Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
i lost my friend nilisoma nae shaaban robert anaitwa Patrick Kibwana alifariki tarehe 22 June mwaka huu kama sikosei . Age 28 alikuwa na amefariki kwa Cancer ya Kongosho sasa sijui huu uzi ni wa nani . but i miss kaka yangu bestie yangu wa darasa Patrick Kibwana. forever love bro . love u
Duu
 
Hivi wewe kwanini unamdhulumu marehemu? Hayo unayoeleza hapa kama angekuwa na nia ya kuyaeleza unafikiri angeshindwa? Sasa hiyo picha uliichukua ili iwaje? Na unatumia watu ili wafanye nini? Yeye alishindwa kuwapa watu picha yake! Jaribu kuwa na utu!
Ndio ninyi mnaoamin iman za umizimu, mtu ameshakufa ,aliaga hapa wana jf,

Kwasasa hajui kitu, huo utu kwa marehemu ni upi? Ndio nyinyi mnaoamin marehemu bado yu hai,

Ndio nyinyi mlio upande wa joka maana Mungu alisema HAKIKA MTAKUFA, joka likasema HAKIKA HAMTAKUFA

watu waliasi na kuanza kufa , Joka likabadilisha msemo KUWA WAKIFA WANAENDA MBINGUNI

Ndio maana ibada za makaburin ,kusalia maiti zimekuwa nying na imekuwa fashen

Ushimen ulitakiwa uanzishe uzi ,kwa wana JAMII FORUM uweke na picha yake uambatanishe na nyuz zake alizoaga hasa hizo nyuzi mbili,

Watu humu jf wajue na Mod waifunge akaunt yake,
 
Asante mkuu. Unajua kuna watu wana mapepo wakisikia mtu kafariki wanalilia kuona picha utafikiri ni maonyeshe. Huu jamaa Ushimen ni mtu mmoja mpumbavu sana. Sijui haya yote anayofanya anafanya kwa faida gani. Marehemu alipoanzisha hii thread angekuwa na nia ya kutoa info zake si angefanya hivyo? Watu wengine wamepitiliza kwa ujinga!
Hebu achen Imani za umizimu,

Folk hakutaka kutoa details zake kwakuwa alikuwa bado HAI , na nikawaida maana jf haiaminiki siku hizi, wasiojulikana wapo, cybercrime n.k

Kwasasa ni marehemu ,details zake zikitolewa kuna ubaya gani.wana jf wengine wajue ,na wakutoa hata rambirambi kwa ndugu zake wapo,

Au mmekaririshwa mtu akifa bado anakuwa Imortal?

Zaburi 6:5 inasema, “Maana mautini hapana kumbukumbu lako: Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?”

Mtu anapokufa hawezi kukumbuka wala kushukuru au kufanya kitu chochote.

Zaburi 88:10-12 “Wafu je! Utawanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi? Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?”

Hivyo katika kaburi ni sehemu ya “usahaulifu”, “uharibifu” na “gizani”. Mtu aliyekufa hawezi hata kumsifu Bwana.

Zaburi 115:17 “Sio wafu wamsifuo BWANA, Wala wo wote washukao kwenye kimya;”

NASHAURI KWAKUWA folk aliaga wana jf, Naomba Ushimen atoe uzi wana jf wajue ,kuna watu wanaguswa wanaweza kufika kwa nduguze wakatoa chochote,
 
Mimi naona mdau aliyetoa taarifa kuwa mwenzetu ametangulia mbeye ya haki hajafanya kosa lolote sababu watu wengi apa walitaka kujua anaendeleaje .....Ila Ili la kusambaza picha zake HAPANA, sio jambo zuri
Sio zur kwanini ? Ikiwa tayar amekufa, na aliaga humu. ,ubaya upo wapi

Au marehemu atakasirika au kutatokea nn?

Ujue mmemezeshwa upuuz na hawa wachungaj na manabii wa uongo
 
Mkuu Ushimen kwa niaba ya wana jamii forum

Nakuomba uanzishe uzi Uunganishe nyuzi za mpendwa wetu aliyetangulia mbele za haki bwana folk ,

Tena ikiwezekana weka na picha ,maana kwasasa hakuna atakayemtafuta labda kwa maswala ya kisiasa,

Marehemu aliaaga wana jf, ni haki wana jf wajulishwe mwenzao ametangulia mbele za haki, hii inafaida za kujifunza vitu vingi na pia hapa kuna watu wataguswa watafikisha rambirambi mahala husika kwa utaratib mzuri ,

Hao wanaosema Sio sawa kuweka picha ,achana nao

Marehemu hawezi kurud , anasubiri ufufuo na parapanda siku ya hukumu.


Zaburi 146:4 “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea”

Sasa kama anaurudia udongo na mawazo yake yanapotea, .HAWA WANAOSEMA USITUME PICHA achana nao marehemu hajui,lolote, funzo na kujiandaa ni kwetu sisi tulio HAI.

Muhubiri 9:5,6 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu yao, husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.”
 
Kuna utu na ubinadamu katika uzi huu. Kwa wengi wetu hatumjui Marehemu lakini tuliguswa sana. Japo kuna waliokebehi na kubeza lakini wengi wetu tulikusanyika pamoja tukajaribu kumtia moyo na hata kutoa ushauri mbalimbali wa kimwili, kisaikolojia na hata kiroho. Ni mambo kama haya yanayompambanua binadamu na wanyama wengine.

Mpendwa wetu huyu keshaimaliza safari yake. Tena kapata na muda wa kutuaga. Mungu Ampe pumziko jema. Nimepata matumaini sana niliposoma hapo juu kuwa aliondoka kwa amani sana. Sisi hatujui tutaondokaje. Mungu Atupe welewa na hekima ili tukatende mema ili nasi siku yetu ikifika tuondoke kwa amani kama mpendwa wetu huyu. Katika kutuaga kwake ametufundisha mengi.

Mungu Atupe amani na kutukumbusha kuwa tu wapitaji tu katika sayari hii nzuri tuipendayo sana. [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Hembu twendeni taratb, Huyu jamaa kuna watu washafanikiwa kumfaham? (Haijalish akiwa hai au mfu), Mna uhakika gan kama ni yeye kweli maana picha tu hazitosh, kama hujawah kumwona yaweza iwekwe picha yoyote. Majib plz
 
Kwa utafiti mdogo nilio ufanye, huyu ndie mwenye na nimefanikiwa hata kuwasiliana na jamaa zake wa karibu na nikapata hata picha yake.
Inasemekena alifariki akiwa na amani tele, huku akitabasamu

Uwiii...[emoji86][emoji86][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]jamaniiiii...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom