Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.
Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenyw udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.
Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.