Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Marehemu ni mdogo wake na EDGAR KIBWANA mtangazaji wa michezo wa clouds fm,

Marehemu jina lake halisi ni Patrick Kibwana



Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee ni kweli kijana amefariki. Huyu marehemu ninamjua nje ndani. Alikua akiishi kibaha na mdogo wangu wamesoma wote visiga seminary kisha yeye akaenda Shaaban robert!!

Marehemu aliitwa Patrick Na alizikwa huko kibaha. Nimethibitisha hili baada ya kuona picha yake. Mungu amrehemu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikitika nilimtaftaga PM maskini apumzike kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa utafiti mdogo nilio ufanye, huyu ndie mwenye na nimefanikiwa hata kuwasiliana na jamaa zake wa karibu na nikapata hata picha yake.
Inasemekena alifariki akiwa na amani tele, huku akitabasamu
aaaaghhhrrr.... Sina la kusema ....

Chozi limenidondoka...nimekumbuka mbali sana....MMungu ampumzishe kwa amani!
pole kwa familia...yaani maumivu yake hayamithiliki!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gf imevamiwa.. na mijitu ya ajabu ajabu..... "wakujua "..... kote ni hivyo hivyo au vimbele mbele humu tuu??
achana nao.... tupo tunaokuelewa ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka yake ni Edgar kibwana wa Clouds fm,

Ni kweli folk amefariki kati ya june 20-21 , jina lake ni Patrick kibwana

Sent using Jamii Forums mobile app
mmh...hii dunia...
kuna watu wanaoishi kama wako peponi.au mbinguni..lakini wapo pia wanaoishi kama wako motoni!..

Folk ..RIP

Aliishi kwa ....

Naamini amepumzika sasa.... ameteseka sana jamani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepitia nyuzi za folk sijaona uhusiano wowote na jina la Late Patrick Kibwana.
-Kwenye uzi wa Folk taarifa fupi amesema yeye ni mtoto wa mwisho kati ya familia ya watoto sita na ana miaka 28.
Tafakuri:-
Profile ya Patrick Kibwana walikuwa wanamwita Biggy wakati Folk mwenyewe anasema kwamba amekonda sasa kwa tatizo alilokuwa nalo na amenaza kuwa na matatizo hayo tangu akiwa na miaka 9 maana amezaliwa kwenye familia ya kimaskini.

-Moja ya melezo Patrick alisoma Visiga seminary na Shaaban Robert,kwa familia hizi za kimasikini ni ngumu kuweza kusoma Shaaban Robert ila Folk alisema familia yao ni ya kimasikin.(inawezekana labda alilipiwa na wafadhili)

Nani aliyeunganisha Late Patrick Kibwana na Member Folk?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…