Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Tofauti ya elimu na dini, elimu ina facts and some evidence supports. Dini one the otherside doesnt, ina require pure imani

Siasa nayo imefanana na dini kwa mbalii ila tofauti facts zake zinafichwa, ili wanasiasa wafaidi

Utaamua utafuata kipi, vyote havipo sawa
Elimu haina facts labda kama huelewi , dini ina facts ndio maana maandishi ya muda yanatumika mpaka sasa ...Elimu yote ni manipulation yaani inapitwa na wakati ...Elimu haina majibu ni vile haina uelekeo mmoja .

Mpaka sasa elimu sio mfunguo wa maisha tena , elimu ni dini maana ni utaratibu : Mfano elimu ya sheria leo haina maana kwa vile ni utaratibu wa wazungu wala hukumu zake hazina uhusiano , ile hukumu ya kunyongwa inaweza kufutwa hata kesho ila hauwezi kubadili elimu ya dini.

Elimu na dini ni ishu pana sana , nikikuambia Hadzabe wana elimu na dini zao utakataa?

Elimu unayozungumzi wewe ni kuongea kingereza 😀 😀 😀 ukienda nchi nyingine ukakuta wanasoma mambo tofauti utashangaa.
 
Namshukuru Allah kwa Neema ya Uislam.


رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ

(They say): “Our Lord! Let not our hearts deviate (from the truth) after You have guided us, and grant us mercy from You. Truly, You are the Bestower.”

(Qur-an 3:8)

Namuomba Allah anifishe katika Uislam, Aamiin.
Kila mmoja kwa maamuzi na utashi wake.
 
Hivyo ndivyo ndivyo inavyotakiwa! Uko sahihi Kabisa! Unachotakiwa ni, 1.Mwamini BWANA Yesu,
2.Tubu dhambi zako kwa Mungu kwa Jina la Yesu
.
Yesu ndie nani?, kwanini niombe kwa jina lake ikiwa na yeye ali muimba baba ake?
 
Watu gani hao walikuwepo kabla ya dini ? Mkiwa mnaandika vitu hakikisheni mnakijua, sio mnaviandika tu.

Watu wamedhibiti kila kitu. Sasa mje na hoja na shahidi, sio maneno maneno tu ya vijiweni na ya kilevi.

Maandiko yenyewe hasa Qur'an inamtaka mtu afikiri, nakuuliza watu gani wamekuwepo kabla ya dini ? Ukute hata maana ya dini huijui, hapa ndipo huwa nawaona hamna akili.
Dini ilikuwepo kabla ya watu?
Au watu walikuwepo kabla ya dini?

Ina maana maisha yalikuwepo na watu walikuwepo kabla hizi dini hazijaanza na Imani mbalimbali.

Sasa hapo usichoelewa ni kipi?
 
Vijana mna matatizo sana. Wangapia wanazaliwa katika Imani fulani, na kwa sababu wanazozijua Wana acha Imani zao ? Nani alikulazimisha wewe uwe katika Imani fulani muda huo huo umepewa uhuru kamili. Hivi huwa mnafikiria kwa kutumia nini ?

Wewe umepewa akili ya kuhoji na kufikiri, kwanini usifikiri ? Mbona kwenye mambo mengine unafikiria iweje kwenye dini ushikiwe akili ? Halafu muda huo huo mnajinasibi na logic. Acheni ujinga vijana, dini inataka watu makini sana, hapa naikusudia dini ya UISLAMU, dini ambayo ni ya mitume na manabii wote.

Mimi nakupa miaka mikumi, uje kuthibitisha ya kuwa hii Qur'an, wazungu walikaa wakaisuka vizuri. Msifikiri kila mtu ni mjinga kama mlivyo nyinyi, ambao kwenu nyinyi kuandika msiyo yajua ni jambo jepesi sana kuliko kupepesa macho.
Mkuu kwanini unaniona mjinga ? Duniani kuna dini ngapi ? Kwanini yakwako uione ya maana kuliko zote ? Wakati wewe utakuwa Muislam sababu tu umezaliwa na wazazi waislam, leo na wap waliipokea hivyo hivyo kabla ya christianity na uislam kuja Africa watu hawakuwepo ? Walikuwa wanaabudu dini gani ? Yan hizi dini za mapokeo zimefanya umeniona mjinga , dini za mapokeo zimekufanya utengeneze matabaka, kama unaweza kuionyesha chuki wazi wazi kwenye mwezi wenu mtukufu wa ramadhani hapa nani ni stupid mimi au wewe ?.. kwanini hamtaki watu wahoji uhalali wa hizi dini ? Dunia ina dini zaidi ya 10 na man uhakika ungezaliwa shiraz huko labda ungekuwa mbahai, leo ungekuja kusema vibaya christianity na uislam, umesahau kufikiria geographia ya eneo ulilozaliwa ndio linaamua uwe dini gani? Ndio mana wazaramo wengi ni Muslim ila wachaga wengi wakristo tena RC, Sababu tu sehemu wanazotokea dini fulani ikiwa kusambazia hawa wote hawakuchagua dini wameipokea kutoka kizazi hadi kizazi, kabla ya hizi dini kuja Africa MUNGU hakuwepo? Umesahau kujiuliza kwanini hakuna Mtume hata mmoja rangi nyeusi, au kwanini hakuna hata mtume hata mmoja alotokea Africa ?
 
Dini ilikuwepo kabla ya watu?
Au watu walikuwepo kabla ya dini?

Ina maana maisha yalikuwepo na watu walikuwepo kabla hizi dini hazijaanza na Imani mbalimbali.

Sasa hapo usichoelewa ni kipi?
Huyu hafikiriii kabisa, uislamu na ukristo ulivyokuja Africa ulikuta watu ndio wakapewa hizo habari wakazibeba kama zilivyo ndio wanatutukania saivi 😂😂😂😂
 
Dini ilikuwepo kabla ya watu?
Au watu walikuwepo kabla ya dini?

Ina maana maisha yalikuwepo na watu walikuwepo kabla hizi dini hazijaanza na Imani mbalimbali.

Sasa hapo usichoelewa ni kipi?
Kwa akili yako unafikiri dini kwa ajili ya watu tu peke yao ? Huu ujinga mnautoa wapi ?

Binadamu ndio kiumbe cha mwisho cha kuumbwa.

Weka ushahidi ya kuwa watu walianza kisha ikafata dini.
 
Back
Top Bottom