Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it was..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk
Ulivoandika "Tangulia tunakuja" are u sure utakuwa mzima mpka kufika hyo miez minne?
 
All the best Ndugu ...hii ndo dunia ...uwanja wa mapambano..na dhiki Pamoja na Faraja....tupe uli tufe maisha sio mchezo wa uoga ...Ukienda msalimie Mzee Nyerere mwambie sahv tunasongeshwa na muhutu...Ambiliki wali asikii... Only God know tomorrow.
 
Imeandikwa yeye aniaminiye mimi hata akifa atakuwa anaishi.Unamwamini nani?.Kufa ni faida ukiwa ndani ya kristo.Hivyo tumefundishwa kutokukiogopa kifo kwani kristo mtangulizi wetu alishapitia kuandaa njia.
Najua si jambo jepesi kuelewa ila naomba malaika wa Mungu wakufunike na kukuandalia njia salama.
Bado Mungu anasema kwake yote yanawezekana hivyo pia aweza kupindua hiyo mauti kwani waliosema hivyo ni wanadamu muulize naye Mungu.Mungu awe nawe.
 
Kaa ongea na kioo Kwa kuangalia USO na mwili wako na ujiambie Kuwa hutakufa Kwa ugonjwa huo uliotamkiwa na daktari Bali utakufa Kwa mipango mengine. Izoeshe akili Yako na roho kwa Maneno hayo ya kupinga kifo cha Aina hiyo. Utaona nafsi na mwili utavyoreact
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na pancreatic cancer stage 4.

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Bye bye Mother earth.


Dah, soo sad!
Nimesoma huu uzi wako wa 2013. Yaonekana umepitia kipindi kigumu sana ndugu. Mungu akupe ujasiri zaidi na AKUPONYE ili utuletee mrejesho hapa.

ATAYENISAIDIA HILI NITAMPA TSH MILIONI MOJA.

Inafika mahali najiuliza, WHY ALL THESE SUFFERINGS??? WHY??
WHY HARDSHIPS?? WHY DISEASES?? WHY?? WHY??

GOD IF YOU ARE THERE, WHY??????
 
Pole sana ndugu yangu kwa Ugonjwa huo uliokupata.....kuhusu kufa baada ya miez minne mi sina uhakika kama ni kweli.....mwenye kufaham hilo sio daktar wala kiumbe hai chochote....bali Mungu pekee.....UTASHINDA
 
daah wote tunakufa lakini kuambiwa unakufa lini na binadamu mwenzio ambaye nayeye atakufa mmh hatari hii, wewe mpuuze dr nae mtu tena sio ajabu akafa kabla yako ,life has no guarantee mkuu ,no one can guarantee your life eti utakufa siku fulani mh mh no lamda nabii anayeona vya rohoni,though cancer ni mbaya sana lakini sio guarantee ya kufa you can be healed.
 
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Ndugu, Folk! Nimekusoma na kufuatilia link ya uzi wako wa mwaka 2013 ambao ni kama ulianza kutoa alerts za tatizo lako. Umesema umeombewa sana, na umeenda sana kwa waganga na hakuna uponyaji...
Nijikite Kibiblia zaidi kwa sababu ndiyo mwongozo wa Kimungu kwa wanaoamini katika Yesu Kristo;
1. Kwanza tukubaliane kabisa kwamba kutafuta kupona Kimungu ulifanya sahihi, japo nimeona kwamba mambo haya ni kama yalikuwa yanafanyika kwa kuchanganywa, yaani Mungu na uganga vilikuwa vinatumika kwa wakati mmoja jambo ambalo naamini kuwa lisingekupa matokeo tarajiwa.
2. Unapaswa uchague upande mmoja wa kusimama nao...kwamba unataka uganga au unataka Yesu akuponye. Kuchagua upande kunakupa mamlaka ya kudai haki yako katika hicho unachokiamini, maana kama umechagua kusimama upande wa Yesu Kristo yeye amesema;
"hapendi kufa kwake mwenye dhambi...'', ''hapendi kumtesa mwanadamu...'', ''alikuja ili tuwe na uzima kisha tusiwe nao tele...'',
Yote hiyo ni mistari iliyo kwenye Biblia ambayo msingi wake ni kumhakikishia mwanadamu usalama wa maisha yake na roho yake. Nakushauri chagua upande wa kusimama nao ila mie napendekeza chagua kusimama na Yesu.

