Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Wabantu wengi tu kabla ya ujio wa wakoloni hawakuwa na dini hizi za nje ya Afrika.
Hawakuabudu chochote na wengine waliheshimu mizimu(mababu waliokufa) waliishi vizuri tu.
Jamii inaweza kujenga taboos, ethics, e.t.c na zikawasaidia kuishi vizuri in harmony.
Sahihi kabisa
 
Nani kakufungua macho, na aliyekuwa amekufunga ni nani?

Angalia kufunguka kwako macho kusikuletee balaa.

Kwenye dini unazozikimbia, kuna stori ya Hawa/Eva aliyedhani anafunguliwa macho na nyoka, nini kilitokea kwa wanafamu wa kwanza?
Mkuu huyo Eva ana asili ya wapi?, mbona sisi ngozi nyeusi tusiwe na kashinje wetu?
 
Wewe una dini ila mahudhurio yako ya kukutana na Wenzako kila jumapili ni hafifu au duni kabisa mkuu.
Nilikuwa naamini dini ya ukristo wa katoliki toka utotoni.
Kuanzia kipindi cha 2016 nilijiuliza maswali mengi sana na kusoma sana mambo mbalimbali.
Nikafikia maamuzi dini ni mfumo flani wa unyonyaji na vitisho unaofaidisha viongozi wa dini na waliobuni mfumo.

Inawafanya waumini kuwa wanyonge na kuwakandamiza fikra.
Nikachagua kutoamini pepo au jehanamu. Hakuna maisha baada ya kifo. Inakuwa huna maumivu, huna furaha Wala huna utambuzi wala kumbukumbu yeyote ya maisha yako ulipokuwa hai.

Hakuna adhabu au tuzo baada ya kifo. Ahadi ya pepo (Paradise) au Motoni/jehanamu (Hell) ni ahadi hewa na vitisho hewa.
Life after Death is Null and void. It is just an Oblivion.
 
Dini ni maisha ya binadamu ,dini ni mila na utaratibu ,bila ya dini hakuna binadamu ..Unataka kusema nn?

Utaratibu wa binadamu umekuwa ukibadilika ,kwanza zamani hapakuwa na umaskini ila gap la umaskini lilianza kujitokeza baada ya Maendeleo
Umasikini na masikini walikuwepo toka kale.
Umasikini ulianza jamii ilipoacha kushare rasilimali kwa usawa yaani kipindi Cha ujima.

Maendeleo ni kitu Cha kale hata kabala umasikini haujawa dhariri yaani hata kugundua moto yalikuwa ni maendeleo.

Utamaduni si dini na dini sio utamaduni.
Dini lazima ihusishe na kuabudu deity kama Allah, Jehova, Yahweh, Mulungu na wengineo.

Mila na desturi nyingi ni mazoea yaliyojiwekea jamii Fulani bada ya muda hugeuka Sheria.
Ni namna jamii inavyoweza kuendesha mambo Yao.

Watu walikuwepo kabla ya dini na dini ilianzishwa na watu.

Sioni kigumu Cha kuelewa hapa
 
Dini hizi hizi ambazo viongozi wake ni wezi, wauaji na hata wanao support mambo ya ajabu ajabu?

Papa kabariki mambo ya upinde, wale wazee wa imani wame support ndoa za miaka 9 ?
Kila mtu ana dini unless uhuni anafanya mtu binafsi kwa kuhukumu hivyo utachelewa sana.

Hata korea kaskazini ukifanya basi wewe na familia yako mtapata adhabu ,tena kizazi chako😅😅ila sio fair kuhukumu namna hiyo.

Kiongozi wa dini ni mtu ,yeye ni kufikisha neno tu basi ila ana dhambi kama wengine.
 
Nimepiga hesabu nikaona dini ni urithi mmoja wa ajabu sana, ninaamini Mungu yupo ila nita mwabudu nje ya hilo box.

Yaani unazaliwa na kukabidhiwa kitu usichokielewa au kupewa nafasi ya kuchagua.

Na hizi dini ndio zimetengeneza viumbe wenye hulka ya mazombie au vampire, ambao wao kazi yao ni kufata wasemayo viongozi au maandishi wasiyoelewa asili yake.

Mara mtu ampige au amtukane mwenzie kisa dini, yaani unajiona bora kisa dini tena utasikia wewe huendi mbinguni!.

Kuanzia Leo nina Imani na sio dini nisizozielewa.
sio kwamba mfungo umekushinda shekhe
 
Wewe una dini ila mahudhurio yako ya kukutana na Wenzako kila jumapili ni hafifu au duni kabisa mkuu.
Kwa nyongeza ya jibu lililo tangulia.
Naamini kuna Mungu na hana ukatili au utata aliopewa na waliobuni dini.
Kutuumba katuacha tufurahie maisha.
Hana sababu ya kuhitaji tuteseke sana kwa ajili yake.
Mengi yanayosemwa kakataza Mungu naamini si kweli. Tumekataza binadamu ili tuishi vizuri. Ni maadili tu na sheria zetu za maisha ambazo ukikiuka maisha yatakuadhibu ila siyo hadi ukifa huko mbinguni au motoni jehanamu.
 
Kwenye dini hapo kinachonikera nikuacha kumsaidia jiraniyangu mwenye shida let say anaumwa anaitaj 10,000 akatibiwe alafu nikaenda kuwapa hiyo ten kama sadaka miamba wenye afya zao na magar ya kifahar wakat jiran yangu anateseka. Alaf wananipiga sound et nimemtolea bwana.
Ubatili na wizi mtupu
 
Kila mtu ana dini unless uhuni anafanya mtu binafsi kwa kuhukumu hivyo utachelewa sana.

Hata korea kaskazini ukifanya basi wewe na familia yako mtapata adhabu ,tena kizazi chako😅😅ila sio fair kuhukumu namna hiyo.

Kiongozi wa dini ni mtu ,yeye ni kufikisha neno tu basi ila ana dhambi kama wengine.
Ubatili mtupu 🤣😂
 
Back
Top Bottom