Nimeamini Kikulacho ki nguoni mwako na mchawi hatoki mbali

Nimeamini Kikulacho ki nguoni mwako na mchawi hatoki mbali

Hilo jitu unalivuta nje unalipiga mangumi kadhaa . Watu kama hao wanaibiwa wake zao
Huyu ni hatari sasa hivi nasikia huko ana cheo kwasbabu ni chawa wa Mkurugenzi wa halmashauri.
 
Hata mimi iliwahi nitokea situation ya hivi, kuna jinga moja tena ni jinga kweli kweli. Yaani nilitengeneza mchongo wangu mwenyewe ambao haukuwa na effect kwa yeyote kiofisi,

sasa lile jinga nilikuwa sijajua kama ni jinga la kutupwa nikalielezea ule mchongo na jinsi ulivyonisaidia kutengeneza pesa iliyonitoa sehemu ngumu kidogo, ebwana eeh imepita kama miezi 3 hivi mi nshasahau kabisa ule mchongo

Tupo kwenye kikao cha utendaji cha kawaida, sasa kuna watu walikuwa wana mikopo kwenye ile taasisi pamoja na lile jinga, hamadi jamaa anasema halipi mpaka na mimi nilipe ile pesa niliyomweleza almost three months back.

Likasema mchongo wote pale mbele ya wadau, unajua tena watu walivyona wivu! Nilijikuta nalitukana lile jinga mbele ya mkuu wa kazi.

Can u imagine huyu ni mtu aliyekuwa karibu yangu kinoma mshikaji ile kinoma, mvivu sana, anajua kutega sana yote haya nilikuwa namzibia mashimo! Kazi zake nyingi nilikuwa namsaidia lakini alikuja kunigeuka kisa dili la milion.
😂😂😂 Kwamba lijinga
 
Duh. Haya!
Huyo jamaa niliyemuita jinga alikuwa mshikaji wangu wa karibu na hata kwenye hiyo kazi nilimkuta, kwenye mihangaiko ya kazi ikatokea dili nikaipiga...nilitumia jina la ofisi lakini haikuwa na impact yoyote kwa ofisi.

Na wakati huo kuna jambo langu lililokuwa linahitaji pesa kidogo.(huyu jinga alikuwa analijua) so ile dili hakuna aliyejua kama imeniingizia pesa ya ziada milion na ushee hivi.

Baada ya kutatua lile jambo langu, si nikawa nampa huyo jinga hiyo habari kama ushuhuda tu, the way nilivyopata hiyo pesa.

Sasa Ofisini kuna watu waliokuwa wamekopa pesa (hapo ofisini sometimes mhasibu huwa anawakopesha wafanyakazi then wakipata wanazirudisha).

Sasa siku tuko kwenye kikao mkuu analigusia swala la madeni na watu wanaambiwa walipe, lile jinga nalo lilikuwa limekopa. Hapo ndio akarise hiyo hoja yeye deni lake halipi hadi mimi nilipe kiasi cha pesa nilichokipata kupitia kazi flani...kila mtu akahamaki pale ndani kumbuka ni kazi iliyofanyika karibia miezi mitatu huko nyuma, yaani jamaa akawasimulia staff each and everything mpaka lile jambo la kifamilia alilokuwa analifahamu yeye tu.

Alinisaliti yule boya ila nilimshinda, japo kuwa watu waliniona mpigaji. Ile kazi ingekuwa na dosari mambo yangekuwa magumu.
Nawe sikunnyingine wacha ulimbukeni wa kitoto.
Ukipiga fweza kaa kinya kama sio wewe ama ukitaka mshirikisha mtu hakikisha na yyeye anapata mgao kwenye hiyo dili.

Sio wewe upige peke yako halafu mi kazi yangu kukutunzia siri tu baada ya kunitambia kwamba umepiga.

Wacha huyo rafiki yako akutumbue maana na wewe ulikuwa na ulofa fulani.

Piga kaa kimyaaa vinginevyo toa gawiwo.
 
