Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Hongera kwa ubunifu mzuri saaana ,isitoshe biashara ya mazao inalipa saana ...cha msingi kingine ni kujarbu kuweka na mwingine stoo pia....ikibidi kwa baadae uanzishe cafe yako ili uwe ukijiuzia ww mwenyewe!! Inalipa saana!!! Big up n keep it
 
Safi nitakutafuta nikuungishe angalau kg 10
Sawa mkuu nisipopokea(nikiwa darasani) ujaribu kupiga namba ya jamaa yangu nae fanya nae haka kabiashara.Namba zote nimeziweka kwenye post number 1,yangu na ya jamaa yangu.
 
Reactions: MC7
Hongera kwa ubunifu mzuri saaana ,isitoshe biashara ya mazao inalipa saana ...cha msingi kingine ni kujarbu kuweka na mwingine stoo pia....ikibidi kwa baadae uanzishe cafe yako ili uwe ukijiuzia ww mwenyewe!! Inalipa saana!!! Big up n keep it
Asante Mkuu sasaivi najitahidi nikuze mtaji kwanza maana na plan ndefu sana kaka.
 
Nakupongeza sana. Ni ubunifu mkubwa. LAKINI Unahitaji elimu ya chuo (sijui chuo gani- University or? )kufanya hayo? Kwa nini usitumbukie mzima mzima!
Nasema hivyo kwa kukumbuka falsafa ya Prof wangu wakati nasoma education . Alisema which is better, kutumia hela nyingi kulipa ada au kumpa motot hizo hela akaanza biashara mapema? Akauliza kama baadaye utakuwa mfanya biashara za mitaani, is there a need to waste time on University education!
Hongera sana!
 
Biashara yoyote ya chakula lazima ikaguliwe na tfda (Tanzania Food And Drugs Authority). Wanakagua sio tu chakula (pengine mpunga umelimwa kwenye eneo lenye DDT), packaging na storage premises. Nadhani suala la kodi ni la kila mtanzania na kuna kodi za aina nyingi. Sina uhakika kama mchele una vat au hauna. Sikumbuki kama ulizungumzia ushuru.

Wageni aka wawekezaji wanapokuja kuwekeza kuna advantage wanazopata ambazo watanzania hatupati. Ili na sisi tufanye biashara halali lazima na sisi tupate advantage kama easy access kwenye mikopo yenye riba nafuu na misamaha ya kodi at least kwa kipindi fulani. Wewe hapo ulipo ulisha create ajira kwa ajili ya watu wawili. Tupate ushauri kwenye packaging na usafirishaji. Nk.

Nakutakia kila la kheri lakini biashara ikikua jitahidi uifanye kihalali.
 
Hakuna mtu asiekula asee ni bonge la idea keep it up
 
Mkuu nimekupata vizuri sana na katika vitu ambavyo sipend nikufanya biashara kiujanja ujanja nimeuchukua ushauri yako.

Kuhusu ushuru kuna mchangiaji mmoja kadai ushuru wa mazao umeshafutwa ingawa sina uhakika,lakini asante sana kwa mawazo wako mkuu.
 
Duu mkuu kutumbikia mazima nalo ni neno,lakini ngoja nitafute angalau hats cheti kwanza cha degree yangu.
 
usikopeshe sana ndo mwanzo wa kuangauka,,,watu hawana tabia ya kulipa madeni bila shuruti..goog idea
 
Duu wakuu kazi hii ningumu sana,sio rahisi kama nilivyofikilia,nilipata asara ya takribani kilo 170 anaenichukuliaga mchele walimuuzia Chenga badala ya mchele.Ilinibidi niziuze chenga kilo moja angalau buku na hela yangu ikawa imerudi kiasi.

Lakini namshukuru Mungu sikukata tamaa,awamu yatatu imenilipa vizuri.Na deni la munzani nimelilipa na watu wananilipa vizuri tu.Na hivi karibuni naingiza mchele zaidi ya kilo mia tano.

Pia hapa nimepopanga baba mwenye nyumba kakubali kunijenge banda la kuku,nataka nifunge na kuku wakienyeji nampango nianze na majike matano na jogoo moja.

Nimesoma sana namna yakuwafuga kuku wakienyeji kule kwenye jukwaa la kilimo,ufugaji,na uvuvi.Naamini ntaweza pia.

Nawashauli wengine wasikate tamaa pindi biashara inapoyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…