Nimefikia Conclusion Kanisa Katoliki ni waungwana, na wavumilivu, dini zote zina ibada za sanamu ukiwemo Uislamu

Nimefikia Conclusion Kanisa Katoliki ni waungwana, na wavumilivu, dini zote zina ibada za sanamu ukiwemo Uislamu

Ifike mahali mods wafunge jukwaa la dini, inakera sana miwatu mizima na vuzi zao kwapani,kifuani mpaka kwenye miguu kila siku inalumbana kama mitoto kwenye tamaduni walizoletewa huku wakiwa hawana uhakika nazo wakiambiwa wathibitishe.

Mimi sio atheist lakini hizi mada ni zakipumbavu, haijalishi we ni mkristo,muislam au mhindu kama umekosa utu wakuheshimu wengine kwa kutaka uonekane bora basi ni mpumbavu tu kama wapumbavu wengine
Naunga mkono hoja mods wapige ban nyuzi zote za kidini.
 
Wewe ukiona dini inakuambia "ukisafiri mpaka nchi fulani, ambayo ni takatifu utasamehewa dhambi zako." Utakuwa kama mtoto mchanga. Hiyo ni ibada ya sanamu. Kutupa mawe kama ishara ya kumpiga shetani, hiyo ni ibada ya sanamu. Kuangalia uelekeo fulani kila unapo sali hiyo ni ibada ya sanamu. Kuhesabu shanga kama njia moja wapo ya kufanya ibada, ni ibada ya sanamu.

Wewe ndiye unapotosha kabisa......
1. Swala sio kusafiri ukasamehewe, swala hapa ni taratibu za kufuata kabla ya hiyo safari; Zikijumuisha; Uhakikishe umelipa madeni yako yote, umepatana na ndugu zako wote, umefunga na kutubu, umewaomba msahama uliowakosea na umewasamehe walio kukosea nk nk baada ya taratibu zote hizo ndio unasafiri...kimsingi kwa kufanya hivyo (kwa nia) unakuwa umesha samehewa tayari....japo wapo wanao jiendea tu kwa sababu wana hela ya safari.

2. Kusali kwa lugha moja na kwa ueleleo mmoja ambao mtu yeyote duniani, anajua tu bila hata kutumia nguvu hiyo yenyewe ni muujiza kwa wenye maarifa.

3. Hakuna kitu kinaitwa kuhesabu shanga...Kile ni kihesabio tu cha kumsadia mtu kuweka kumbukumbu (sawa na vile vya primary), na sasa Shanga zinatoweka wanatumia vihesabio digital. Mfano unataka kuita jina la Mungu mara 30, kile kihesabio kinakusaidia (kama shanga zipo 15 inamaana utarudia mara mbili).
 
Kwani Musa aliyeandika torati alikuwa mkatoliki?
Mfalme Suleiman na Daudi aliyeandika zaburu alikuwa mkatoliki?
Wale manabii kama Hagai na Danieli walikuwa wakatoliki?
Walioandika injili yaani Mathayo, Marko, Luka na Yohana walikuwa wakatoliki?
Yohana aliyeandika ufunuo alikuwa mkatoliki?

Sasa kwa kigezo kipi unasema biblia imeandikwa na Catholic? Catholic imefanya editing.
🔨nakazia
Wakati Yesu anasoma chuo(scroll 📜 ) cha Isaya Ukatoliki haukuwepo
 
Qur-aan 109 : 1-6

1. Sema: Enyi makafiri! 1

2. Siabudu mnacho kiabudu; 2

3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. 3

4. Wala sitaabudu mnacho abudu. 4

5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. 5

6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu. 6
 
Sawa kila mtu ashinde mechi zake.
 
Na mimi siku zote huwa nasimamia hapa, siwezi kujiona dini yangu ni bora kuliko nyingine hadi kuanza kutukanana

Dini yako iwe bora kwako. Na si kuwa bora, kwa sababu unadhani inazizidi dini zingine
 
Wewe uliyekisoma ndo utuletee ushahidi hapa. Kwani kuna ugumu gani?

Waandishi wote wa vitabu vilivyoko kwenye biblia hakuna hata mmoja aliyekuwa mkatoliki.

Pengine ana maanisha aliye compile na kutafsiri katika lugha nyingine
 
Sio kweli...

Pindi tu Yesu Kristo alipoondoka, wafuasi wake walianza kuwa na fellowship lakini kwa kujificha sana...