Huo ndio ukweli, mimi mwenyewe nimewahi kukaa na wazazi nimefanya mambo kibao lakin ilikuwa kama natwanga maji kwenye kinu.
Ndg zangu walikuwa mkoa mwingine wakifanya kadogo sifa kibao.
Bro kama nakuona vile nikijitazama. Ni hivi majuzi tu ila sikuoata kufahamu kama uadui na vita kubwa napigwa kutoka kwa familia waliyonilea tangu utoto.
Yakuelezea ni mengi ila nimeamini Mungu hulipa hapahapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibuuu.
 
Nawe sikunnyingine wacha ulimbukeni wa kitoto.
Ukipiga fweza kaa kinya kama sio wewe ama ukitaka mshirikisha mtu hakikisha na yyeye anapata mgao kwenye hiyo dili.

Sio wewe upige peke yako halafu mi kazi yangu kukutunzia siri tu baada ya kunitambia kwamba umepiga.

Wacha huyo rafiki yako akutumbue maana na wewe ulikuwa na ulofa fulani.

Piga kaa kimyaaa vinginevyo toa gawiwo.
Nimekuelewa sana jombaa, situation iliyokuwepo ndio ilifanya nikamwambia tena mshikaji hiyo kipindi alionekana kufurahia na tulivyokuwa alipaswa kuni support pia (kifedha).

Na kabla ya hapo kuna mambo niliyokuwa nimefanya kwa ajili yake. Hata ningesema nimpe mgao ingekuwa ni aibu kama angeipokea.

Hivi ulishakuwa na mshikaji akapata tatizo ambalo ulipaswa kumsuport but akalisolve mwenyewe kwa njia zake, na wewe ukapata relief?

Kusingekuwa na ile shida singemwambia chochote.
 
Hao ndio wananzengo kasahau yote kisa kununua pale..alijua nilipopata shida ya kiafya sitofanya maendeleo sitopata tena watoto nitaishia mmoja tu..wanapenda kuona tunateseka..
Pole sana..mimi ndugu zangu watoto wa mama mkubwa walinifichia vyeti vyangu ,mbaya zaidi baada ya siku kadhaa wakavitupa chooni na hii nilikuja kuifahamu baada ya mwaka kupita.

Sababu kubwa nishindwe kupata kazi niliyokuwa naifatilia...ila sijawahi kuwaa mbia na nishasamehe mara 70'.
 
Mara nyingi unaweza kudhani kwamba upo salama na umezungukwa na watu wanaokutakia mafanikio na kumbe ni kinyume chake.

Kuna mtu pale Halmashauri nilimuomba nimuweke kwenye CV yangu kama referee akakubali.

Nikampa rafiki yangu namba yake ampigie ajitambulishe kama HR officer wa shirika fulani na amuombe taarifa zangu kwani anataka kunipa nafasi ya kujitolea kwenye Hilo shirika, tukaweka loud speaker.

Huyo Referee wangu wa Halmashauri akaanza kumuambia; huyo kijana hakufai, kwanza Hana communication skills na punctuality nzuri. Tafuta vijana wengine. Ameongea mengi mazito ya negative kuhusu Mimi. Bila yeye kujua kwamba ni Mimi[emoji28][emoji1616]

Unavyodhani ndivyo sivyo, sivyo ndivyo [emoji445][emoji445][emoji2425][emoji2426].. Prof Jay ft Chameleon

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daah maisha haya aisee acha tujifunze na kuona mengi
 
Kwanza niwape big up wote wanajamii,

Experience ndogo nilioyo nayo job, hata watu wakuzidi kila kitu elimu, cheo, mshahara, kipato, magari, nyumba ila mfano wakiwa wanafahamu wewe shida tupu ila ni brain sana bado watakuonea wivu, sikuwahi kujua kipawa ni kero hata ukiwa wa kawaida
JK anakwambia mtu akikuchukia hata mkiwa mnaogelea ziwani atakwambia unamtimulia vumbi.
 
Pole sana..mimi ndugu zangu watoto wa mama mkubwa walinifichia vyeti vyangu ,mbaya zaidi baada ya siku kadhaa wakavitupa chooni na hii nilikuja kuifahamu baada ya mwaka kupita.

Sababu kubwa nishindwe kupata kazi niliyokuwa naifatilia...ila sijawahi kuwaa mbia na nishasamehe mara 70'.
Aisee 🙄
 
Back
Top Bottom