Nimechukua mkopo benki, naomba ushauri katika namna niliyopanga kuutumia

Na hizi ndizo akili za wafanyakazi wengi wa serikali za dunia ya tatu. Baada ya Mambo kuwa magumu hapo mbeleni chuki zake atazielekeza kea serikali na wengine wasiohusika na umbumbumbu wake!Mimi ninakushauri mleta mada hapa kijiweni,chukua pesa kiasi nunua eneo nje kidogo ya mji anzisha project ya ufugaji au hata hapo uliposema unamlizia kujenga weka mabanda ya ufugaji wa kuku na ng'ombe wa maziwa Hilo gari ahirisha Kwanza kununua au Kama utanunua iwe ni gari ya kazi Kama kirukuu hivi then we'll vijana wa kusimamia wakati unaendelea na ajira yako,au hata Kama wife/husband Kama yupo free asimamie!acha hao wafanyakazi wenzio wakucheke we endelea kudandia tu daladala and trust me miaka mitano ijayo utadrive gali Kali zaidi yao kwenda nayo kazini.acha kuishi ili wengine wakuone kuwa unaishi Bali ishi ili maisha yakufurahie yatamani uendelee kuyaishi!
 
Ndio mim mtumishi ila sitegemei kazi kuendesha maisha nina baadhi ya vtega uchumi napia sina familia

Sent using Jamii Forums mobile app
Unadhani mtu Kama Bakhresa angekuwa na akili Kama ya kwako angekuwa hapo alipo?hivi wewe unavyoona anahangaika Hadi kupika chapati huwa unamchukuliaje?huhitaji kuwa milionea?kwa comment hii unaonekana Bado una akili ya kimasikini japo Mungu amekujaalia fursa za kupata zaidi maendeleo kea manufaa yako na wengine.huwezi just Kuna watu Mungu amewaandikia watakula kupitia wewe either kea ajira au misaada lakini unawachelewesha kwa sababu binafsi!
 
Sijawah ila nilikua natumia ya baba

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana umeng'ang'ania kununua gari kumbe hujawah kumiliki.
Ndio inakuwaga hvyo kwa mtu ambaye hajawah kumiliki gari kunakuwa na shauku sana.
Hata mm iliwah kunitokea kuna hela niliipata nikasema niigawanye nyingine nikanunua gari ili inayobaki nimalizie mjengo.
Basi kilichofuata hapo ile pesa iliyibaki yote ikatumika kwenye gari kujaza mafuta na kununua spares mara kwa mara na nyumba haijamalizika hadi leo
 
Pole kk..huenda ulinunua gari yenye high consumption of wese
 
Nimeajiri watu 2 kaka had sasa i hope wew mwenye akil kama ya bakhresa utakua una maviwanda
 
Sawa ushaur mzur ila hizo biashara ulizonitajia ushawah kuzifanya ? Maana nilishawah kushauriwa nifuge kuku chotara na mtu asie na uzoefu badae nikaambulia hasara tupu
 
Shukran san mkuu
 
Ulipoomba mbona hukuomba ushauri asee.. We pambana tu
 
Mbona hiyo pesa ndogo sana labda ununue gari la mbao.
 
Sawa ushaur mzur ila hizo biashara ulizonitajia ushawah kuzifanya ? Maana nilishawah kushauriwa nifuge kuku chotara na mtu asie na uzoefu badae nikaambulia hasara tupu
Nilishawahi kufuga kuku wa kienyeji but ni mkoa tofauti na ninaoishi sasa.fuata maelekezo ya wataalamu wanaohusika Kama unafanya project yoyote ile,huku tunakupa options tu uamuzi ni wako mwenyewe kuamua.
 
Unakopa hela hujui unazifanyia nn. Daaaah, nipe n
Mm baada ya miaka 3 njoo nikupe 40mil
 
Unakopa hela hujui unazifanyia nn. Daaaah, nipe n
Mm baada ya miaka 3 njoo nikupe 40mil
Duh yan nikupe mil 30 alaf aftr 3yrs unipe 40mil? Profite 10mil? Hapana aisee hio hasara
 
Ninavyo faham kwa Ulaya mtu akiajiriwa moja ya mambo ya kwanza ni kupewa mkopo wa kununua gari kama hana na cha pili unapewa mkopo wa kukodi nyumba/kulipia nyumba.
Kwa mtazamo wa Waafrika walio wengi, huona gari kama anasa ila gari ni kitendea kazi kinachoweza kumuongezea mtu MUDA na hivyo kumuongeza kipatato.
Angeongelea GARI kama v8, prado nk hapo tungeweza kuona ni anasa
Sijamshauri mtoa mada ila ningependa kuliweka hili la gari vizuri
 
Harooo!!! huyo mwarimu ariyekufundisha herufi na matamshi arikuwa anaandika hivyo na kutamka hivyo!!!?
 
Mkuu loan me 2 million ntarudisha 4 ,million in 30 days...
If interested pm me please
 
Asikupangie mtu matumizi ya pesa yako! Utakapokuwa unailipa nani atakusaidia?

For Car, go for IST, kama huna haraka agiza Japan haitazidi 13M mpk mkononi bt huchukua wiki 6-8.

In the mean time unakuwa unamalizia mjengo wako!

Ushauri: Tumia kwa busara, uchumi mgumu na hakikisha unaanza na vipaumbele vyako, bata baadae sana!

Masalia jazilizia kwenye bness zako ikusaidie kupunguza makali ya marejesho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…