3. Inaonesha kuhudhuria kwako maombi hakukuchanganyika na imani katika hayo maombi. Kama utapata nafasi naomba usome vitabu vya Mchungaji Kenneth E Hagin jinsi ambavyo Yesu alimponya ila baada ya kuwa ame-struggle sana kiimani hasa kuliamini neno la Mungu. Na Biblia inasema; ''...IMANI HUJA KWA KUSIKIA, NA KUSIKIA HUJA KWA NENO LA MUNGU...'' Vitabu vichache vya Kenneth Hagin ni YOU CAN HAVE WHAT YOU SAY, RIGHT AND WRONG THINKING, TURNING HOPELESS SITUATIONS AROUND, HEALING BELONGS TO US, CASTING YOUR CARES UPON HIM, EL-SHADAI, THE BELIEVER'S AUTHORITY.
Naamini Mungu hataki ufe, at such demonic oppression. Nakumbuka mtu mmoja (msaafu wa JWTZ/JKT) miaka kadhaa alituma mwanae atafutiwe mchungaji wa kumuombea ilikuwa Dar Es Salaam, Mbagala Mbande. Mtoto wake akaifikia nyumba ya mchungaji na hakumkuta mchungaji na nilimpokea (nilikuwa mgeni tu pale), baadae kidogo mwenyeji (mchungaji) akawa amerudi na mgeni huyo akaeleza shida na nilifikiri huyo mgonjwa alikuwa anataka uponyaji na nikaomba niambatane na mchungaji kwenda kwenye mji huo ila nilipofika nilishangaa sana kukuta yule mama alikuwa anataka aombewe maombi ya kufa tu maana alikuwa amekata tamaa sana ya maisha sababu ya mapito ya magonjwa yasipona.
Kwa mara ya kwanza niliona mwanajeshi anavyolia...(shida hazina mafunzo ya ukakamavu), mwenyeji wangu (mchungaji) alinipa nafasi ya kusema na yule mama, ila niseme tu kwamba Mungu alibadilisha kila hali na yule mama naamini kuwa angali anaishi hata leo maana siku ya kwanza alianza kula na kuweza kusimama. Na mara ya mwisho nilimwacha yeye na familia yake yote wakiwa wameokoka...
Ndugu Folk, amini Mungu na utaishi
 
Na mm natamani kifo change kiwe kama chako Ili nipate mda kuaga marafiki zangu ndugu na jamaa Naona hii uliyopata ni Golden chance ....kwani Dunia sote tunapita cha muhimu kaza sana Ibada ili Angalau usikumbane na moto uko uendako Miaka 28 sio midogo ...kwani iyo ni robo karne.
 
Huu ni uzi unaotia simanzi sana maana habari ya kifo huogopesha sana kwa kila asikiaye

Lakini mimi nikutie moyo ndugu yangu Folks Mungu anaweza kufanya yote mawili anaweza kuruhusu ulale mauti lakini pia anaweza kuruhusu ukapona pia maana Yeye ni muweza wa yote

Cha msingi usiwe na hofu wala woga mwamini Mungu tu kwa lolote atakaloruhusu lifanyike. Kila siku atakayokupa jikabidhi kwake badilisha kabisa mfumo wako wa maisha uache imani nyingine tofauti na Mungu wa mbinguni, omba kwa dhati maana anasema lolote mtakaloomba kwa Mungu mkiamini mtapokea kama ilivyokuwa kwa Ayubu Bwana anaweza kutenda kwako pia.

Lakini kama akiruhusu ulale basi ulale katika tumaini ili siku akirudi uwe miongoni mwa wale watakaofufuka katika ufufuo wa kwanza maana hao wana Heri ili wairithi nchi waliyoandaliwa.

Bwana akubariki sana, akugange majeraha yako na aizidishe imani yako kwake katika jina la Yesu amina
 
Pole sana mdogo wetu
Lkn nkutie moyo tunaishi kwa Imani
Hutakufa bali utaishi ni neno la Mungu linasema
Wale ni madokta tu lkn Yesu ni daktari Pekee asoshindwa na kitu
Na Imani hutakufa
 
Option uliyobaki nayo ni moja Tu KATAA ROHO YA UMAUTI, Hivyo basi kwa Imani Yako nenda kaombewe na uombe sana kila kilicho negative kiwe positive kuanzia leo.

Amen
ofcoz mkuu aachane kabisa na kulia na kuwaza kufa ,lazima aamini hatokufa kwanza halafu uponyaji ufuate
 
daah wote tunakufa lakini kuambiwa unakufa lini na binadamu mwenzio ambaye nayeye atakufa mmh hatari hii, wewe mpuuze dr nae mtu tena sio ajabu akafa kabla yako ,life has no guarantee mkuu ,no one can guarantee your life eti utakufa siku fulani mh mh no lamda nabii anayeona vya rohoni,though cancer ni mbaya sana lakini sio guarantee ya kufa you can be healed.
Mkuu, kwa teknolojia ya sasa kuna terminal illnesses madaktari wana uwezo wa kukukadiria muda uliobaki.
No offense!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom