Hata mimi iliwahi nitokea situation ya hivi, kuna jinga moja tena ni jinga kweli kweli. Yaani nilitengeneza mchongo wangu mwenyewe ambao haukuwa na effect kwa yeyote kiofisi,
sasa lile jinga nilikuwa sijajua kama ni jinga la kutupwa nikalielezea ule mchongo na jinsi ulivyonisaidia kutengeneza pesa iliyonitoa sehemu ngumu kidogo, ebwana eeh imepita kama miezi 3 hivi mi nshasahau kabisa ule mchongo
Tupo kwenye kikao cha utendaji cha kawaida, sasa kuna watu walikuwa wana mikopo kwenye ile taasisi pamoja na lile jinga, hamadi jamaa anasema halipi mpaka na mimi nilipe ile pesa niliyomweleza almost three months back.
Likasema mchongo wote pale mbele ya wadau, unajua tena watu walivyona wivu! Nilijikuta nalitukana lile jinga mbele ya mkuu wa kazi.
Can u imagine huyu ni mtu aliyekuwa karibu yangu kinoma mshikaji ile kinoma, mvivu sana, anajua kutega sana yote haya nilikuwa namzibia mashimo! Kazi zake nyingi nilikuwa namsaidia lakini alikuja kunigeuka kisa dili la milion.