Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Mwambie uyo mwamba aka mchape makofi namba moja pale magogoni .
Ha! Hivi hujanisoma humu kua pale ndio lango la kwenda dunia zingine? Na pale jirani ndio kituo cha kukutana na Arsis?

Mule Ikulu kuna mambo makubwa sana kwa kujulisha tu, Sina ujuzi napo zaidi wala siruhusiwi kuuliz ya mule ndani, Naogopa.
 
You are very warmly wellcomed

Sina kandokando zotote za kuogopa habari zangu.

Na aziseme hapa namruhusu.

Mimi nakunywa bia tu na kuilea familia yangu.

Sio mtu wa mademu wala dili za kudhulumu watu.
Na sio mchawi
Nilikua sijaiona hii ruksa.

Arsis anasema wewe ni Muislam, ila ni asi tu.

cc; FaizaFoxy
 
Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1.

Hiki kisa kilitokea kama miaka 2miwili baada ya kurudi sagfari yangu ya Shinyanga.

Siku hiyo nimepigiwa simu na mtu nisiemfahamu, yaani halikutoka jina kwenye simu Kupokea ni mwanamke akajitambulisha kua yeye kapewa namba zangu na Sharifu Ali wa Shinyanga, kamwabia aongee na mimi mwenyewe moja kwa moja.

Nikamwabia, karibu sana, Sharufu ni mzee wangu. Akaanza:

Mwanamke; Sisi baba (sauti ya mtu mzima) limetutokea tatizo kubwa sana inakaribia miezi sita sasa, tumehangaika sana mpaka kwa waganga wa kienyeji huko, ndio tukaletwa kwa Sheikh Ali na mama ambae binti yake aliumwa akafanikiwa kuponeshwa kwa Sharrifu. Tumeongea na Sharreifu amesema alieifanyia hio kazi ya yule binti yupo Dar, alikuja tu hapa kwa kazi zake. Ndio katupa namba tuongee na wewe.

Sema tu mama; Mimi baba nimepoteza mwanagu wsa kunzaa mwenyewe, wa kiume, mtu mzima ana miaka 33, sio mtoto mdogo. Huyu mwanangu alikua na biashara zake hapa ikawa hayupo mbali kuoa, akapata maradhi kama ya kurukwa na akili, tukampelka hospitali haikusaidia, akawa anatoroka toroka nyumbani, haendi kwenye kazi zake, siku hio katoroka nyumbani ndio mpoaka leo hatujamuona. Sasa baba tunahotaji msaada wako, hatujuwai yu hai au kafa, tumemaliza Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida kumtafuta na kuhangaika kila sehemu, ndio tukaelekwa kwa Sharifu. Hivi nipo hapa Shinyanga lakini nimetokea Mwanza, nipo hapo lo wiki nzima.

Mimi;Upo hapo kwa nyumbani kwa Sharrifu?

Mama: Hapana baba, hua nakwenda tu kumsikiliza ndio mpaka leo kanipa namba yako, naomba baba tusaidie.

Mimi; Mama nimekusikia nimekuelewa, mtangukize Mwenyezi Mungu mbele. Nitakupa jibu mimi au Sharrufu, leo hii au kesho. Toa shaka.
Mama: baba hata ukiniambia nisubiri wiki, mimi nitasubiri, sina cha kufanya,mwanagu najua kwa ugonjwa ule anapata shida hajiujui hajitambui. Moyo wangu haukubali kua kafa baba.

Mimi; Usijali mama, nitakupigia. Kwaheri, usiwe na wasiwasi.

Nilikua nipo kazini na mzee lakini hakuna za maana ambazo zinanihusu sana mimi, nikamuaga mzeenikaenda nyumbani. Hata mke wangu kashangaa nimerudi mapema.

Wife: Vipi, kwema?
Mimi: kwema wacha nikoge kwanza nitakuelezea, wifa anafahamu nikiwa na jambo linanizonga, akaniwacha nikaingia kukoga nikabadili nguo nikatoka jje nikaenda kunywa juice kwanza.

Wife; Nikuletee kahawa?
Mimi; No, sio sasa hivi, mbona kimya? Wametoka na mwanao kamlilia bibi yake amchukue na bibi yule anavyo mdekeza nikaona isiwe kero aende nae tu.
Mimi; Si mama mwenyewe kamzowesha kwenda nae mizunguko yake?

Wife; Bira haswa, na imi napata kufanya yangu.

Mimi ; Nipo ofisini kwamgu.

