Nimeanza safari ya ufugaji Sungura mwaka jana (2024) mwezi wa kumi, namshukuru Mungu, nimeanza kuona maendeleo taratibu, hatua kwa hatua

Nimeanza safari ya ufugaji Sungura mwaka jana (2024) mwezi wa kumi, namshukuru Mungu, nimeanza kuona maendeleo taratibu, hatua kwa hatua

Jike aina ya flemish likaja kuonyesha aina zote kuwa lina mimba. Kama kawaida likaanza kuingiza majani kwenye kiboksi cha kuzalia, na likaonyesha kuongezeka uzito. Hiyo ilitokea baada ya kupandwa na dume kwa muda wa wiki mbili. Nikawa nasubiri kwa hamu sana nikiamini baada ya mwezi mmoja, na yeye atajifungua.



Kwa kawaida mimba ya Sungura inadumu kwa siku 28 mpaka 30. Sasa hili jike aina ya flemish, akapitisha siku 30 mpaka zikafika siku 35. Nikaona bila bila. Ikabidi niingie kwenye internet niperuzi kidogo, nijue zaidi. Kuna mahali nikasoma kuwa Sungura kuna wakati mwingine anaonyesha dalili zote za mimba kumbe unakuta ni fake pregnancy. Pia dume lilimaliza kupanda jike moja, inabidi ulipumzishe angalau wiki mbili, huku ukimlisha vizuri, ili ajenge mbegu za uzazi vizuri na apate nguvu za kupanda tena.



ikabiidi nifwate huo utaratibu nianze upya, utaratibu wa kumpandisha huyo jike aina ya flemish. Baada ya kumpandisha upya, sasa hivi ameonyesha dalili tena za kuwa na mimba, na ninamuomba Mungu, safari hii azae watoto kama yule jike mwingine.



Baada ya kumtenga yule dume kwa zaidi ya wiki moja sasa, leo nimenunua jike mwingine aina ya carlifornia, Nimemuweka kwenye kizimba chake mwenyewe, nitamlisha kwa wiki moja, alafu nitaanza utaratibu wa kumpandisha. So far hiyo ndio hatua niliyofikia mpaka leo tarehe 11.01.2025.



Nitaendeleka kuweka updates humu pamoja na picha kadri nitakavyokuwa najaaliwa na mwenyezi Mungu kusonga mbele zaidi. Nakaribisha maoni, maswali, na ushauri. Asante 🙏🏿

Hongera
 
Baada ya kukaa muda mrefu bila kujihusisha na ufugaji wa aina yoyote, kuacha mbwa mmoja ambae namfuga kwaajili ya ulinzi, mwaka jana, 2024 mwezi wa kumi mwanzoni, niliamua kuanza ufugaji wa Sungura kwaajili kupata mboga kwa matumizi ya nyumbani na pale patakapokuwa na Sungura wa ziada, basi nitawauza niingize kipato kwaajili ya kuendeleza zaidi ufugaji huo.

Katika thread hii ntajitahidi kutoa taarifa kwa kadri ya uwezi wangu, kadri mradi huo utakavyokua ukiendelea, ninakaribisha maoni, ushauri, na maswali. Namuomba Mwenyezi Mungu aniongoze katika hili jambo.🙏🏿

baada ya kufanya utafiti kidogo, kukusanya taarifa na kuandaa fungu la pesa kwaajili ya mradi huo, niliamua kuanza ujenzi wa kibanda cha kufugia chenye vyumba viwili. Niliamua kujenga banda kwa kutumia vifaa vya chuma, na nyavu za chuma. (nita weka picha baadae kidogo)

Nilitafuta fundi, akafanya kazi hiyo vizuri sana, namshukuru Mungu, banda likaisha salama kabisa. Baada ya kujenga banda, nikatengeneza viboksi vya kuzalia (nesting boxes) viwili, kwaajili ya kila chumba (cages) hapo banda likawa limekamilika. Kazi yote ya kujenga banda pamoja na kutengeneza nesting boxes ilichukua wiki moja. Baada ya hapo, nikapumzika kwanza.

Itaendelea.....

Updates zote ziko kwenye posts zilizofwata huko mbele kwenye huu uzi
Soko lake liko vipi mkuu ?
 
Back
Top Bottom