Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Sio kila mtu alizaliwa kutenda mema kila mtu na mission yake iwe nzuri au mbayaKila mtu ataondoka na matendo yake hapa duniani, hata aombe akazikiwe papua island haitosaidia chochote ikiwa haukutenda mema hapa duniani, ivyo matendo yako ndiyo itapelekea uingie paradise, na ukiwa muisilamu.
Unaamini marehemu aweza kuua ila huamini jiwe linaokoaSiku jaribu kuweka hilo jiwe uone kitakachotokea! Kama hatukuziki sidhani
How old are you?Huyo marehemu ni mpumbavu? Sasa kuna faida gani? Umekataa asije kukuzika lakini mali zako anatumbua na hawara yake? Halafu unakimbilia kufumbua macho ndani ya jeneza, hivi ana akili kweli huyo mume? Na ndiyo maana akapewa sumu. Alitakiwa na yeye kulipa kisasi kabisa, sio kujifumbulisha fumbulisha macho, shame on him!
machozi kutoka ni jambo la kawaida kwa mwili wa marehemuBinafsi hatukuweka jiwe ila tuligehza jeneza mbele nyuma nyuma pakawa mbele ili marehemu asitusumbue napo cha moto tulikiona.Msiba ulifika kwa tabu sana na maiti ilikua inalia machozi kabisa ma shingo ilikua imeangalia pembeni.Kaburi lilichimbwa matatu maana mawe makubwa yalikua yanajitokeza kuzuia kuzikwa.ikafanyika mila ndio kaburi la nne likawa saaa akazikwa.Ila cha moto tulikiona
Hebu achana na ya pili nipe hiyo ya Kwanzaa ya kufungua macho popcorn[emoji897] zake ninazo mkuuHiyo ya 'sitaki fulani afike siku nikifa' nimeshuhudia matukio mawili maeneo tofauti.
La kwanza ilikuwa mke alikula njama kumwua mumewe kwa sumu. Alihangaika kwa matibabu ilishindikana. Kabla hajafa akasema mkewe asisogee msibani. Kwa jeuri ya pesa alikodi polisi wakamsindikiza kijijini kumzika mumewe wakati muda wote wa kuumwa hakujali. Aliposogelea jeneza aiangalie maiti, marehemu alifungua macho live.
La pili ni ndugu waligombana. Mmoja akasema hata nife mdogo wangu asisogee kunizika.Siku ilipofika dogo akajitosa kwenda msibani. Kiangazi mvua ilinyesha na ilipiga radi ya kutisha. Bahati nzuri haikuleta madhara. Dogo akaondolewa eneo la tukio na mvua ikaisha jua likawaka.
Wengine tunamkumbuka kwa maovu!Na nyingine akasema "Najua mtanikumbuka na tena mtanikumbuka kwa mema" kauli ya marehemu naona imetimia 100%
Ni kweli wafu wanaishiDuh!!!. Wakatoliki tukizungumza habari za wafu na kusema kuwa wafu bado wanaishi ktk Ulimwengu wa roho kuna watu huwa wanabisha na kutuona sisi washamba tusiojua Maandiko lkn ukweli ndo huo kifupi yapo mengi tusiyoyajua kuhusu wafu.
Hawajui kuwa mila inaua ila dini aiuiWajinga nyie mnayebisha mambo ya kiutamaduni,bado hayajawakuta.
HahaaaaKauli za Magufuli mnazikumbuka lakini? Alisema tusimuache Mungu
Haya mambo yapo wala usibishe ..mimi nakumbuka katika ukoo wetu tulizika mzee mmoja,wakakosea masharti katika mambo ya kimila..ilikuwa wanaume tunanyolewa nywele zinawekwa sehemu halafu kuna mzee anakwenda kuzizika shambani..basi walikosea kitu wakafa watu kama wanne mfululizo ikabidi wazee wakamwage mbege kuomba msamaha ndo ikawa pona oona yetu.Hizo ni hekaya ukifa umekufa ni giza tuu
Mliambiwa na dr chanzo cha kifo ni niniHaya mambo yapo wala usibishe ..mimi nakumbuka katika ukoo wetu tulizika mzee mmoja,wakakosea masharti katika mambo ya kimila..ilikuwa wanaume tunanyolewa nywele zinawekwa sehemu halafu kuna mzee anakwenda kuzizika shambani..basi walikosea kitu wakafa watu kama wanne mfululizo ikabidi wazee wakamwage mbege kuomba msamaha ndo ikawa pona oona yetu.
Aha haha! Hata mini atakaeoa mke wangu atajuta.Nikifa, mke wangu asiolewe
Oyaaa acheni UBINAFSI bwanaAha haha! Hata mini atakaeoa mke wangu atajuta.
"The Nun" itakuwa na afadhali kwake.
Hakuna, dawa ni kuwa Zombi tu, umuoe mke wangu halafu watoto mnawapeleka kwa bibi, acha zenu ninyiOyaaa acheni UBINAFSI bwana
Si mchezo!!! Watu mnajua Mambo ya asili.Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.
Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenye udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.
Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.
Kuna Nchi mambele huko sikumbuki vizuri mamlaka ya Anga waliambia wachawi wapunguze kupaa na mifagio usawa zinapopita ndege.Ulaya nako kuna vituko pia na mambo ya ajabu, ila kwa kuwa wao wametuacha kiuchumi tunaona km huu upuuzi hakuna.. Ni km huku mwenye nacho(tajiri) tunaamini kuna mambo hana, ukiambiwa anafanya utashangaa.. Au tajiri ana ruhusa ya kusema chochote na kuaminika kirahisi, sema wewe KAPUKJ sasaa[emoji23]
New Zealand wana mchawi wa taifa
Benfica wana laana ya kocha wao aliwaapiza jinsi walivyomkosea adabu hawatabeba kombe la ulaya miaka 100.. Mpaka sasa waishapoteza fainali km 5 hivi..
Kuna wachezaji ulayA wana imani za kiwaki, sikumbuki vizurii, km sikosei JT yeye alikuwa lazima wa mwisho kuvaa, ikitokea kavaa halafu mtu hajavaa atavua na kuvaa upya.
NOTE. sisemi naamini hizi imani, ila nasema zipo duniani koote. Si mzungu, muafrika, muhindi, wala mchina.
Tena wenzetu mambo hayo wanasomea kabisaKocha wa zamani wa Italia Marcello Lippi alikuwa anapanga kikosi kwa nyota zao za siku hiyo.
Hata uwe mchezaji mzuri vipi unaweza kushangaa siku 1 anakuweka benchi kisa nyota ysko siku hiyo haijang'aa
Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Dunia ina mambo aiseeNinayoikumbuka kuna mzee alisema sitaki siku ya kunizika mfanye mbwembwe kama sherehe kutokana na uwezo wa kifedha wa ile familia. Alisema anataka azikwe simple sio mambo ya vyakula, pombe n.k.
Sasa alipifariki watoto ni kama walifanya sherehe.. kitaa watu walihamia pale ni kula na kunywa. Siku ya maziko vivyo hivyo wakazika fresh.
Baada ya siku moja wakaja polisi wana kibali kwamba mtu aliyezikwa sio huyo. Kaburi likafukuliwa kuangalia kweli marehem sio wa familia husika. Ikabid waende tena mortuary kuchukua maiti yao na kuja kuzika kimya kimya bila mbwembwe.
[emoji2297][emoji2297][emoji2297]Kingine kichwa lazima kielekee anakokwenda sivyo hamfiki popote