Ukatoliki wa Kirumi ulikuja baadaye sana na hata matawi yake yalikuja baadaye pia...

Kuna imani za kikristo ambazo hazifuati wala kuwa na vinasaba na ukatoliki wa kirumi...
Sahihi kabisa
 
Wewe ndiyo umeongea.watu siyo wafuatoliaji wazuri wa dini hizi mbili. Almost kila kitu kinafanana. Isipokuwa tu wale wanasali kilatini wengine kiarabu. Hata mavazi ya mitume na wanawake enzi hizo walivaa kama waislam
Mkuu, hayo mavazi ya aina ya " Kanzu" sio mavazi ya kiisilamu bali ni mavazi ya watu/wenyeji wa Baara la Asia ya Kati na Mbali
 
Naunga mkono hoja mods wapige ban nyuzi zote za kidini.
Sijui kwa nini wanaiachia. Haileti afya kwa jamii. Halafu ni kosa kisheria kukashfu dini ya mwenzio, lakini knaonekana JF inaacha watu waendelee kuvunja sheria humu.
 
Wasabato ni sanam gani wanayoiabudu, je na phd ysko unajua maana ya kuabudu, ungeenda ku google then rudi tujadili. Roma hupiga magoti mbele ya sanam 2, bikra maria na yesu.
Soma vizuri kutoka 20 ndo ujue kuabudu ina maana gani. Kushika ukuta sio kuabudu. Hata wakristo huwa tunarnda mshsli yedu aliishi kwenda kutembelea
Unazungumzia Hawa wasabato waumini wa Ellen G white walioanzia juzi juzi tu hapo na kutabili mwisho wa Dunia kabla ya mwaka 2000?
 
Wewe ndiye unapotosha kabisa......
1. Swala sio kusafiri ukasamehewe, swala hapa ni taratibu za kufuata kabla ya hiyo safari; Zikijumuisha; Uhakikishe umelipa madeni yako yote, umepatana na ndugu zako wote, umefunga na kutubu, umewaomba msahama uliowakosea na umewasamehe walio kukosea nk nk baada ya taratibu zote hizo ndio unasafiri...kimsingi kwa kufanya hivyo (kwa nia) unakuwa umesha samehewa tayari....japo wapo wanao jiendea tu kwa sababu wana hela ya safari.

2. Kusali kwa lugha moja na kwa ueleleo mmoja ambao mtu yeyote duniani, anajua tu bila hata kutumia nguvu hiyo yenyewe ni muujiza kwa wenye maarifa.

3. Hakuna kitu kinaitwa kuhesabu shanga...Kile ni kihesabio tu cha kumsadia mtu kuweka kumbukumbu (sawa na vile vya primary), na sasa Shanga zinatoweka wanatumia vihesabio digital. Mfano unataka kuita jina la Mungu mara 30, kile kihesabio kinakusaidia (kama shanga zipo 15 inamaana utarudia mara mbili).

Naheshimu mawazo na imani yako licha ya kuwa sikubaliani nayo kwa asilimia zote.
1. Umetaja hatua za kufuata, hivyo umethibisha.
2. Waumini wanaunganishwa kwa imani, itikadi na mapokeo lakini kabila, nchi au jamii wanaunganishwa na lugha, ambayo imo kwenye mila, tamaduni na desturi. Ambavyo havihusiani na dini. Dini ni imani dini si lugha.
3. Pitia upya wazo lako, naona umejaribu tu kuwasilisha mawazo niliyoyasema kwa maneno mengine. Kuhesabu shanga ni ibada ya sanamu. Hata wale wanaotumia sanamu watakwambia ni namna tu ya kuvuta hisia ya uwepo wa Mungu
 
Unawajua wahubiri wote ? Katika uislamu au vitabu vya uislamu hakuna neno ukristo kuna manaswara ...Hakuna ibada inataja wakristo hata surah moja ,ndio kaana Qur an inatafsiriwa kama ilivyo ...Hao wanaotaja wakristo ni matakwa yao .

Tafsiri za mchongo wanaweka ukristo kwenye neno manaswara hapa utaelewa kwa nn Qur an inasomwa kwenye lugha yake ya asili.
Mkuu, umenene vyema kwamba " ndio maana Quran inasomwa kwenye lugha yake ya asili" Kwa mantiki hiyo nguvu ya kitabu hicho kipo kwa ajili ya wale wa asili yake; nje ya hapo kinapoteza uasili wake?
 
Back
Top Bottom