Baada ya kukaa muda mrefu bila kujihusisha na ufugaji wa aina yoyote, kuacha mbwa mmoja ambae namfuga kwaajili ya ulinzi, mwaka jana, 2024 mwezi wa kumi mwanzoni, niliamua kuanza ufugaji wa Sungura kwaajili kupata mboga kwa matumizi ya nyumbani na pale patakapokuwa na Sungura wa ziada, basi nitawauza niingize kipato kwaajili ya kuendeleza zaidi ufugaji huo.
Katika thread hii ntajitahidi kutoa taarifa kwa kadri ya uwezi wangu, kadri mradi huo utakavyokua ukiendelea, ninakaribisha maoni, ushauri, na maswali. Namuomba Mwenyezi Mungu aniongoze katika hili jambo.🙏🏿
baada ya kufanya utafiti kidogo, kukusanya taarifa na kuandaa fungu la pesa kwaajili ya mradi huo, niliamua kuanza ujenzi wa kibanda cha kufugia chenye vyumba viwili. Niliamua kujenga banda kwa kutumia vifaa vya chuma, na nyavu za chuma. (nita weka picha baadae kidogo)
Nilitafuta fundi, akafanya kazi hiyo vizuri sana, namshukuru Mungu, banda likaisha salama kabisa. Baada ya kujenga banda, nikatengeneza viboksi vya kuzalia (nesting boxes) viwili, kwaajili ya kila chumba (cages) hapo banda likawa limekamilika. Kazi yote ya kujenga banda pamoja na kutengeneza nesting boxes ilichukua wiki moja. Baada ya hapo, nikapumzika kwanza.
Itaendelea.....
Updates zote ziko kwenye posts zilizofwata huko mbele kwenye huu uzi