Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
Kama Kasulu kuna fursa kwa nini usiombe uhamisho uende huko?Niko manispaa mkuu, mjini hapa, at least ninakuelewa, ningepata nafasi ya kuhama kwenye manispaa au majiji nisingefikiria kwenda kusoma maana ningeanzisha biashara immediately, lakini akili haijatulia kwa sababu sioni fursa za biashara kabisa, mji mgumu huu, Bora kasulu kuliko mjini hapa.
"As long as" huko ndani ya ajira tena ajira ya ualimu hutoboi na utakuwa masikini milele! Chukua maamuzi magumu huku ukimtanguliza Mungu! Umesema hujaoa na hela ya mtaji unayo! Maeneo ya mbezi mwisho ni maeneo mapya yenye msongamano mkubwa wa watu na wengi zaidi 75% ni wageni (hakuna uswahili)! Tafuta chumba cha karibu upange anzisha biashara ya vyakula. Ukipata watu sahihi utakaowaajiri utatoboa!Nimetenga mpaka 1.5 m nihame huu mkoa, nifike hata kibaha tu lakini Ngoma imekua ngumu, nadhani kwa sababu sijampata mtu sahii wa kunifanyia mchongo.
Shukrani sana mkuu nimekuelewa."As long as" huko ndani ya ajira tena ajira ya ualimu hutoboi na utakuwa masikini milele! Chukua maamuzi magumu huku ukimtanguliza Mungu! Umesema hujaoa na hela ya mtaji unayo! Maeneo ya mbezi mwisho ni maeneo mapya yenye msongamano mkubwa wa watu na wengi zaidi 75% ni wageni (hakuna uswahili)! Tafuta chumba cha karibu upange anzisha biashara ya vyakula. Ukipata watu sahihi utakaowaajiri utatoboa!
Shukrani sana Mkuu, ngoja niwaze kwa upande huu, sijawai kufikiria kabisa.Optimists
Mkuu nafikiri ukiweza fanya michakato ya kusoma nje haswa Western countries, yaani endelea na masters.. NI vema Sana Kama unampango was kufanya kazi hukohuko.
1.. Tafuta nchi ambazo Zina sera nzuri za kufanya kazi na maswala mazima ya uhamiaji Kwa wageni.
2.. Nchi zinazotoa government scholarship, zinazokubali kiurahisi mifumo ya elimu ya Tanzania
DOKEZO: Sweden...
✓Wana government full funded scholarship.
✓Tanzania ni eligible
✓No English test
✓ minimum ni 2 years of work experience
✓Centralized University application system
✓Hulazimishwi kurudi in your home country baada ya kumalizia masomo
Zipo nyingi mfano Canada,USA,German
100%ukiona mtu anaomba ushauri hawezi kuachana na kitu maanake anahofu. Pia usitegemee mawazo ya watu ufikirie utatoka huna self-esteem. Ni sawa na mapenzi ukiona mtu anaomba ushauri huyo bado anapenda
Mimi ninakuelewa ila post yako ya kwanza kwenye mada imebeba mawazo na fikira zoote za huyu dogo.sema una busara ungelijibu vibaya ningejua IQ yako cha kufanya tafuta connection ya kuhamia maeneo yenye biashara na vyuo kwa ajili ya kusoma.
Na maanisha usipohama hilo eneo ukahamia sehemu zenye mzunguko wa hela kama Dar... utaenda kusoma ukimaliza utarudishwa huko huko pia hadi upewe IT au cheo chochote ni connection.
Tafuta connection ya uhamisho ama nenda kusoma ila weka akilini neno kuhama na connection.
ukiendelea kuwaza kufanyiwa re-cate utatumia nguvu kubwa halafu mwisho utakuja kukata tamaa maana mshahara ni mshahara tu hautoshi.
Nikupongeze kitu kimoja umeshagundua kuwa ajira ni utumwa. Neno mtumishi kwa mimi mwanalugha (a linguist PhD) limejificha kwenye maana ya msingi "mtu anayetumwa" yaani anayetumika kwa niaba ya mtu fulani ambaye anapata faida kukutumia anavyotaka.
Poor Brain Intelligent businessman
Narudia Tena mkuu, siwezi invest million 15 alafu nikauza 60,000/= kwa siku na Mimi nikajitapa kwamba Nina biashara huo ni ujinga, ningekua kwenye miji mikubwa ungenishangaa sana, lakini kwa kigoma ndio nimeshindwa ning'amue nifanye nini, nimefanya biashara dar kwa mtaji wa million 1.5 nilikua nauza viatu hapo karume kwa mwezi nilikua sikosi laki 5 hapo nimeshafanya kila kitu, hapa nazingumzia kigoma, hizo idea za kufungua kijiwe cha kahawa sio mambo yangu ndoto zangu ni kubwa zaidi ya hizo.
Shukrani sana mkuu, kwa sababu ndoto zangu ilikua ni IT na nikaona open university hawatoi hiyo kozi upande wa degree, ndio nikaja na hiyo idea ya uhasibu.
Shukrani mkuu, Mimi hii naisoma mwaka huu huu.View attachment 2961824
Siku nyingene fanya research vizuri open wanatoa degree ya IT We jiandae TU muda ukifika uombe usome
Ipo nadhani umeshindwa kuona tu,inaitwa bachelor of Science in information communication and technology (ICT)Nimeangalia Nimeikosa mkuu, wanatoa kwa ngazi ya certificate sio degree.
Health service? Management ?Nakushauri nenda kasome Course inaitwa HSM(Health Service Management) Ukatibu wa Afya inapatikana Mzumbe University na St John University sijajua kama UDOM wameanza kutoa.
Faida yake ni kwamba ukifanyiwa Recategorizing Salary haitoshuka wanatumia viwango vyao vya Salary ambavyo nitofauti vya Food n Nutrition ambavyo salary Yao iko chini.
Pia IT ni nzuri sana na wakikufanyia recategorizing hutoathirika Salary wananzia TGS E ambayo ni Million na kidogo.
Mm nimesoma Degree ya Educationa nimeona NILIKOSEA nimeamua kurudi tena kusoma Health Service Management namaliza mwakani, ila ni msoto mkali sana aisee no Boom lakini najua nilimaliza tu nitakuwa pahala sahihi sana.
Nyie watu mnaongea tu hamuijui kigoma vzuri... mm namuelewa jamaa kwasbb nimeishi kigoma huku hata uwe na million 100 kama sio mwenyeji wa kigoma inaweza kuisha bila ww kujua...!!! Ww mkoa wachanga wameushindwa unafikiri kuna biashara hapoWatu wanatoboa na milioni moja mkuu...ni mipango mizuri na target tu✊🏽
Ila hapa lazima akomae fuvu unit 40 za open co poa kabisaView attachment 2961824
Siku nyingene fanya research vizuri open wanatoa degree ya IT We jiandae TU muda ukifika uombe usome