Wife anajua nikiwa ofisini kwangu nyumbani sitaki kero kabisa, hata akija mtu wtanipigia simu, hawagingi mlango.

Nikachukua bakora nikaisimamisha mbele yangu, nikamwita Jini Bakora, akaja, tukaslimiana pale, nikamweleza kisa chote. Kanambia mwite Jini wa Arsis, mweleze. Mimi hio sio kazi yangu. lakini nikihitajika kwa lingine nitakuja.

Tukaagana, nikamwita jini 1, hua hachelewi kabisa, akaja dakika hio hio, siku hizi nikiwaita ofisini kwangu wanajua wapi watokee na wapi wakae, tuongee. Nikamweleza mwanzo mpka mwisho. Akasema ngoja nakuja nipe nusu saa. Akaondoka zake. Ile anaondoka natazama simu kama kuna mtu kanitafuta nikakuta miss call ya Sharrifu Ali. Nikapigia, baada ya kusalimiana.

Sharrifu Ali, yule mama kakupigia kanambia sasa hivim kasema utamjibu wewe au nitamjibu mimi. Sawa?
Mimi; Sawa, Sharrifu. Inabidi unisurbirie mpaka baadae au kesho nitakupigia, sijui tufanye nini, hii kesi ya polisi.
Sharrifu; Wamemaliza polisi zote, polisi wakijua kama jamaa aliwehuka wanakuwa hawaitilii mkazo sana. Kuna polisi Mwanza huko kamwabia "mama zungukeni majlala yote ya mwanza, watu namna hio wanapenda sehemu chafu chafu". Ndio hivyo mama akija kwangu anaia tu. Hata sijui tufanye nin, leo wiki hapa tunapiga kitabu na vijana wangu, ndi wife wangu akasema nikwambie, akanishauri nimpa namba yako mama yule aongee nawewe, nisamehe kwa hilo, ilikua nikujulishe kabla sijamwabia.
Mimi; Umefanya la maana Sharrufu, maana Sharrufu wala usijali.
Sharrifu: Kama si Anti yako hapa nisngempa namba wala nisingewambia, toka ulipoonambia hii kazi huifanyi, ni bahati tu ulikuepo lakini hufanyi tiba. Nikawa naogopa kukubesha mizigo, maana niyie vijana na kazi hizi wapi na wapi.
Mimi; Kweli mzee wangu, lakini tuombae Mwenyezi Mungu, tukaagana nikaenda kufanye mengine.

Kam nusu saa hivi, akaja yule jini lakini hakujitokea nilikua uani kwetu, nikaongpoza chumbani ikawa nimeingia nae akakaa sehemu yake.
Jini 1; Nimekuja na mama, nimwite?
Mimi: Mwite, kidogo mlango wa ofisini ukagongwa nikafungua akaingia mama yule jini. Tikaslaimina. Akaanza;
Jini2; Nimepata ujumbe wako na nimeufanyia kazi, tumeongea na Arsis kasema tukueleze tu nini cha kufanyika.
Mimi: Sema tu.
Jini e: Chukua kahawa ukae utulizane, nikueleze kwa kituo.

Nikaenda kuchukua kahawa jikoni, nikauta chupa nzima nikaingia nayo ofisini, nikawakuta wananisubiri/
Mimi: hya jamani nipeni habari.
Jini 2; Habari zjnuri sio mbaya, huyo kijana yupo hai lakini hajijui hajitambui, Arsis anasema atapatikana na huko aliko, kawekewa ulinzi na Arsis ili wasinedelee kumfanyia mambo ya kishirikina.
Mimi ; Yuko wapi?
Jini 2: Hilo atakufahamisha Arsis, Arsis kasema leo usiku uende kule mkaongee. Mimi alinipa kazi na akanambia nije kukufahamisha hilo, usiwe na wasiwasi lakini usiwaambie chochote watu wake mpaka ukishaongea na Arsys usiku.
Mimi' Sawa. kunalingine?
Jini 2: Ndiyo yapo kidogotu. Hii simba ni mamaboi ya kichawi, uchawi wa kishenzi kabisa, ndio maana wameniita mimi nikaifanye hii kazi. Mimi nimekwenda nimuona kijana, hali yake sio nzuri, wachawi ni watu wabaya sana. lakini, Arsis kasema hakuna wasiwasi, atapona kila kitu kwa muda mfupi sana, yeye anaanza kufanya kazi kuanzia ssa, wewe nenda usiku. Mimi nimemaliza;
Mimi; haya mwabieni nitakwenda.

