Inatokea post namba 223.
Nimeona tuwekane wazi kidogo. Kisa kilichowisha post namba 223 kimeelezea nilipokabidhiwa majini na babu yangu, yeye alikuita kufunguliwa macho. Kwa kiwango fulani kweli nilifunguliwa macho. Kisa kilochofatia nikaonesha safari yangu ya kwanza baada ya kuoa, ilionipeleka Shinyanga na majini wakafanikiwa kumfanyia mwanamke aliekua anasumbuliwa na majini. Ieleweke kua sijatibu mimi na wala sijui walitibu vipi zaidi ya mimi kumshika kichwa tu yule mwanamke na walichonielezea hao majini siku ile na baadae.
Kisa hicho ni cha miaka mingi sana nyuma, sasa hivi ni mtu mzima. Babu yangu alishatangulkia mbele ya haki. Shamba letu la ufukweni Duga, lipo mpaka leo, wanaokaa pale kwa sasa ni watoto na wajukuu wa babu walioamua kuishi pale. Watoto waliopo pale ni mmoja mkubwa kwa baba yangu wa kike. Na wakiume na mkewe na wanawe ni kwa mama mwingine na baba yangu, wanachangia baba tu.
Binafsi huwa nakwenda sana Duga shamba la babu, kwa sana namaanisha kila msiumu wa kamba huwa tunaenda mimi na mzee kuvuna kamba. Licha ya kamba, kwa babu kuna minzi mingi sana, kuna miembe mingi. Babu yangu alikua anapenda sana miti ya kudumu, kuna miembe ya aina )ofautoi isiopungua 500 na minazi zaidi ya 1000 aliyoiacha marehemu babu.
Bhati watoto zake wote wanajiweza, wanashughuli zao na mali zao, na wawili, mkubwa wa kike na miumewe na watoto zao na mkubwa wa kiume watumbo lingine ndio wanaoishi huko full time. Waliamua wenyewe waishi huko ili shamba lisikose mtu na lina utajiri wa kutosha. Mbali ya minazi na miembe alioicha babu, kuna miti mingi ya hapa na pale ya matunda, ambayo haipo kwa kiwangi cha biashara. Babu alipanda kila aina ya matunda kidogpo kidogo, shamba la babu ni kubwa sana, sio la kitotpo na nazi karibia kila siku zinangushwa, na pesa wanagawa kwa kila ndugu, Hakuna tatizo, wasimamizi ni wazuri sana na wacha Mungu.
mambo ya tiba na pango kuna wanafunzi wa babu lakini hawako kwa kiwango cha babu lakini mradi wapo tu. Umaar8fi wa kwenda kutibiwa watu kwa mzee Mabruyki uliisha alipoondoka mwenyewe. Mimi binafsi sijairithi kazi ya uganga ya babu, kabisa tena. Wapo majini alioniwachia babu, ikitokea, wao ndio wanatibu watu bila mimi kujua wanachokifanya zidi ya kunijulisha tu.
Arsis yupo, pete yake naivaa kila siku. Jini wa bakora yupo na bakora ya babu aliirithi binti yake ambae anakaa shamba kwa sasa, yeye ndio anaitumia kwa tiba watu wakienda. Anaelewa mwenye anatibu vipi, mimi simuingilii wala simuulizi. Ni shangazi yangu, yeye ananipenda sana na anawaambia kila mtu., mimi ndio mroithi wa babu kwenye uganga.
Visa vinavyofatia sana sana vitakua vya mahojiano kat yangu na Arsis, nitajitahidi kuvifanya vyepesi vieeweke ingawa mimi sio mwandishi.
Arsis mpaka leo ni rafiki yangu na anakuja kila nikimuita xile sehemu zake za kumuita. Mwenyewe anapenda sana kila nikija kwenye msimu wa kamba nimuite kila siku tuongee. Mpaka leo kwa Dar nikita kumuita nakwenda pale oshen road, [pia alinionesha na sehemu nyingine mtajijua wakati kisa kinaende;lea. Hii ipo nje ya mji kidogo.
Visa vijavyo vina elimu kubwa ssna ya Arsis, sio yangu. Mimi najifunza kwake.
Kuna watu wengi wanaongelea kuhusu majini waongo, wazuri, wabaya. Kwenye mahojiano na Arsis tutapata mwanga mkubwa sana kwa mujibu wa Arsis. Napend ieleweke, Arsis anasisitiza sananijifundishe kusoma uandishi ili niandike vizuri, ananambia yeye atanisaidi kumbukumbu kwa niliyoyasahau na atanisaidia kunielezea yale amabyo nitahisi yanahitaji aeleee zaidi.
Nawaahidi nitapitia post moja moja za nyuma na kurekebisha maandishi, kupunguza au kuzidisha na kurekebisha nilipokosea na kuyakusanya kwenye post moja ikiwezekana, yaani kufanyia editing. Ardis kanambia kuna makosa mengi sana, afahamu kua anusoma huu uzi, sifahamu kama ni member JF au hapana, nimemuuliza hilo akanambia " mimi nimekwambia nasoma tu, usiniulize zidi kuhusu hilo". Hiyo ni kawaida yake Arsis, mtajionea mbele huko namuuliza mpaka anakasirika.lakini ni mtummwema sana. Mwenyewe anashikilia nimwite mtu. Ingawa kiukweli sijui ni kiumbe wa aina gani. Mimi nachukulia ni mtu kama mimi lakini hataki aonekane. Isipokua anasema umeshaniona mara nyingi lakini hujui kama ni mimi. Anasisitiza anakuja kwa sura na muonekano tofauti bila mimi kufahamu.
Itaendelea.