We jamaa nimekuelewa sana, mie nimewahi kupitia kipi ndi kigumu sana kwenye ndoa yangu ya Awali. Nilikurupukaga kwenda kuoa bila kujipa muda wa Uchumba na kufahamiana vyema, niseme tu kuwa yule mwanamke sikua nimempenda ila nilikuwa nimemtamani kwani kumpenda kule hakukua kwa muda mrefu, ndipo nilipoona maumivu na majuto kwanini niliamua kumuoa kama sikua simpendi. Ila kwa sababu ya Dini, niliandika Taraka tatu mbele ya kikao vha ndugu. Ila nilimueleza ukweli wa Moyo nikiogopa kuendelea kumtesa kihisia nikaona afadhali nimwambie ukweli. Nilijitahidi kutokuonyesha ila sikua tu na hisia naye kabisa.
Na hili limenitafuna sana kwenye akili yangu kwani nimekua najihisi mwenye makosa sana kwa kumuumiza mtoto wa watu. Ila sasa hivi namshukuru Allah, amepata Bwana mwingine na wameshaoana na wana mtoto. Ila sitarudia ujinga wa kuoa bila kukaa kwenye mahusiano. Sijajua mtoa uzi ameandika huu uzi kufurahisha jamvi yaani Chai au anamaanisha. Polee kwa Bidada ila amemsaidia sana huyo mdada, ataumia lakini atapona na kurudi kwenye ubora wake.