Napendekeza pia liandaliwe tangazo la dakika 2-3 la Tundu Antiphas Lissu akiongea kwa utulivu kuhusu sera za chadema kwa ujumla. Awe amekaa nyuma yake Kuna bendera ya Tanzania, huku akiwa anawaomba kura watanzania na akitaja sera Kuu na vipaumbele vikuu vya Chadema.
Nyimbo hii iwe sehemu ya Tangazo hili Yaani Soundtrack wakati Lissu anazungumza!!
Tangazo hili likishaandaliwa liipiwe kurushwa kwenye Radio stations hasa za mikoani, na mijini bila kusahau Channel za Video( ITV na Clouds) pamoja na Channel za online.
Najua CCM wakiona hili wataiga na kutengeneza lao Ila Chadema na nyie tengenezeni lenu mkitumia hii nyimbo kama Soundtrack!!
Cc
Chadema Diaspora,
Tumaini Makene,
John Mnyika na
CHADEMA