Nimeachwa na mpenzi wangu jamani!

Nimeachwa na mpenzi wangu jamani!

Vzr sana, Lia weee tena jifungie hata ulie kwa sauti ili uchungu uishe then mshukuru Mungu, wewe ni wathamani na UTAPATA kilicho bora zaidi.

Ktk mahusiano yatupasa tutambue kuwa mambo MAWILI yaweza kutokea, ndoa au kubaki na jambo la kujifunza ili uwe bora zaidi. Usijihukumu wala kujuta, mbele Kuna maisha bado yanahitaji kukamilishwa na amani ya moyo wako.

Stay happy bro.
Happiness is a choice.
Ahsante sana dada kwa ushauri wako mzuri umenitia nguvu sana leo siku yangu kazini imekuwa mbaya sana siitamani tena hii siku
 
A
Pole Sana bro ila tambua tu likuepukalo lina kheri, kwanza shukuru Mungu amekuepuaha na kukutoa katika utumwa wa dhambi ya zinaa,si unajua uzinzi ni dhambi bro!!

Pia 2year ni Mingi, ulitaka ugundue Nini kwa mfano na huku mnazini🤔🤔, hayo ni mahusiano sugu pengine ameona hakuna hata dalili yoyote ya ndoa🤣
Amna ndoa mipango ya ndoa ilikuwepo ila afadhali hatujafika mbali sijui ingekuwaje aise
 
Unapitia hali ninayopitia mimi for now. Leo nimepika wali bila mafuta na chumvi nione kama ntakula. Lakini wapi. Vumillia tu. Ambaye hajui anaweza cheka.
Kabisa kaka ile time ananichana nilitamani niende chooni nikalie kilio cha mbwa mwizi we acheni tu
 
Siku kama ya 5 hivi mpenzi wangu simuelewi mawasiliano hafifu ubize mwingi si kawaida nikimuuliza ananiambia ni kazi za nyumbani maana ameenda kwao baada ya kufunga chuo so kazi za shambani ni nyingi muda mdogo.

Sasa tokea jana hatukuwa na maelewano mazuri mpka siku inaisha hakuwa sawa. Leo sasa kanitamkia Live kwamba karudi kwa jamaa yake kwa kuwa 'ametoka nae mbali' so ni ngumu kumuacha.

Nyie huyu msichna nina miaka nae miwili leo anakuja kuniacha ghafla hivi mumivu yake sikieni tu ni afadhali hata maumivu ya kutolewa roho😭😭.

Kuchwa kunauma sana hasa muda na pesa nilizowekeza kwake nikifikiria ningekuwa na mtu seriously pengine ningeshapata hata mtoto now.
Japo nimecheka na sio mazuri ila kuchezea future ya watu sio poa

Kwa hiyo ulitaka akupe mtoto tu ila kuoa aaah, ilipaswa wakati huo uoneshe nia ya kweli na kuwa serious naye


Lazima angekuzingatia tu, miaka miwili unazagamua halafu huoneshi nia ya kujenga kibanda lazima ashtuke


Anyway, tafuta utapata mwengine anaweza asiwe na sifa kama za aliyepita ila ndio hakuna namna zaidi ya kupenda unachopata
 
Back
Top Bottom