Nimefanikisha kutimiza ndoto za binti wangu wa kazi

Pongezi nyingi sana
Ukweli ukiwatendea hawa vyema umebarikiwa mno. Shuhuda wangu Nina kijana wa shamba nilichukua toka 2004 na sasa ni baba wa familia ambaye anajitegemea akiwa bado kwangu shamba nikiwa nimewawezesha mke fundi cherehani na yeye kulima wa mboga na kuuza maji ya bomba nilimuunganisha ili apate kipato. Kuwawezesha ununuzi wa shamba huko Bagamoyo. Wanajikusanya kujenga nyumba yao na ninaamini nitawasaidia. Kupitia kwake huko tumekuwa familia
 
Muda wote huo huyo ni ndugu kabisa, hongera sana! Kuna mtu unakaa naye mnakuwa vizuri kushinda hata ndugu yako wadamu, hongera sana
 
Hongera sana ndg,umefanya jambo limpendezalo Mungu.
 
Hongera, kikubwa ni kuwa mkeo ana moyo mzuri.

Hongereni kwa hilo.
 
Safi sana mkuu Mungu akubariki
 
Angalikuwa rikiboy na timu yake ovu wangemtafuna kimasihara na kuleta mrejesho kwenye kambi yao chafu uzi wa wakubwa. Ningeweka hapa kieleelzo ila Sina connection
 
Aiseee.... Hongera Sana mkuu. Wewe ni binadamu wa kipekee Sana na Nina uhakika toka ulipoanza kumhudumia na kumchukulia kma ndugu yako nachelea kusema hujawahi kukwama au kutatizika kikubwa katika uchumi wako. Wakati mwingine, mema tunayotenda kwa ajili ya wengine huwa mtaji wa neema, baraka na fadhila za Mwenyezi Mungu katika maisha yetu ya kila siku.

Tusikimbilie kupeleka mamilioni ya sadaka na zaka madhabauni Wakati Kuna ndugu zetu wanataabika na kupitia magumu Sana kwenye maisha.
Vitabu vyenyewe vinatuhimiza kuwa tutasemaje kuwa tunampenda Mungu tusie muona Wakati ndugu/rafiki/jaama zetu tunao waona hatuwajali.

Alamsik
 
[emoji871] Mungu akufanyie wepesi mkuu, pole sana
 
Angalikuwa rikiboy na timu yake ovu wangemtafuna kimasihara na kuleta mrejesho kwenye kambi yao chafu uzi wa wakubwa. Ningeweka hapa kieleelzo ila Sina connection
Ule Uzi huwa siusomi Kati ya Uzi nisio u mind ni huo wallah.
 
Mkuu barikiwa na wewe pia
 
Duu pole sana, unaongea mpaka kwa uchungu duu

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…