani ungemuuliza hili swali mleta mada.
Haisaidii tuu kusema niliona haya yakifanyika tena ukiwa JF! Je ni hatua zipi umechukua na kwa wakati gani?
Ukiniuliza mimi, nitaanza na shuhuda halafu ushahidi nikiridhika mchakato wa kupata justice unaanza.

Wewe ulitakaje kwani?
 
Kuandama kudai haki zenu hamuwezi na hakuna lolote mnaloweza zaidi ya kuja kulalamika tu humu mitandaoni.
 
Justice wapi bwana mkubwa, Tanzania?! Justice nchi hii katika masuala ya siasa ni majina tu kama majina mengine, Innocent,Gasper,Rahim e.t.c
Msaidie basi Tundu Lissu kupata hiyo Justice katika issue ya kupigwa risasi tu, walau hata uchunguzi uanze...

Hapa ni kususia tu mauchaguzi yote, kupeleka lawama kwa jumuiya ya kimataifa, kubadilisha vyama kutoka kuwa vya siasa typical na kuwa vya kimapinduzi, hali iwe ngumu kweli kweli mpaka tuongee lugha moja na MATAGA, meantime unga wa ugali kilo uuze 9000/- hivi.

Hivyo ndio mi nataka, tuwezeshwe...sio mi nakuja na uma, mwenzangu ana " spray silver".
 
Hata yeye hakujua kama hyo yanatendeka. Wateule ndo walijipendekeza kumpa kura nyingi ili waonekane wanpig kazi.
Unaona wameanza kuulizia usalama wa vibarua vyao
 


Kazi ilianza na inaendelea .. Si lazima yote yawekwe hadharani!
 
Ndo maana tunasema wote walomtegemea Mwanadamu na kushiriki wizi wa kura basi laana na iwe juu yao.

Mungu Baba tunaomba watu hao wote waloshiriki uwalaani kupitia andiko lako hili, amen...

"5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana."
~Yeremia 17 :5~
 
Nipo tayari, ila kiukweli msiniue tu.
Usiende kichwa kichwa piga ramli kwanza haya Manyani ya Lumumba hayatabiriki! ndiyo chanzo cha sisi kulinganishwa na hayawani Nyani!!

Lazima gujiwe ataongoza kwa shida sana miaka hii, kura za mwaka huu ni afadhali awamu yake ya kwanza kidooogo alipatamo japo pia ni hayo hayo tu! hataamini atakapoangukia!!!

Majeshi yetu nayo yanapenda kuburuzwa sana na Raia ambaye hauji hata Mdeki ni nini!! sijui kwa nini!!! ...nadhani Jibu rahisi ni Mwenge.
 
Kwa kulazimisha km hivi afanyavyo!!! Hata hiyo miradi yake haitaishi miaka mingi, itakufa mbele ya macho yake tena kifo cha Mende, tukianzia na Bombadier yatasahaulika tu. km lile hekalu alilojenga Herode!
 
Uliapishwa kuwa msimamizi wa uchaguzi. Haiingii akilini mwangu kwamba uliona maovu yanatendeka na wewe unakubali tu maagizo kinyume cha kiapo ulichofanya.

Watu kama wewe, kama kweli wapo, ndiyo wanaokwamisha demokrasia nchini. Bora ungekataa kujaza nafasi hiyo kama unajiona huwezi kukataa agizo ambalo linakinzana na ukweli wa mambo.
 
Hayo mazingira yalikuwa magumu si rahisi kama unavyoongea .
 
Uchaguzi umeisha wewe hujasikia? Leo ukitueleza upuuzi wako huu unadhani sisi ni UN? Nenda Mahakamani
Kwa kuwa na watanzania wenye mentality kama yako basi Tanzania haitobadilika, tutabaki tu viongozi wakiiba na kuvimba vitambi na sisi wananch wa kawaida maisha yakizi kuwa magumu, lakini hey CCM oyeee!!
 
Usishangae sana. Lipumba aliibiwa hadi kura yake, yaani alijipigia kura, lkn kwenye hesabu haikuonekana. The same applied kwa Selemani Bungala (Bwege) kule kilwa. Huu ulikuwa uchafuzi, sio uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…