Nimefika mwisho wa kufikiri.... Nifanyeje? Naomba msaada wako

Kama unaishi Geita haupaswi kulalamika hauna kazi.

Toka mjini nenda vijijini huko kuna vijikazi kibaaao.

Hiko kibiashara cha mpesa hakiwezi lisha familia mkuu.

 
Mpesa umeanza na 13 yrs.
 
Kama unaishi Geita haupaswi kulalamika hauna kazi.

Toka mjini nenda vijijini huko kuna vijikazi kibaaao.

Hiko kibiashara cha mpesa hakiwezi lisha familia mkuu.

View attachment 3625553
Umenikumbusha na hii andiko langu dah mwaka wa pili Sasa sjasimama.

Kwa mtu mwenye mashaka nami anaweza ona hii picha akasoma niliko toka na nilipo.

Labda kaka unaweza ku recommend na kijiji nacho paswa kwenda kiongozi huwenda unataarifa napo Kwa Sasa Sina taarifa yoyote huko vijijini.

Ingawa najua vijiji baadhi vya geita vinajihusisha na uchimbaji huko nimetoka. Kuna KAZI ambayo ni free inahitaji nguvu zako ni uzegaji ile kazi kaka hapana. Nimekuweko nina picha na video ile KAZI hapana.

Uzegaji Kwa asiye fahamu ni kwamba, unabeba furushi na mawe kwenye mfuko wa kilo 60 kutoa shimoni Hadi juu unalipwa 2000 Kwa mfuko.

Siwezi Kwa sababu ya hatari ya zile kazi unaweza vunja mgongo, mguu n.k Bora saidia fundi ubeb4 tofali za cement au zege kuliko ile.

KAZI nyingine nafuu ni upigaji WA jackhammer ile inahitaji uzoefu tu shida pia ni sehemu ya kufikia na mtu wa kukushika mkono Kwa wiki Moja ukiwa unajifunza. Namaanisha yaani anaamua kwamba akufundishe Kwa kujitoa kwamba mnaenda kupiga kazi badala ya kufanya KAZI anatenga nusu saa anakuelekeza anakuachia upige.

Changamoto ni sehemu ya kufikia na malazi. Kwa wastani wa chini mtu kama atafikia guest atalala Kwa sh 3k atakula na kunywa kwa sh 4k jumla 7k Kwa siku.

Ni fedha ambayo Sina kumbuka wakati huo familia inatakiwa ile mkuu. Hapo ndipo nakwama.
 
Kwahiyo soon utaanza kututambia mshahara wa madollar
Hahah!! nitagawa hela Selfika , na nahitaji machawa kama wa 5 hapa Jf wakunisapoti .

Mimi sio Mzee wa kuvimba hakuna mtu ambaye anapenda umasikini na sio kila masikini mvivu au hapambani wengine hawana fursa tu na watu wa kuwashika mkono .

Imagine Mimi nilitafuta passport tokea nasoma 2024 na nikawa na pesa ya kuanzisha mchakato wa kutoka bongo tokea 2024 , nikakosa mtu wa kuniongezea M1 nikashike Madollar na mkwanja mrefu , ikabidi pesa yangu niwekeze kwenye biashara Fulani ilivyotoki nikaja baada ya hapo ndio nikaja KuActivate mpango tena 2026 .

Fursa ilikuwepo , mipango , jitihada na mapambano yalikuwepo ila nikakosa mtu seriaz wa kunisapoti kidogo tu nikakwama kwa niliyopitia nakosa mood ya kutamba na kuwaona wengine wazembe na kuwabeza maisha yao .
 
Mpesa umeanza na 13 yrs.
Nimemjibu hili swali kaka.

Ni kwamba biashara nimeanza zamani kuuza, miwa, mifagio matunda, mkaa nikiwa nawasaidia wazazi.. baadae waka transform kutoka huku Kuja huku hatimaye mwaka 2010 tukaanza huduma ya mpesa rasmi. Nikiwa na umri huo nilikua naingia shope kusaidia majukumu mle dukani. Miaka 14 nilikua na uwezo wa kuhudumia kabisaa
 
KABLA YA YOTE UNATAKIWA KUTUBU KWA MUNGU kwasababu ya kujihusisha na KULA RIBA.


RIBA NDIO SABABU KUBWA YA KUFELI WEWE KATIKA BIASHARA ZAKO

QURAN 2:275-276

"Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.
Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi."
 
Walokole bhana!🤣 Mbona kukopa bank mnaenda?
Hivi huwa mna akili timamu?
 
Kama unaishi Geita haupaswi kulalamika hauna kazi.

Toka mjini nenda vijijini huko kuna vijikazi kibaaao.

Hiko kibiashara cha mpesa hakiwezi lisha familia mkuu.

View attachment 3625553

Toka hayo

Toka hayo mazingira mkuu
Nina sababu nyingi zinazo ungana na wewe na nina tamani changamoto kwasasa nina home tie. Nikimaanisha nina watu wanao nifanya nisitoke Kwa haraka ama nitoke nikiwa na uhakika wa ninako kwenda. Kwasasa Sina hela Sina kazi
 
BIBLIA

KITABU CHA

Kutoka 22:25 BHN​

“Ukimkopesha fedha mtu yeyote miongoni mwa watu wangu walio maskini, usiwe kwake kama mdai, wala usimtoze riba."
 
Nashukuru sana Kwa quote y

Nashukuru sana Kwa quote kutoka katika kitabu Bora zaidi duniani.

Kama una Kazi au connection yoyote naomba kiongozi wangu niweze kujipatia ridhiki, hiyo itafaa zaidi.
 
BIBLIA

Mambo ya walawi 25:35-37

"Kama ndugu yako amekuwa maskini hata asiweze kujitunza mwenyewe akiwa pamoja nawe, ni lazima umtunze aendelee kuishi nawe; mtendee kama mgeni au msafiri aliye kwako. 36Usimtake akulipe riba ya namna yoyote ile. Ila mche Mungu, naye ndugu yako apate kuishi pamoja nawe. 37 Usimkopeshe fedha kwa riba au kumpa chakula ili akulipe faida. 38Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri ili kukupa nchi ya Kanaani, na ili nami niwe Mungu wako."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…