Nimeanza safari ya ufugaji Sungura mwaka jana (2024) mwezi wa kumi, namshukuru Mungu, nimeanza kuona maendeleo taratibu, hatua kwa hatua

Nimeanza safari ya ufugaji Sungura mwaka jana (2024) mwezi wa kumi, namshukuru Mungu, nimeanza kuona maendeleo taratibu, hatua kwa hatua

sasq sungura na kuku ambaye ni ndege wanafananaje sungura mfananishe na paka au mbwa hawa ndio wanafanana na sungura
Nimefananisha nyama, nyama ni nyama hata nyama ya kuku naweza ifananisha na ya nyoka au mamba.
 
Mkuu sio kweli labda upenzi/ushabiki tu ya kuku ni tamu sana. tumewawinda sana machungani na kula sana nyama zao mwaka 2006 nikafuga kienyeji wakatoroka wote walikuwa 4. mmoja akawa anarudi yaani anapotea kama siku3 au wiki halafu usiku anarudi .

Sasa hivi sili sio kwamba wamenishinda yaani kuamua tu na kutokuvutiwa nayo tena
Basi umewazoea sana mkuu, ila sungura ni mtamu aisee.

Mimi sijala sana sungura
 
Nimefananisha nyama, nyama ni nyama hata nyama ya kuku naweza ifananisha na ya nyoka au mamba.
hhhhhhh,,,,,,,wewe nimekuelewa unaifananisha na kuku ili kujifariji kiufupi unaakili ndogo sana hii ndio sababu unakula nyama za ajabu ukiulizwa unataja kuku ili kupumbaza akili.
 
Baada ya kukaa muda mrefu bila kujihusisha na ufugaji wa aina yoyote, kuacha mmbwa mmoja ambae namfuga kwaajili ya ulinzi, mwaka jana, 2024 mwezi wa kumi mwanzoni, niliamua kuanza ufugaji wa Sungura kwaajili kupata mboga kwa matumizi ya nyumbani na pale patakapokuwa na Sungura wa ziada, basi nitawauza niingize kipato kwaajili ya kuendeleza zaidi ufugaji huo.

Katika thread hii ntajitahidi kutoa taarifa kwa kadri ya uwezi wangu, kadri mradi huo utakavyokua ukiendelea, ninakaribisha maoni, ushauri, na maswali. Namuomba Mwenyezi Mungu aniongoze katika hili jambo.🙏🏿

baada ya kufanya utafiti kidogo, kukusanya taarifa na kuandaa fungu la pesa kwaajili ya mradi huo, niliamua kuanza ujenzi wa kibanda cha kufugia chenye vyumba viwili. Niliamua kujenga banda kwa kutumia vifaa vya chuma, na nyavu za chuma. (nita weka picha baadae kidogo)

Nilitafuta fundi, akafanya kazi hiyo vizuri sana, namshukuru Mungu, banda likaisha salama kabisa. Baada ya kujenga banda, nikatengeneza viboksi vya kuzalia (nesting boxes) viwili, kwaa kila chumba (cages) hapo banda likawa limekamilika. Kazi yote ya kujenga banda pamoja na kutengeneza nesting boxes ilichukua wiki moja. Baada ya hapo, nikapumzika kwanza.

Itaendelea.....
 
hhhhhhh,,,,,,,wewe nimekuelewa unaifananisha na kuku ili kujifariji kiufupi unaakili ndogo sana hii ndio sababu unakula nyama za ajabu ukiulizwa unataja kuku ili kupumbaza akili.
Kijana tafuta kijiwe cha unywaji upate moja moto moja baridi upooze akili.

Mambo ya nyama ya kuku ndio hadi uniite nina akili ndogo 😂😂😂.

Uko wapi kwanza nikuletee kitimoto na bia mbili??
 
Kijana tafuta kijiwe cha unywaji upate moja moto moja baridi upooze akili.

Mambo ya nyama ya kuku ndio hadi uniite nina akili ndogo 😂😂😂.

