Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi


Biashara yoyote ile ina ups and downs chamsingi ni kukabiliana na changamoto na si kuzikimbia changamoto.
 
Siku nyingine jitahidi kutumia maneno yenye mtazamo chanya!
Mkuu achana nae huyo, hasara katika biashara yeyote ni jambo la kawaida.Suala la msingi nikutokata tamaa.
 
Huo mchele unauuzia wapi? Yaani hayo maelezo yako hayana budget ya frem wala mizani
 
Huo mchele unauuzia wapi? Yaani hayo maelezo yako hayana budget ya frem wala mizani
Mkuu mzani ninao nilikopeshwa,lakini now nimeshalipa deni lake.Sasa ivi naumiliki mweyewe niwangu.

Frem sina,naupaki mahali napoishi.Nauzia mama ntilie,pia wanafunzi wengi wananipigia simu nawapelekea mchele mahali walipo.

Pia nikipata muda natembea nyumba mpaka nyumba kuwaonyesha sample ya mchele anae hitaji nampelekea.Ingawa nikazi ngumu lakini inanilipa vizuri tu.
 
Jitahidi kutafuta watu waaminifu watakaokuuzia mchele huko unaponunua.

Inasikitisha mtu anakuuzia wewe chenga kwa bei ya mchele daraja la juu.

Anategemea wewe ukauzeje?

Kuna watu wana roho mbaya sana.
Asante mkuu kwa mchango wako murua.
 
Poa ndugu
 
Hongera Kwa kuthubutu kwako kikubwa Uwe mvumilivu,kuwa mbunifu, nidhamu, Uwe Makin, uweze kuiongoza biashara yko, kuwa mwaminifu na mkweli na kufanya kazi kwa bidii na maarifa hasa uweze kuiongoza na kusimamia biashara kwani wengi hushindwa hpo hsa ukizingatia ww ni mwanafunzi.
 

usiseme ni ngumu watu watakuona machinga ila mwenyewe unajua unachofanya acha waendelee na usharobaro! niliwahi uza hereni nikiwa chuo dozeni jumla manunua 12,000/ nauza @ hereni 1 shilingi2000, 2000×12×8 kwa mwezi faida ni kama 96 minimum sometimes hadi 120,000/ nlikuwa napata hapo nikienda chuo nnazo kwenye handbag tu wala huwezi jua nimebeba kitu hyo biashara ilinipa hela ya kula full time na sikuwa na boom watu walikuwa wanaona nafanya ujinga flan hivi[emoji1] [emoji1] hadi nikaikuza nafanya ingine zaidi
 
Asante Madam kwa mchango wako,ngoja niendelee kukomaa namshukuru Mungu nachopata ingawa si kikubwa lakini kinanisukuma.
 
Mkuu asante sana.
 
Hongera sana kijana....Idea yako mzuri...mwezi ulipita kaka yangu alinitafuta na kuniambia ana shilingi milioni 5.Anataka kuanzisha biashara lakini hajuwi aanze biashara gani....Nilimshauri wakati huu wa msimu mikoani nenda kanuniue mpunga then sangisha uanze biashara ya kuuza mchele.Muda huu yuko mkoani na ameshaanza kununua...Kwa uchumi wa kipindi hiki biashara ya nafaka ndio utapata wateja....kwani ndio hitaji kubwa la mwanadamu kuliko nguo ama makazi....Hongera sana kjana na Allah atakubariki....Waarabu wana msemo wao hesema MANIJITAHADA WAJADAA(kila mwenye kujitahidi atafanikiwa),,,,,,
 
Hongera, endelea kupambana,
 
Hongera.. Upo chuo gan mkuu?
 
safi sana mkuu..mtaji ukikua jaribu kuboresha biashara yako weka na unga wa sembe..vitunguu..karoti nk..trust me soon hautakua hapo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…