Nimeamua sasa kuachana na ualimu na kwenda kusoma

Nyie watu mnaongea tu hamuijui kigoma vzuri... mm namuelewa jamaa kwasbb nimeishi kigoma huku hata uwe na million 100 kama sio mwenyeji wa kigoma inaweza kuisha bila ww kujua...!!! Ww mkoa wachanga wameushindwa unafikiri kuna biashara hapo
Aisee very sad
 
Nyie watu mnaongea tu hamuijui kigoma vzuri... mm namuelewa jamaa kwasbb nimeishi kigoma huku hata uwe na million 100 kama sio mwenyeji wa kigoma inaweza kuisha bila ww kujua...!!! Ww mkoa wachanga wameushindwa unafikiri kuna biashara hapo
Hawaelewi mkuu, kigoma sio mji wa kuwekeza, hela itapotea yote mwisho wa siku nimekata shauri ya kusoma hiyo IT, uzuri mimi ni mtu wa msuli nitapambania wanipe ruhusa kwenda chuo wakininyima nitakula open tu.
 
1. Ruhusa ya kwenda chuo
Ruhusa hutolewa tu ukipata barua ya kuthibitishwa.
Hayo ya miaka mi3 kwanza achana nayo..!!
Mfano:- niliajiriwa Feb/2012 na May/2013 nilipata barua ya kuthibitishwa Ila Oct/2013 nilienda chuo kusoma bach..!!
Niliongea na watu (wasaidizi wa mkuu wa idara wa kipindi hicho) nikavaa viatu.

2. Tunakubaliana kwamba serikali haiajili Masters, hivyo bachelor mpya kwako lazima.
Mimi niliajiriwa na diploma ya kitu x ila nilienda kusoma kitu y.
Wakati huo nipo katani, hivyo sikuwa na taarifa yoyotee kwamba "halmashauri fani fulani haina watu" ila nilienda kusoma ile course ya ndoto zangu.
Hivyo kilichonipeleka shule hakikua kwamba nimeona fursa idara fulani Ila ni moyo ndio uliochagua course.
Hivyo nilienda chuo kutimiza matamanio yangu na ndoto zangu za elimu.

3. Chukua huu mfano:-
I. Kuna jamaa angu alisoma bachelor of science in education with IT.
Akawa anasaidia halmashauri kama IT, ila haikuwezekana kufanyiwa recategorization ya u-IT kutoka ualimu hivyo ilimlazima kusoma tena U-IT bachelor mpya, alifanya hivyo na sasa ni Afisa Tehema wa halmashauri yetu.
2. Kuna jamaa angu yeye alikuwa ni mwalimu, hivyo yeye alisoma Accounts by means of NBAA, akaanza foundation mpaka CPA, sasa hivi anasubiri recategorization (kamaliza bachi iliyopita ya CPA). Ila yeye Alikuwa mjini, hivyo evening classes kwake haikuwa shida kabisaaa.

4. Nakushauri omba ruhusa kasomee huo U-IT unaoupenda.
Je ruhusa ya miaka 3, sasa hapo sijui kwa halmashauri yako.
Ila kwangu, niliomba kusoma bachelor nikapata ruhusa.
Bachelor ilivyoisha nikarudi kazini na swaga za kuwa nimepata scholarship ya masters (ulikuwa Uongo mtupu) nikawajaza wakajazika. Nikaenda kusoma masters..!!!
Kwahiyo mi naamini kwenye hiyo idara ya elimu yupo mtu hapo halmashauri mnaelewa hebu mfate akusafishie njia kwa mkuu wa idara. Au tafuta uongo wowote ukauombee ruhusa..!!!

5. Chakukushauri, soma mapemaa kabla ya majukumu kuanza.
Miaka 26 ni perfect sanaa, komaa kwanza na elimu kabla ya familia.
Mimi hili jambo la kutokuwa na familia masomo kulinifanya shule iwe mtelezo sanaa. Ila kwasasa nilivyopata watoto tu "Basi PhD nimekuwa naitafakari sanaa kwasababu ya kuacha wanangu mimi nipande ndege""

6. Biashara
Hili jambo ni akili yako tu.
Binafsi Mimi kazini kwangu siku ona fursa na mpaka Leo sijaona fursa niliyoielewa.
Wakati nasoma nilianzisha biashara ya stationery huko huko chuoni (nilienda chuo na mil 7 saving) ilikuwa kubwaa, niliifanya kwa miaka 3 nilivyomaliza bachelor nikaiuza na kupata hela/ada ya masters.

KASOME KILE UNACHOPENDA NA KASOME MAPEMA SANAAA.

Hayo ya biashara yenyewe yatajiset kutokana na exposure unayoendelea kuipokea unavyo zurura kwenye hii dunia..!!!

Tuendelee kujadili.

#YNWA
 
Shukrani sana mkuu hapo umemaliza Kila kitu.
 
Unamiaka 26 umesema naomba kujua yafuatayo
1. Chuo umemaliza mwaka gani?
2. Umeajiriwa mwaka gani?
3. Una muda gani kazini toka uajiriwe?
 
Betting nimeliwa sana sioni mapya kupitia betting, hata hiyo million 15 inaweza kubaki 0 kwa muda wa mwezi mmoja TU, Sasa kama Jana liver kafungwa na Atalanta utamshawishi nani aone betting ni Bora?
Kwani hiyo 15mln uliipataje? Nadhani uendeleze hapohapo, kama umeuza miti ya babu hapo sawa.
 
Ningekuwa mimi, naenda benki nakopa 25mln, 25mln +15mln=40mln, 30mln napereka kwenye biashara, 10mln ni marejesho ya kila mwezi, baada ya mizi 6 tayari nina 10mln nyingine ya marejesho, hivohivo mpaka mwaka unaisha.
 
Umehitimisha vizuri sana.
 
mwenyewe nafikiria kwenda kusoma ila sasa nawaza nafamilia tayari mke na watoto wawili, yaani nikatoe hela nilipe ada hizo hela zinaniuma, pili nikisha hitimu hicho kisomo kitanisaidia nini hapa nina miaka 31.
Umeongea vyema sanaa, kusoma ukiwa na familia ni MTIHANI MKUBWA.
Mi nilivyoajiriwa tu nikiwa na miaka 22 nilikimbilia mapema chuo kusoma bachelor na masters.
Ila sasa tangia nipate watoto kusoma hito PhD naona mtihani, yaani niache wanangu TZ mi nipande ndege..!!
HAPANA KWA KWELI.
Ila najua nisingekuwa na hawa watoto ningeenda..!!!

#YNWA
 
Hapa umetisha.
 
Mpaka hapo,inaonekana huna akili kabisa.Weka Kwanza matokeo yako Kwanza ila ficha jina.
Ili tuone tunamshauri mtu kweli au mtu fake.
Wewe ni mzigo Kwa Taifa.

Shule zetu za Umma zinateseka kuwa na watumishi dizain hii.
 
Well said!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…