Uko wapi kwanza nikuletee kitimoto na bia mbili??
naona huwezi kula sungura kwa amani hadi ujipumbaze kidogo akili kwa kufananisha na kuku alafu unajisemea nyama ni nyama kisha ndio ule huoni huna akili mkuu, mimi nakula ng"ombe, kuku, mbuzi, samaki mwisho sili nyama tofauti na hizo na pia nakunywa maji, juice, maziwa n.k wala mimi sio mlevi sinywi bia wala gongo.
 
Kwahiyo asiekula unachokula wewe ama akisifia anachokula dhidi ya unachokula ni hana akili??

Binafsi ukinipa kuku na sungura nachagua sungura, na nimetumia nyama ya kuku maana ni popular na watu wengi mnaihusidu kua ni tamu kuliko zote, hiyo nyama ya ng'ombe unayoipenda kwangu haifui dafu kwa kitimoto , ajabu "genius man" kashindwa kung'amua kua binadamu tunatofautiana mpaka atukane.

Badili hiyo Id, unawaaibisha genius wa kwelikweli.
 
kwasababu umeniambia nyama ni nyama tu inamaana wewe unaweza kula hata nyama za watu mtu mwenye akili, genius lazima awe na mipaka kwenye vitu wewe unakula nyama yoyote ili mradi ni nyama lakini genius naangalia virutubisho na point za msingi kama magonjwa n.k kwasababu wewe unaangalia utamu wa nyama pekee ni wazi unaweza kula hata nyama ya mtu huna mipaka wewe sio smart

mimi nakula nyama kwa kuangalia ni nyama ya nini na vipi magonjwa yake na wala sili kwa kuangalia utamu sijui kwasababu tu ni nyama kama wewe naweza kusema wewe huna akili hata bia wala gongo sinywi kwasababu siiangalii vitu negative hetu utamu naangalia point za msingi katika uhalisia hakuna point yoyote ya muhimu kwenye bia, wala sungura, wala ngurue bali vina madhara makubwa kwenye mwili wa binadamu hivyo anaetumia naweza kusema hana akili.

kumuita mtu hana akili sio tusi inategemea limetumika katika mazingira gani mfano wewe unakula nyama kama nyama ili mradi ni tamu tu bila kuangalia magonjwa na point za msingi ni halali wewe kuwa huna akili nikimaanisha hujui unachokifanya kwa undani zaidi huna maarifa na hicho kitu.
 
Wapi nimesema "nyama ni nyama" wapi nimesema nakula binadamu ndgu "genius".?? Mbona unanilisha maneno aiseee.

Bandiko reefu na hamna ukichoandika chenye maana, nilitegemea mpaka sasa uwe ushaleta sababu za kisayansi za kutokula sungura na nguruwe sio hizo blah blah.

Kumuita mtu "hana akili" ni defending mechanism wanayotumia(ga) sana watu wasiojiamini na wasio na uwezo wa kujenga hoja na kueleweka, hivyo kuijengea hofu hadhira yake.

Jenga hoja sio vioja.
Karibu genius.
 
💉 soma hapo
Hukuelewa, yes nimeifananisha nyama ya kuku na nyama ya sungura coz zote ni nyama. Au mantiki yako ni kua nifananishe ndege kwa ndege, mnyama kwa mnyama??

Hiyo stateme ya "nyama ni nyama" haina maana nakula nyama zote..
Aloo we jamaa unatumia nini kufikiri?

Aisee genius usitumie hisia, tumia akili.
 
sawa sawa
 
😋
 
Attachments

  • 6A98D600-6A82-4033-A7DB-013F35CC654E.jpeg
    6A98D600-6A82-4033-A7DB-013F35CC654E.jpeg
    83.1 KB · Views: 3
Baada ya kumaliza kujenga banda nikaanza kutafuta mbegu. Kwasababu ya ufinyu wa bajeti, nikaamua kuanza na sungura wachache. Nilianza na New zealand white wawili, mmoja dume.na mmoja jike, pamoja na flemish jike mmoja.