Tukaagana wakaondoka.

Itaendelea.
 
Arsis ni Jinn tena mkubwa mzee maana jinn anavyokuwa mzee ndio anazidi kuwa na nguvu pia anaonekana licha ya nguvu ana elimu na ilmu.
Ila ni muongo kusema yeye anaqeza kuwa chochote kawaida ya making wengi ni waongo hawapendi kusema ukweli kila kitu haswa jina lake asli yake sababu wanaogopa kutumikishwa na mwanandamu, Mwanadamu ana nguvu sana ni khalifa, Ila jinn anamuogopa sana Mwenyeezi Mungu kuliko sie wanadamu na ukiwa Mcha Mungu ndio kabisa wanakuogopa.

Majinn wanapenda sana ubinadamu wanapenda sana kila kitu cha mwanandamu japo wana uwezo Ila hawawezi kitu kuchukua bila idhini ya mwanadamu mfano jinn anataka damu kwanini asikamate mwenyewe akamfyonza jibu ni hawezi mpaka mwanadamu ampe go ahead.
Naona hao wa kutaka damu ni wachawi, Arsis hajawahi hata kuguzia hilo au kutaka chcochote na hapatani kabisa na binadam na majinni wachawi.
 
Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 B.


Usiku nikaenda Ocean Road kama kawaida, nikamwita Arsis;

Aysis: Simba, vipi hali yako
Mimi; Sipo sawa kabisa leo.
Arsis: Nafahamu sana, hii habari ni nzito sana. Subiri nikueleze kilichopo na nini kifanyike.
Mimi: Sawa.
Srsis: Sikia simba, Ali asingekupigia simu kabisa wala asingetoa namba yako lakini sisi ndio tulifanya akupigie.
Mim; Nyinyi kivipi?
Arsis: Please subiri usiulize maswali maka nimalize kukufahamisha, usiumize kichwa, acha mimi niwe niulize maswali.
Mimi; Sawa.
Arsis: Unakumbuka ulimuona mke wa Sharifu ulipokua Shinyanga?
Mimi; Namkumbia sana.
Arsis: :lazima umkumbuke, kwa sabu yupo tofauti na watu uliozowea kuwaona. Si unafahamu kua yule ni Muindonesia?
Mimi: Nafahamu hilo, alinambia mzee hapa. Alinambia "Ali alikwenda Indosia, kwa ami yake, ndio akaozwa yule binti kule na yeye ni Sharifu vilevile.
Arsis; sawa kabisa, yule mwanamke ni mwema sana na alijaaliwa Qareen, wqengine wanaita Ruhani, lakini ni Qareen., mwema mwema sana. Wale Ali na mewe kwenye ukoo wao ni watu wa Ilmu na wa tiba, lakini Ali yeye watu wanasikia Sharifu wanakwenda anawaombea dua na anawasome Qur'an inakuwa kubul, alipokuaja mkewe, alkua hata Kiswahili hajui kabisa, kajifundisha haraka sana kaelewa. Qareen wa mkewe ni wa tiba, za ilm na dawa za Kiarabu, binadamu wengine wanadanganya za sunna, sunna ya nani, waongo tu.

Sasa wakija watu kusomewa dua, mkewe anaobeshwa na Qareen wake wana matatizo gani na watibiwe vipi anamwabia Ali, Ali akawa hata hizo dawq HAJUI apate wapi. akawa anaagoza mafduka ya dawa kutokea Dar. Zikifika yule mwanamke anatzama zingine anazikubali zingine anazikataa. Anasea hizi sawa, hizi sio swa. Ali hakuwa na wasiwasi sana kwa sababu anajua kule kwao Ami yake ni mtu wa ilm sana na anasaidia watu wengi, hakujua kua ni Qareen mwenye kufanya yote yale sio mkewe peke yake. Ikaenda mpaka akazowea. Ba watu wkawa wanapata habari wanafanikiwa wakienda kwa Ali. Nina uhakika hilo ulikua hujui.

