Inaendelea kutokea post namba 1.
Babu akatupokea pale, tukakumbatiana kwa futraha, mara na bibi nae akaja aliposikia nimefika, akanambia "aah, sasa mume wangu ndio kaingia, sio hiki kizee, sina habari nacho tena". na yeye bibi akanikumbatia akanipiga mabusu ya ngubu ya shavuni, akanambia twende ndni mume wangu, nimekutayarishia chumba chako.
Nyumba ya babu yangu ilikua ni kubwa sana kwa maisha ya kijijini, inavyumba self contain vitatu, umeme utafikiri upo mjini. maana umeme umepita hapo hapo kijijini kwao, wenyewe wanasema huu unakwenda Kenya, unagtikea Hale. Kwa ufupi hauhisi kabisa kama upo kijijini mpaka utoke nje ya bma lake. babu alikua na nyumba hiyo yake kubwa na nyingine ndogo ndogo z vyumba viwili auj kimoja zimetapakaa pote kumzunguka. Nyingi zilikua za kufikia wageni wanaokuja kwa matatizo yao kwa babu yangu, babu alikua mganga wa jadi, tena anaesifika kweli. Kwake hapakosi wageni, mpaka mawaziri utawakuta huko. Kila mmoja na shida yake.
Babu toka nimefika alikua haniwachi peke yangu, ana nyumba moja ipo karibu na kwake hiyo mwenyewe ndio ofisi yake, ina chumba kizuri tu, cha kufanyia shughuli za ke na wageni wake, na kama ina baraza kubwa ndipo wanapoisubiri wageni wanaokuja kumuona, na ina vumba viwili vidogo ndani, mwenyewe anavoiita "operation rooms". Babu alikua anaongea na kuandika Kingereza na Kijerumani kwa ufasaha kabisa. Kabla ya kaumua kurudi kuishi kijijini alikua ni fundi mekanika, tena fireman, wa idara ya vifaa na magari ya serikali hapo tanga. Alikua ni mtua anaejulikana sana Tanga na anaheshimika sana. Ni mcheshi sana, kutwa anatabasamu, akikasirika humjui kabisa, wewe kutwa kucha unamuona ni mtu wa furaha tu.
Itaendelea.