Nimeangalia filamu ya Royal Tour. I was not impressed. Itawakera sana baadhi yenu

Unadhani huo upande usiojulikana Sana unaweza kuvutia watalii wengi zaidi kuliko kuonyesha kuonyesha vivutio vinavyojulikana sana kama mbuga za wanyama ?
 
Reactions: Tui
Ndio maana anko magu alilijua Hilo
 
Tofauti tu ni kwa Rais wetu kushiriki hiyo tour otherwise hakuna kipya!
 
Hata Pepsi tunaijuwa lakini hujiulizi kwanini kila siku wanatangaza hiyo hiyo Pepsi
 
Reactions: Tui
Tofauti tu ni kwa Rais wetu kushiriki hiyo tour otherwise hakuna kipya!
Hakuna cha tofauti hata hizo nchi zingine pia viongozi wao walishiriki. Israel the royal tour 👇


Rwanda the royal tour 👇




Ukisoma post ya #11 na #98 kwenye uzi huu utaelewa kila kitu.
 
Filamu bila scene ya malove love haiwez mpendeza mtu mweusi

Hiki kipengele wangejitahid kikawepo,ili kuonesha uzur wa mahotel yetu
 
Sio lazima kila kitu kipendwe na wote,hata wewe wapo wasiokupenda na wapo wanaokupenda,huwezi kupendwa na watu wote.
 
Kama haijakufurahisha ujuwe wewe siyo target audience. Endelea na kazi yako inayokupa shibe.

Hiyo ndiyo layout yake kadri director alivyoiandika. Peter Greenberg hajaanza kuandika na kushoot royal tour ya Tanzania. Soma hapa;
"He also produces and hosts a television series called The Royal Tour which airs on PBS. The series features various heads of state giving Greenberg and viewers a personal tour of their country. It has featured a number of world leaders including New Zealand's Helen Clark, Israel's Benjamin Netanyahu, Abdullah II of Jordan, Peru's Alejandro Toledo, Mexico's Felipe Calderón, Rwanda's Paul Kagame, Poland's Mateusz Morawiecki and Tanzania's Samia Suluhu Hassan. Greenberg was previously the Travel Channel's chief correspondent."
 
Hata Pepsi tunaijuwa lakini hujiulizi kwanini kila siku wanatangaza hiyo hiyo Pepsi
Wanao sema hawajaona jipya hawajui nguvu ya matangazo ya biashara.Hii ni documentary ni tangazo la biashara.
Bidhaa au huduma huwa zinatangazwa mara kwa mara ili mteja anase na kuvutiwa kununua huduma au bidhaa.
Ndio maana baadhi wanakosoa bila kujua azma ya hii documentary.
 

Muwe mnapongeza basi yeye kathubutu
 
Tangu lini mpemba akajua mambo ya utalii wa mbuga, yeye mpeni mashua akavue samaki arudi nyumbani ale urojo
Wapemba ndio walistaarabika kwanza,ndio ukaona hata Msumbiji kuna mji waitwa Pemba.Hata mahindi yalianza kulimwa Pemba,mbegu ilipotoka India,ndio ikasambaa kwingine.Na ndio chakula kikuu Afrika mashariki na kati.
 
Reactions: Tui
Na wao pia nasikia wanatoa filamu yao inayoonyesha Mlima Kilimanjaro na serengeti zipo kwao...Filamu inaitwa the Tour Guide
 
Umesema kweli,sisi wananchi,sasa tumeelewa kwa nini,wanaumia kuhusu hii filam,kumbe walikuwa wanajitangazia vivutio vya Tanzania ni vya nchi nyingine.
 
Hata hapa itazinduliwa, Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…