Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Kunguni hawangalii masikini wala tajiri.

Prado hizo ziko 2. noah 2. Amarok 1. Pick up 1, Terrano 1, Pikipiki XL 250 iko 1.

Vikorokoro ni vingi ndio maana wadudu wanaingia bila taarifa
Kilichowaleta Kunguni Humo Ni Wivu Tu
Pia Tumia Dawa Inaitwa Lava Nayo Hii Bhaghosha
 
Mama angu alinisimulia kuwa kunguni zamani hizo kijijini walikuwa wanasumbua,mpk serikali ya kijiji inawahamisha watu,mnaweza hama mwaka mzima mkaacha nyumba,makazi mkirudi kunguni mnawakuta![emoji119][emoji848]nikasema hawa wadudu kiboko!
Lkn sikuhizi dawa zipo,wanakufa kabisa!
Mi niliyotumia walikufa kabisa hawakubaki!
 
Kunguni hata MAJI YA POVU KALI unawaua vizur tu.. Nunua sabun ya buku 2 dofi alaf changanya yote na maji Lita 20 njoo nishkuru baada ya wiki alafu mwagia KO na zote Kama unaosha kitanda
Jamani labda km kunguni wako wa aina tofauti,ila hawa naowajua Mimi hii njia ilifeli!
 
Mkuu hiyo dawa ni hatari sema umeweka kidogo ungechukua za 100ml chupa tatu ukapulizia
Mimi pia nafanya famigation
 
Sawa
Sawa, ila mara nyingi nimekuwa nikiona kunguni kwenye poor housing systems na mazingira ambayo si masafi sana.
Sijui kwa wengine ila mi home waliletwa na dada wa kazi kutoka kijijini!
Na hakukuwa na uchafu!
 
Kunguni ni kama jeshi la wa Vietnam katika Movie za kimarekani
 
Heeee yaani mna mpaka prado mna net ya maana mapazia ya bei nyumba ina rangi lakini hao wadudu wanaingia, pole
Kunguni hawana adabu, niliwaokota hostel nikawapeleka home, piga dawa waapi, bimkubwa aliishia kutupa masofa yake aliyokuwa anayapenda kama nini sijui, hata sijui walikuja kuishake pale home.
 
Mtakua watu wachafu sana mpka mpate kunguni,badilikeni acheni kua wachafu...
 
Kunguni ni kama jeshi la wa Vietnam katika Movie za kimarekani
Dah wale jamaa ni jeshi kweli, wakati nipo boarding bhana, ukiingia tu kitandani Hao wanaanza kuja mdogo mara wanaingia kwenye nywele, utasikia shingoni wengine wanauma mapajani na mikoni,
Nilikua nikishtuka kwa kuchoka vurugu zao nawasha tochi/solartaa, mara naona wahuni wanasepa speed kwenye machimbo yao, ukilala tena hao wanakuja tena.
 
Wana speed kali, halafu wanakua kunyuti, mumgu kawajaalia wale wapuuzi, anasimama sehemu na huhisi km kuna kitu, siku moja niko hostel mchana, namuona kabisa nikajidai kujitikkisa alisogea kidoogo kwa speed ya ajabu kisha akasimama, pale aliposimama huwezi kujua kama kuna kitu. Ndio nikajua hawa umbwa kwanin usiku anakuuma ila ukishtuka kapotea
 
Suluhisho pekee la Kunguni ni Maji ya Moto. Chemsha Maji yapate Moto kwa kiwango cha Juu kabisa halafu kamwagie Sehemu zote zenye Mazalia yao. Fua vitu vyote halaf anika Juani baada ya hapo kunguni utawasikia kwa wengine
Hawa wadudu washenzi sana. Hiyo dawa imenifaa pia. Inapendekezwa maji hayo yawekewe sabuni ya unga. Ifanyike mara kadhaa hata kwa muda wa wiki mbili mpaka tatizo litakapoisha. Aidha, inapofanyika hivyo si budi kuanika baadhi ya vitu nje mfano. Godoro, chaga, n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…