Uzi naona uliwekwa April, 2018 na leo ni August, 2018. Sasa cha ajabu ni kuwa umekuja tena na maneno kuwa huenda ukafikisha miezi 8. Pole sana, ila kidume usikate tamaa ya kuishi. Wala hayo maumivu siyo ya kukuua bali kukufanya umtafute Muumba wako zaidi. Ningelitamani kifo cha jinsi hiyo ili nipatane na Mungu kwani najua sasa naiacha dunia niende kwingine na huko kuna uchaguzi. Upatane na Muumba uende kwake au umkatae uende kuzimu.
Yoh. 14:6 anasema; Mimi ( Yesu) ndiye njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa Baba (Peponi) ila kwa njia ya mimi(Yesu Kristo). Hakuna nabii mwingine yeyote aliyesema hayo ila huyu mmoja tu. Mwamini yeye uende unakojua yaani mbinguni aliko.