Nimeamua kujilipua kwenye kilimo, nimeandaa shamba la heka tatu za tikiti na nimepanda

Nimeamua kujilipua kwenye kilimo, nimeandaa shamba la heka tatu za tikiti na nimepanda

Mkuu wasomi wa bongo hasa wa miaka hii ya Leo ni watu wa ovyo sana na ni wa kupuuza.

Wasomi wengi wa bongo ni wavivu,waoga,wajuaji na ni wajinga pia.

Ukimchukua msomi wa bongo na msomi wa Kenya ambao wako level sawa kimaisha na hawana ajira baada ya miaka miwili msomi wa bongo utamkuta yuko pale pale anaomba hela ya nauli wakati huo wa Kenya atakuwa hata anaendesha NGO yake mwenyewe.

Huyo niliyemquote ni mmoja wapo ya wapuuzi ambao wanastahili kupuuzwa kwenye hili jukwaa.



sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.

Kweli kabisa mkuu kwa hili ni [emoji817]
 
Nimeipenda sana hii mkuu. Mm niliwahi fanya kama ww baada ya project ndio nikasema walipinga sanaaaa. Ila baadae mmoja mmoja akataka TU JOINI PAMOJA. Yani ww acha tu.
Sema baada ya kufanya tu.hasara ni sehemu ya bznes
Ww dogo ulichopenda apo ni nini sasa..huyu the list na mwenzake chasha watawapoteza nyie kuweni makini sana

Mnaambiwa mfanye ujasiriamali muache shulle mtasaga meno
 
Tatizo wengi wanakimbilia kwenye kilimo baada ya kupigiwa hesabu na hawa wahamasishaji faida za kilimo kwenye semina zao.

Kilimo sio kirahisi hivi kama kinavyochukuliwa, jamaa kabla hata hajaanza kulima kaishapigia hesabu za 16M na 28M.

Ngoja ale za uso kwanza kuondolewa wenge, wengi tunamininishwaga kuwa kuna supernormal profits bila kuhusisha risk analysis and contigencies katika kilimo husika.

Yalinifika hayo quater of last year katika kilimo cha kitunguu baada ya kuzika mamilioni ardhini baada ya kupangwa na mwenzangu alielima mwaka juzi akatoka. Kuja kuvuna soko likawa limefurika mavitunguu huku kidume nna heka 6 zimesimama tayari!

Expectations zangu zikaenda na maji. Unatarajia ukapige 180 mjini Dar. Unaambiwa madago yote gunia top elfu 70 si wazimu ule ulinipata, labda uvihifadhi uje kuuza ambayo godauni kila siku unalipia huku hujui bei itapanda lini.

Mwishowe nikagawa tu mavitunguu yenyewe kwa stress nilizokuwa nazo. I was puzzled na baada ya kucheki gharama zote nilizotumia na zilizokuwa zinaongezeka tu mbele.
 
very true. Jana nimeongea na mshikaji wangu wa kateshi ambaye amelima heka 20, amesema anauhakikika wa kuvuna 450 bags za mahindi. gharama aliyotumia ni kama 12mil hivi. Kinalipa haswa.kikubwa ni kuthubutu.

Mahindi hayazingui sana kichwa na hata soko likizengua unaweza hifadhi kwenye ma ghala makubwa ukaja kupiga hela yakiadimika.

Kimbembe ni kwa haya mazao perishable, sijui nyanya au matikiti. Hivyo lazima ulie kilio cha pusi!
 
Siasa kila sehemu? Waache wadau wajadili kilimo, ujasiriamali na changamoto zake. Huyo usiempenda hata ukimshambulia vipi hatabadili maisha yako kama hautatumia muda wako vizuri kujitafutia kipato.
Mkuu Siasa ndio kila kitu... haikwepeki ndio maana mnaambiwa msipopiga kura mnajinyima wenyewe haki zenu..Wafahamu baada ya kuvuna.. hayo mazao yanakuwa katika muongozo wa Serikali? Na ukikosea kuuza mazao jela utaiona...

this time around pesa itafute kama sungura anavyotafuta majani matamu.. juu anaogopa mwewe, Tai na kipanga even kicheche.. limeni upesi upesi na msiwekeze akiba zenu zote muwe na machale machale.
 
Mbolea, madawa, bei ya mbegu, labour, gharama za kupeleka sokoni i.e gari litabeba matikiti mangapi kwa bei gani? je ni kilimo cha kutegemea mvua au umwagiliaji? Shamba umekodisha au la kwako? zingatia hayo yote kwenye mahesabu yako. Kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar wana Jf ok nilikuwa shamban hko hata network haipo vizur ,ok nimeona maoni yenu na maswali yenu pia yote ni mazur na yanalengo moja la kujikwamua kutoka point moja hadi nyingine ,Kiukwel changamoto ni zipo kwenye kilimo lakini changamoto hizo haziwez nifanya(kunifanya) nikate tamaa never ever maana mimi mpaka sasa hivi naona nimechelewa am 24yrs now with nothing than education that I graduated, kitu ambacho siwezi nkawa proud of , Sasa kama nimechelewa natakiwa kukimbia pale ambapo watu wengine wanatembea. Oh karibu sana huku ardhi ipo unakodi kwa bei ndogo tu yaani 30k up to 50k Kwa msim mashamba yapo. Huu nimwanzo tu sasa hivi naanda pia shamba la passion hekari moja naotesha miche kwenye viriba zen mwez wa 10 napanda na hii project itakuwa tayar ya watermelon .hekar moja ya passion will make me a millionaire baada ya miez 9 hadi 14 stay turned

Sent using Jamii Forums mobile app
Location ni wapi mkuu na sisi tuje
 
Naamini mleta mada toka umeanza kulima matikiti mwezi July kwa sasa utakuwa unavuna au unakaribia kuvuna. Tunaomba mrejesho maana na sisi ndio tunaanza kupanda mbegu miezi hii ili tuvune mwezi December.
 
Naamini mleta mada toka umeanza kulima matikiti mwezi July kwa sasa utakuwa unavuna au unakaribia kuvuna. Tunaomba mrejesho maana na sisi ndio tunaanza kupanda mbegu miezi hii ili tuvune mwezi December.
Kweli alete mrejesho mwezi wa tisa unaelekea ukingoni sasa.
 
Wadau habar, nina tikit-imaji ambazo zitakuwa tayar (1 acre) kuvunwa kwanzia wiki ya pili ya mwezi wa 10,naomba wadau wa masoko tafadhali.
Mzigo upo Vikindu. Mawasiliano 0714-087253 & 0784-429215 Karibuni Sana.
 
Wadau habar, nina tikit-imaji ambazo zitakuwa tayar (1 acre) kuvunwa kwanzia wiki ya pili ya mwezi wa 10,naomba wadau wa masoko tafadhali.
Mzigo upo Vikindu. Mawasiliano 0714-087253 & 0784-429215 Karibuni Sana.
Mkuu hongera sana. Hivi kwa makadirio eka moja inakuwa na miche mingapi na unaweza kutoa matikiti kiasi gani?
 
Tatizo ni soko
Hatuhitaji kujua soko lipoje, tunahitaji kujua mavuno yapo kiasi gani kwanza, je kafikia lengo, kavuka lengo au hajafikia lengo..!!!?

Kuwepo au kutokuwepo soko ni jambo jingine, kwa sababu kama ana hela anaweza akasafirisha mzigo to point B, ila uwingi au uchache wa mavuno ndo concern yetu nadhani.
 
Back
Top Bottom