Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
uwiiiiiii"" huu Uzi sintoweza kuu handle " ...
 
aisee...najaribu kufikiria kama ningekuwa mimi ndiye na ambiwa maneno haya wakati...huuu"" kwakweli "" machozi yananitoka muda huu
 
KAKA YANGU MIMI ALIKIWA NA SARATANI YA KOO PALE MUHIMBILI DAKTARI AKAROPOKA HIVI....
"wewe ni wa kufa tu.... huna miezi miwili"

KWA HIYO USISEME MANENO HAYA KWA MADAKTARI WA TANZANIA LABDA KAMA UNATIBIWA ULAYA NA MAREKANI.
aiseeee"" Omg
 
Aiseeee...""
 
aisee...najaribu kufikiria kama ningekuwa mimi ndiye na ambiwa maneno haya wakati...huuu"" kwakweli "" machozi yananitoka muda huu

Jamaa ana bahati sana,anajua hatma yake,sio kila mtu atapata bahati hiyo mkuu
 
Jamaa ana bahati sana,anajua hatma yake,sio kila mtu atapata bahati hiyo mkuu
mkuu" hapo bado hajaijua hatima ...kuna wanaumwa kama hivyo lakini kifo chao kina kuwa NI cha ajali ya moto ""...
 
Daah, very sad !! Machozi yakiwa karibu kwa uzi kama huu lazima yatiririke.
mimi nimeshindwa kuendelea kusoma comments "" nimeona nije tu katika page ya mwisho ....huko mwanzoni sinto paweza
 
Daaaah,, usikate tamaa mkuu unatakiwa kujaribu kila njia na ikishindikana hakikisha unaenda sehem salama..


Usijione kama huna cha kupoteza kwani uhai ulio nao bila juhali uko katika hali gani ni wa thamani kuliko kitu chochote duniani.

Ningepata kua karibu na wewe ninge hakikisha unakufa kwa tabasamu.
 
Mungu anapenda kweli watu wake waumie kiasi hiki?
 
Maneno yako yameniupunguzia uoga wa kifo nilionao kwa kiasi kikubwa sana mkuu
 
Saratani ya Kongosho:

Saratani ya kongosho hutokea katika tishu za kongosho, ogani iliopo karibu na sehemu ya chini ya tumbo. Kongosho hutoa vimeng'enya ambavyo husaidia usagaji wa chakula na pia hutoa homoni zinazosaidia kusimamia sukari iliyopo katika damu.

Saratani ya kongosho kawaida husambaa kwa kasi kuelekea katika ogani za karibu. Ni mara chache hugunduliwa katika hatua za awali. Lakini kwa watu wenye uvimbe wa kwenye kongosho au ambao wana historia katika familia juu ya saratani ya kongosho, baadhi ya taratibu za uchunguzi huweza kusaidia kugundua tatizo hilo mapema.

Mojawapo ya alama za saratani ya kongosho ni kisukari, hasa pale inapoandamana na upunguaji mkubwa wa uzito, manjano (Jaundice) AU Maumivu katika sehemu ya juu ya tumbo yanayosambaa mpaka mgongoni





Matibabu yanaweza husisha upasuaji, mionzi ya kikemikali kwa njia ya dripu, mionzi au muunganiko wa vyote hivi vitatu





Dalili

Alama na dalili za saratani ya kongosho mara nyingi hazionekani au hazitokei mpaka pale ugonjwa unapokuwa umesogea katika hatua za juu. Zinaweza kuwa:

  • Maumivu katika upande wa juu wa tumbo yanayosambaa kwenye mgongo
  • Kukosa hamu ya kula au upunguaji usio wa mpangilio wa wa uzito
  • Depression
  • Mwanzo wa Ugonjwa wa Kisukari
  • Kuganda kwa damu
  • Uchovu
  • Ngozi kuwa ya njano na macho kuwa meupe

Wakati gani wa kumuona tabibu.

Muone tabibu kama unaona unapungua uzito sana bila ya sababu maalumu, au ikiwa una uchovu mwingi wenye kuendelea, maumivu ya tumbo, ngozi kuwa ya njano na dalili nyengine zinazokusumbua. Magonjwa mengi yana dalili hizi, hivyo daktari anaweza kuangalia magonjwa hayo pamoja na saratani ya kongosho.


Visababishi

Haipo wazi ni kitu gani hasa kinasababisha saratani ya kongosho , lakini matabibu wanatambua kuwa tabia kama ya uvutaji wa sigara, inaongeza hatari ya kuupata ugonjwa wa Saratani ya kongosho.

Sababu hatarishi

Sababu zinazoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya kongosho inajumuisha:

  • Uvimbe sugu wa kongosho (pancreatitis)
  • Kisukari
  • Historia ya ugonjwa katika familia (genetic syndromes that can increase cancer risk, including a BRCA2 gene mutation, Lynch syndrome and familial atypical mole-malignant melanoma (FAMMM) syndrome)
  • Uvutaji sigara
  • Unene uliopitiliza (Obesity)
  • Umri (watu wengi huonekana na ugonjwa wakiwa na zaidi ya miaka 65)





Complications & Prevention

Diagnosis & Treatment




Courtesy of Mayo Clinic

May Allaah almighty heal you from the adversity you are facing, like He cured Ayoub from what he was suffering with, and May Allaah spread his blessing and cures to all of us suffering from whatever form of illness. Get well soon folk

Further readings

Cholecystitis

Gallstones
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…