Chakula wanachokula mpaka sasa ni majani, matembele, mchunga, kabech na karoti. Pia mara moja moja nawapa na rabbit pellets ambazo zinauzwa kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Mwanzo nilimuweka dume wa newzealand white pamoja na jike wa newzealand white ili wapandane. Nikawaacha wakae pamoja kwa wiki mbili, baada ya hapo nilamtoa yule dume, na kumuamishia kwa jike la flemish, na huko akakaa kwa wiki mbili. Hapo nikashinda kumhamisha kwasababu banda lenyewe lina cages mbili tu. Nikagundua nimechemka 😀 nikaona inabidi niwe na vyumba zaidi ya viwili.

Nikamwita fundi, tuka design jinsi ya kugawa lile banda ili tupate vyumba zaidi. Tukafanikiwa tukapata vyumba (cages) vinne. Hapo sasa nikaweza kumhamisha dume na kumweka kwenye chumba cha peke yake.

Baada ya mwezi mmoja na siku kama nne hivi tokea lile jike la new zealand white amalize dozi yake ya kupandwa, akazaa vitoto vitano, vizuri vyenye afya. Mpaka sasa vimeanza kuacha kunyonya na kuanza kula vyakula vya sungura wakubwa. Sasa kimeo kikawa kwa huyu jike aina ya flemish.

Itaendelea....
Jike aina ya flemish likaja kuonyesha aina zote kuwa lina mimba. Kama kawaida likaanza kuingiza majani kwenye kiboksi cha kuzalia, na likaonyesha kuongezeka uzito. Hiyo ilitokea baada ya kupandwa na dume kwa muda wa wiki mbili. Nikawa nasubiri kwa hamu sana nikiamini baada ya mwezi mmoja, na yeye atajifungua.

Kwa kawaida mimba ya Sungura inadumu kwa siku 28 mpaka 30. Sasa hili jike aina ya flemish, akapitisha siku 30 mpaka zikafika siku 35. Nikaona bila bila. Ikabidi niingie kwenye internet niperuzi kidogo, nijue zaidi. Kuna mahali nikasoma kuwa Sungura kuna wakati mwingine anaonyesha dalili zote za mimba kumbe unakuta ni fake pregnancy. Pia dume lilimaliza kupanda jike moja, inabidi ulipumzishe angalau wiki mbili, huku ukimlisha vizuri, ili ajenge mbegu za uzazi vizuri na apate nguvu za kupanda tena.

ikabiidi nifwate huo utaratibu nianze upya, utaratibu wa kumpandisha huyo jike aina ya flemish. Baada ya kumpandisha upya, sasa hivi ameonyesha dalili tena za kuwa na mimba, na ninamuomba Mungu, safari hii azae watoto kama yule jike mwingine.

Baada ya kumtenga yule dume kwa zaidi ya wiki moja sasa, leo nimenunua jike mwingine aina ya carlifornia, Nimemuweka kwenye kizimba chake mwenyewe, nitamlisha kwa wiki moja, alafu nitaanza utaratibu wa kumpandisha. So far hiyo ndio hatua niliyofikia mpaka leo tarehe 11.01.2025.

Nitaendeleka kuweka updates humu pamoja na picha kadri nitakavyokuwa najaaliwa na mwenyezi Mungu kusonga mbele zaidi. Nakaribisha maoni, maswali, na ushauri. Asante 🙏🏿
 
Kijana tafuta kijiwe cha unywaji upate moja moto moja baridi upooze akili.

Mambo ya nyama ya kuku ndio hadi uniite nina akili ndogo 😂😂😂.

Uko wapi kwanza nikuletee kitimoto na bia mbili??
Wanasema Kila mtu atachanganyikiwa kwa wakati wake🤣🤣🤣

Kuna watu wanachukulia serious vitu vidogo sana
 
Back
Top Bottom