Nimeamini safari ya kuitafuta na kuishika ml 100 as cash ni ngumu mno. Najitaidi lakini yataka moyo!

Wafanyakazi wengi wanastaafu bila hata kushikaa milioni 30 cash, milioni 100 ni mbali sana.
 
Wengi wangapi?? Hata kama kuna Watanzania milion moja wenye ukwasi TZS bilioni 2.5 bado huwezi kusema ni wengi kwenye taifa la kariba watu milioni 40 ambao wamefikia umri wa kufanya kazi.
 
Matajiri wana furaha tofauti na masikini, Tajiri yeye kadri pesa inavyoongezeka ndio anazidi kuwa na furaha, pia atapenda zaidi kutembea Dubai, paris n.k, weekend moja moja atataka kuwa sehemu yenye utulivu akiwa anapata John Walker, Hennessy au Moet, ahudhurie matukio ya Lions, Rotary na golf clubs. Usitegemee tajiri apate furaha yake katika ngoma za mdundiko, vigodoro, mdananda, mchiruku n.k
 
Ni huzuni kwa kweli.
 
Wengi wangapi?? Hata kama kuna Watanzania milion moja wenye ukwasi TZS bilioni 2.5 bado huwezi kusema ni wengi kwenye taifa la kariba watu milioni 40 ambao wamefikia umri wa kufanya kazi.
Nenda kwenye kamusi tafuta maana ya neno wengi.
 
Kuna pointi yangu fulani hivi bado hujanipata mantiki yangu ngoja nikupe mifano miwili labda utanielewa,shida sio kuhudhuria kwenye sehemu ya burudani shida ni je hiyo furaha anayo?
Ukienda kwenye sehemu ya starehe na tajiri muda mwingi akili yake itakuwa inahama hatokupa ushirikiano unaotakiwa muda mwingi atakuwa anafikiria madeni ya biashara yake,vitisho anavyopewa na mamlaka mbalimbali,maadui na usalama wake.
Maskini akienda kwenye furaha anafurah kwelikweli
 
Hapa kwenye timing, Nieleweshe mkuu
Inategemeana na aina ya biashara unayoifanya na mtaji wako ila kikubwa zaidi ni kumuomba Mungu akutangulie maana mambo mengi yapo nje ya uwezo wetu hata ujitahidi vp bado utakuwa na point fulani ambayo ikiguswa inaweza kukukwamisha kbs ila ukimtanguliza Mungu ana namna nyingi za kukusaidia utoboe
 
Huu ni mtazamo wako ila kwangu ni tofauti na naamini utajiri haumpi mtu furaha wala Amani vinginevyo
 
Nmekuelewa vyema.
 
Kasema nani ....huyo masikini nae atakua anawaza matatizo yake mara kodi ya nyumba, ada za watoto , madeni, Pesa za matibabu n.k
Yani inshort ni hivi Kila mtu ana level ya matatizo yake , na ni afadhali hata kwa tajiri atakua na resources za kusolve matatizo yake .


Pesa inaweza isikupe furaha ila itakusaidia kukutengenezea mazingira ya kupata furaha.

Masikini kinachowasaidia/kutusaidia ni ile hali ya I don't care
 
hongera mkuu
umewezaje? tunaomba kujifunza
 
Hapo kwenye mazao ni unyama sana maana wakenya wanavyosomba mpunga sio poa january ni mbali nadhani kufikia mwezi wa 10 bei itakuwa juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…