Nimeacha Rasmi Kutazama Mechi za Yanga NBC PL

Tawiireeeee kakaka tawireeeee
Umewaona leo wadogo zao wa kule singidani??
Nakwambia ipo siku huu upupu utaisha...
 
Kwani ulivyoanza kuangalia NBCL ulitupa taarifa?
 
Maana yake Yanga ni bora sana kwa wakati huu. Sawa.
 
Hao Dodoma jiji kaka wakicheza na Simba ni kama mangariba...yanataka damu ni miguvu kwa kwend mbele...
Niliitazama mechi zake na dodoma au hata mashujaa. Labda tuseme Simba kwa sasa ni mid team, lakini Yanga uwezo wake ni mkubwa sana.
 
Tawiireeeee kakaka tawireeeee
Umewaona leo wadogo zao wa kule singidani??
Nakwambia ipo siku huu upupu utaisha...
Si mchezo aisee. Hata hizi motisha zinapaswa kutazamwa upya, kwanini zinawekwa kwa timu moja pekee. Kama ni matokeo chanya kwanini ilitolewe kwa timu zote zenye ubora.
 
Naomba tutafute mbinu ya kuokoa ligi yetu tunayoinasibu kuwa ni bora.
 
Mwanzo ilikua ni ngumu sana kuthibitisha, ila kama mamlaka hawata simama hata katika hii Mechi dhidi ya Singida, basi wajiudhuru tu maana kazi imewashinda.
 
Tulionya mapema kuwa hii mipango haisaidii, wote tumeona kimataifa Yanga alivyo-struggle while mechi za nyumbani anatamba tu.
 
Umoja wa timu zinazo fadhiriwa na GSS wameweka mkakati kuwa ni lazima mshindi wa Ligi atoke kwenye Umoja wao.
Wameunda hadi Wasap Group la kuwasiliana.
Mkakati ni kuwa Simba akaziwe kwa ahadi hadi za pesa.
Sijaona timu inawekewa ahadi ya pesa ili Uto wafungwe.

Tunamsubiri Mkuu wa mkoa siku ya mechi zao kama ataweka zawadi ya pesa ili Pamba ishinde.
 
Tulionya mapema kuwa hii mipango haisaidii, wote tumeona kimataifa Yanga alivyo-struggle while mechi za nyumbani anatamba tu.
5imba alofungwa mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alihongwa bei gani?
 
Umoja wa timu zinazo fadhiriwa na GSS wameweka mkakati kuwa ni lazima mshindi wa Ligi atoke kwenye Umoja wao.
Ila kupitia mechi ya leo naamini TFF na bodi ya ligi lazima wataamka kutoka usingizini. Ni fedheha kubwa kwa ligi yetu.
 
5imba alofungwa mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alihongwa bei gani?
Andiko langu linazungumzia msimu huu, labda sijakuelewa point yako Mkuu.
 
Ila kupitia mechi ya leo naamini TFF na bodi ya ligi lazima wataamka kutoka usingizini. Ni fedheha kubwa kwa ligi yetu.
Nakumbuka Singida hawa walivyo fungwa na Simba baadhi ya wachezaji walikuwa wanalia mpira ulipo isha.
Leo wanatoka uwanjani huku wanatabasamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…