Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.
Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenyw udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.
Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.
Ufafanuzi mzuri, umeweka details nyingi ndogo ndogo kiasi kinachofanya niamini kuwa unayosema hujayabuni tu(sina maana ni ya kweli au si kweli)
Tatizo ambalo mimi linaniwia vigumu kuamini aina hizi za story, ni kwamba zina base kwenye correlation yaani Tukio B linatokea baada ya tukio A bila tukio A kuwa sababu ya tukio B
Na sio causation, yaani pale tukio B linapotokea baada ya kusababishwa na tukio A
Kwanini naamini haya matukio ni correlation?
Let say kuna case 1000 kila mwezi ambapo marehemu kwa sababu anazozijua yeye anatoa masharti fulani ambayo yanapaswa kutekelezwa baada ya kifo chake
Then case 50 tu kati ya hizo, ndio zikaonyesha hayo madhara ya kutotimiza hayo masharti
Je cases 950 kwanini hazionyesha madhara?
Pia kwenye maelezo yako... Umefafanua kiasi gani tunaweza epuka hayo madhara
Swali langu ni "how" hii njia inafanya kazi?
Mfano Daktari akinambia ninywe hizi dawa kutwa mara tatu, kuna reason za "how" hii dawa inafanya kazi na kwanini napaswa kunywa kutwa mara tatu
Sio kwa ubaya, unaweza nipa maarifa kidogo on behalf ya kina "Tomaso" wenzangu kivipi hii njia inafanya kazi?
Kivipi jiwe dogo juu ya jeneza linaweza kuzuia kauli ya marehemu isifanye kazi
Na hii kauli ya marehemu ni nini haswa?... Masharti ya mwisho ya marehemu au "natural force" nyingine tusiyo ifahamu
Na kivipi inafanya kazi?... Ina base kwenye inverse square law pia (like 1/d^2)