Ulipoenda wewe yule Qareen wake alimuona yule mwanamke kijinni ulienda nae, tulimwabia awe na wewe safari yoite. Yule mwanamke akaongea na huyu Jini wetu. hawa majini huwa wanaongea wenyewe kwa wenyenyewe, hio ni kawaida kabisa.
MImi: Nafahamu hilo lakini la yule mke wa Ali sikujua.
Arsis; nafahamu hukujua, ilikua haina sababu ya wewe kujua, lakini sasa nimeona nikueleze, aana alipokuja huyu mama, yule mwanamke ya Ali akamuhurumia sana, akaona yeye kua mtoto wake yupo lakini hajui wapi kwa sababu amefichwi na wachawi wakubwa, siuo rahisi mtu au jinni au Qareen ambae sio kazi yake akajua. Basi yule mwanamke akakumbuka huyu Jini wetu, akawa anamwita, huyu akatuuliza sisi tukampa rukhsa aende akasikilize anaitiwa nini ndio yule mwanamke akamuonesha yule mama akamwabia matatizo yake ndio wakanifahamisha kwa kua wao haiwezi ile kazi peke yao. Ndio tukaamua wamwambie yule mke wa Ali amkubushe mumewe wakawambie ili tuifanye kwa idhini ya mumewe. Umeelewa?
Mimi; Nimeelewa.
Arsis: Sfi sana, usiulize kitu sasa hivi najua una maswali mengi sana. Mimi nikaanza hii kazi kabla yule mwanamke hajaja, tukaweka ulinzi iliwasoiweze kuendelea kumdhuru, aKawa ameanza kupwa dawa na Jini Bakora, zakuua uchawi kwenye mwili wake. Jini Bakora ni hodari sana, anampa dawa bila wachawi kujua na majini waowachafu.

Tulipona anaweza kukolewa na anaweza kupona ndio tukaamua sasa kazi ifanyike. Simba, kazi itafanyika hivi, lazima yule anaefanya hii mambo apatikane, sisi tumeshamjua, lakini amefanya mengi sana kwenye ukoo wao, tunataka wajue na wapo wengine kwenye ukoo kama yeye. Tunataka tusafishe ukoo mzima wasisumbuliwe tena na hawa watu wabaya, mashetani wakbwa sana hawa.

Kwa hio ni lazima ukoo mzima ule uende Tanga kwa babu yako, sio shamba, pale kwake mjini.

Kwa hio wewe leo ukirudi usowaambie kitu, ongea na babu yako, na labada tayari anayo habari lakini wajib wako umfahamishe kwa mdomo wako, ukishaongea na babu yako kesho asbuhi utamwambia Ali amwambie yule mama lazima wote waje, ndugu wote, wakubwa,wadogo, kina mama, kina bibi, kina shangazi waliopo Mwanza< Shinyanga, Tabira na kokote pale lazima waje. Umeelewa?
Mimi: Imekua vizuri Mzee Ali amwabie. Na wewe wakiku[pigia na Ali akikuuliza mwabi hujui chochote hii tulioongea mwambie tu lazima waje Tanga, yeye afanye hima awaambie, waje na basi, wanazo basi kubwa za safari kwenye ukoo wao. Waje hata basi tatu au nne, mbona nyinyi binadam kwenye harusi na kwenye kuzika watu wenye pesa wote wanakenda kwa gharama kubwa popote. Hawa gharama hio kuja, kula kulala ni juu yao, usiwe na wasi wasi, wale wapo vizuri. Mengine tutapanga na babu yako na wewe. Mimi kazi hii nitakua karibu sana lakini mawasiano itakua wewe nayule Jini mwanamke. Sawa?
Mimi: Sawa/.

Arsis: Una swali lolote?
Mimi: Sasa ...
Arsis usiulize hilo swali, wewe waambie tu ndio kwenye ufumbuzi.Mengine tutaongea kesho. Kwaheri.

Mimi: haya kwaheri.

Arsis akaenda zake na mimi nikaondoka, nikarudi nyumbani, nikampigia babu saa hiyo hiyoi, akanisiliza, akanambia hakuna shida nijulishe lini wanakuja na wakiondoka huko waseme watu wangapi ili tufanyue mipango ya Tanga. Wewe uje siku moja au mboili kabla yao.
Mimi: Babu ndio hilo nilitaka kusema, mimi, kuna sababu ipi ya mimi kuja?
Babu: Sbabu ipo kubwa sana, ukija utaiona, utaelewa.
MIMI; Babu kai za watu huku.
Babu; Atazifanya baba'ko, mimi nitangea nae ukiwa tayari, hukai huku, wewe mwabie wiki moja tu, sasa usinambie mkeo sijui mwanao. Hao wazoeshe kuwa peke yao. Kwaheri babu saa nyingi.

Ka heri babu, keshonitakupigia.
abu; Okay.

Nikajua babu hataki kuongea zaidi ujumbe kisha nipa.


Itaendelea.
 
