Nilipata kusimuliwa kisa kimoja,
Kuna bwana mmoja alikua akitembea ufukweni huku akitafakari juu imani ya kikristo ya utatu mtakatifu yaani Mungu baba,Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu,huyu bwana aliona kwamba anapigwa haiwezikani Mungu mmoja nafsi tatu.
Ghafla akakutana na katoto kadogo pake yake kakiwa kanafukua mchanga wa ufukweni akavutwa kuongea nacho kwani kalikuwa peke yake pasipo wazazi.
Huyu bwana akakauliza kanafanya nini pale kakiwa peke yake?
Kale katoto kakamjibu kanachimba shimo ili kahamishe maji yote ya bahari kwenye kishimo anachochimba na bahari itakauka kabisa.
Yule bwana akakaambia kale katoto karudi nyumbani kwani haiwezekani kuhamisha maji ya bahari yaenee kwenye kale kashimo.
Kale katoto kakamjibu kwamba uwezo wa kichwa chake ni mdogo Sana kulielewa fumbo la imani la utatu mtakatifu linalo msumbua kulitafakari,vivyo hivyo ataendelea kuona haiwezekani maji ya bahari kuyahamishia kwenye kale kashimo kwani uwezo wa kichwa chake ni mdogo.
Yule bwana akaingiwa hofu dogo amejuaje kwamba yeye anatafakari juu ya utatu mtakatifu.
Kwa bahati mbaya kale katoto kalitoweka kwenye mazingira yakutatanisha.
Kwa mafano huu ni dhahiri uwezo wa vichwa vyetu ni mdogo Sana kutafakari na kuelewa habari za uwepo wa Mungu.
Samahani kwakujibu kwa hadithi ndefu chief.