Ivi kama unaishi na una afya njema na mambo yako yanaenda...hayo mambo ya mauzauza yana faida gani ukishayaona?
Nauliza tu.
Kuyaona au kuwa nayo hayana umuhimu.

Kwangu mimi nahukulia ni kama marafiki alionoiwachia nao babu yangu.

Mimi naamini, kila binaadam ana Qareen (karina) wake, hata wewe unawako, lakini ni wa aina ipi? Mara nyingi ma Wareen huwa on the background hawajioneshi kabisa.

Kuna vionjo vya Qaree siku za mbele tutaviona. Hii ni elimu kubwa sana, Mwenyezi Mungu kawapa watu wachache sana na kwa uchache sana wa elimu hio. Binafsi sijaitafuta, sijaisomea, siijui kbaisa lakini wapo hao viumbe wakifanya shughuli zao naonekana mimi "superstar".
Hivyo vitu vipi, kisa cha Nabii suleimna kina mengi, kisa cha Nabii Musa kina Mja wa mwenyewai Mungu aliekuwa na akili sana. Wote hao hawaawatafuta wao. Ni shani yake Muumba wetu.

Unajua kuhusu pete ya Mfalme Suleiman?
 
Yesu ni cheo sio jina la mtu, Sikumbuki ni kitabu gani katika biblia kinamzungumzia Yesu mwingine aliyekua Ngariba.. nautafuta huo mstari nitarudi
Nani kaandika kuhusu "ngariba?

Wapo Yesu wengine kwenye biblia, labda a huijuwi tu:

Jesus Barabbas, Jesus ben Ananias and Jesus ben Sirach

Au Jesus siyo Yesu?
 
Tukapanda taci akamwambia mwenye taxi, nipitishe kw Issa hapo nichukue vitu vyangu. Huyu Issa ni maariufu sana duka lake la vyakula pale Kariakoo
Yah Isa namfahamu na dukani kwake mtu ni shazi muda wote na maneno yanayozungumzwa juu yake ni mengi ila haigeuzi hii str kuwa si kamba
 
Unaonesha una ujuzi wa majini, tupe elimu tufaidike.
Kiasi nawafahamu hupiga nao story sio wangu lakini wa kaka yangu yeye mi mtu wa tiba so huongea nao wakiwa kichwani bila kupanda unakuta najua naona nae yeye kumbe watu wake na hunijia sana ndotoni kama kuna jambo.

Hunifundisha sana mambo ya tiba huniambia andika kaka yako akiwa hayupo mtajisaidia wenyewe japo wameshasema akifa watakuwa kwa mtoto wa Dada yetu.

Wao ndo huniambia majinn usiamini sana wana uwongo sio kila kitu wanasema ukweli kuna vitu wanaficha hakuambii real name asli yake atakuwa rahisi kukamatwa.

Na jinn kaumbwa kwa moto akiwa karibu na mwanadamu lazima kuna athari utaipata tu sababu hawakuumbwa kuwa karibu na wanadamu sema wanapenda sana ubinadamu kuanzia life style kila kitu hata wewe ukaribu na Arsis sijui Sharrif mwenye bakora yake sijui fimbo ya hinzirani 😄utakuwa una athari umepata uwe unajua au hujui huwezi kuwa karibu haswa kama wewe ukawa sawa kuna athari mwilini umepata.
 
Kuyaona au kuwa nayo hayana umuhimu.

Kwangu mimi nahukulia ni kama marafiki alionoiwachia nao babu yangu.

Mimi naamini, kila binaadam ana Qareen (karina) wake, hata wewe unawako, lakini ni wa aina ipi? Mara nyingi ma Wareen huwa on the background hawajioneshi kabisa.

Kuna vionjo vya Qaree siku za mbele tutaviona. Hii ni elimu kubwa sana, Mwenyezi Mungu kawapa watu wachache sana na kwa uchache sana wa elimu hio. Binafsi sijaitafuta, sijaisomea, siijui kbaisa lakini wapo hao viumbe wakifanya shughuli zao naonekana mimi "superstar".
Hivyo vitu vipi, kisa cha Nabii suleimna kina mengi, kisa cha Nabii Musa kina Mja wa mwenyewai Mungu aliekuwa na akili sana. Wote hao hawaawatafuta wao. Ni shani yake Muumba wetu.

Unajua kuhusu pete ya Mfalme Suleiman?
Sijaelewa kitu Qareen mara wareen alafu Qaree Duu Elimu zenu kiboko.
 
Back
Top Bottom