Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Kwa hiyo unaamini simu imetengenezwa na mtu na yupo, unaamini gari kuna wajapani wameitengeneza ila hayupo aliyekutengeneza wewe na babu zako wote? Mzee kuna eneo lingine tofauti na hili ambapo una ukilaza wa hiyari?

Yaani simu haukumuona mtengenezaji ila kwa confidence kabisa unaamini yupo. Grai unaamini yupo aliyelitengenza japo hujawahi hata kuongea naye. Ila Aliyekutengeneza wewe umeamua kuamini hayupo? Dah, kweli kuna ujinga wa hiyari!
Tunachohitaji is the cause of every cause.
Mungu ametuumba kama ni hivyo yeye ameumbwa na nani?
Na kama hajaumbwa kwa nini sisi iwe lazima tumeumbwa!?
 
Shetani ndio husema hivyo ili afiche ukweli. Anyway Yehova hahitaji wewe mimi au mtu mwingine amwamini ili awepo. Yaani Yupo halafu ndio Mungu sasa. Alikuumba na huna cha kufanya. Na kuna siku utakutana naye uso kwa uso. By then hata ujasiri wa kumwita Mungu let alone shetani utakuwa huna.

Angalau utaikumbuka hii post! Hello, wake-up before it's too little late!
Vipi kama wewe ndio umesinzia and you need to wake up?
Kusema wake hata kwenye ndoto unaweza kusema.
 
Mpumbavu husema moyoni mwake hakuna Mungu, bible.

Usitazame nje ili uone uwepo wa Mungu
Anzia kwako wewe hapo

Ulipokua haupo, shahawa ya baba yako na yai la mama yako vilivyokutana ukaanza kutengenezwa,
Kwanza ukiwa bonge zito la damu
Baadae ukajishika kwenye mji wa mama yako
Ukakulia humo huku viungo vyako vikijitengeneza ukianza na moyo, then mishipa ya damu, ubongo, na viungo vingine , mifupa yako inayokufanya uweze kuwa na hiyo fremu , sikio, jicho na kila kitu

Ukakua hadi muda ukafika ukaanza uchungu, ukapita kwenye uke wa mama yako!

Umbilical cord ikakatwa ukaanza kunyonya huku hujui unachokifanya!
Kwa sababu hakuna ambaye ana kumbukumbu ya hayo hadi pale wakati unapofika kumbukumbu unapozaliwa na ufahamu kuwepo, Mambo yote haya yakitokea kwa mpangilio wa aina yake!

Ufahamu kuwa wewe siyo hizo hisia ulizoziandika hapo! Ubongo wako ukipewa chakula na moyo wako ukawa hai ndivyo vilivyokufanya uandike hayo!


Pamoja na uhuru uliopewa ukatype bila obvious consequences as of now!


Njoo Nje yako sasa

Tazama hapo ulipo angani wakati wa mchana...
Jua

Je unajua kwamba dunia na ardhi yake ipo angani inaelea!

Unayo hii perception? Kwamba unaweza kwenda Around hii ardhi/ dunia— ile circumnavigation?
Kwamba Gimba hili liitwalo dunia linaelea angani na hawa watu wengi wasioona?!

Je mpangilio huu umejiweka wenyewe!
Je vitu alivyovifanya mwanadamu vimejiweka tu vuu vikawa?

Kama ni ndege ulaya ina design yake, kama ni gari/ pikipiki vilevile.

Hakuna chombo chochote kilichozuka!
Lazima kila chombo kina design yake na designer wake!

Vyombo artificial vina design yake na designer wake ambae ni Mtu

So kupanga ni kuchagua lakini unapowaza kuhusu Mungu ukafikiri hayupo jitazame wewe kwanza—look through you you siyo unamtazama mtu kwa ngozi yake tuu!

Mtazame as a whole and as made of Parts.
Mtazame kwa hilo jicho la kitabibu kama kitu kamili kilicho na parts na Umuone akiwa hai lakini akiwa wa kufa pia.

“See now that I, even I, am he, and there is no god with me: I kill, and I make alive; I wound, and I heal: neither is there any that can deliver out of my hand.” Bible
Hayo yote yana prove vipi ndio Mungu unayemwamini na si Alla kwa waislamu,
Shinto kwa japan, Budha kwa wa china au Krishna kwa wa hindi?
Na kama Mungu alikuumba, yeye aliubwa na nani?
Kama hakuumbwa kwa nini wewe unalazimisha uliumbwa?
 
Huyo huyo unaye amua ww kumu amin ..
Lets say kama umemuamini Mungu Allah

Halafu tukarejea kwenye hoja yako ukasema "ni bora uamini Allah yupo na ukaenda usimkute kuliko ukaamini hayupo na mwisho wa siku ukamkuta yupo"

Halafu ukaulizwa swali, vipi kama ukaamini Mungu Allah halafu mwisho wa siku ukamkuta Mungu yahwe kua ndiye Mungu wa kweli ambaye ulimpuuza?

Utafanyaje?
 
Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
Shida ukiamini haya Mambo unakuwa chizi sadaka zinaliwa tu na wajanja
 
Umeanza kuamini katika movie[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😅😅😅 Too slow. Nimempa iyo movie ili nikimuelekeza baadhi ya mambo tofauti tofauti aweze kuhandle.
Nothing=Everything
 
Amini tu kuwa Mungu yupo, haitakugharimu chochote.

Ukifika huko ukakuta hayupo it's okay.
Statement hii haipo specific katika ulimwengu wenye dini zaidi ya 5,000 ambazo kila mmoja ana abudu Mungu tofauti na mwingine

Kwa hiyo weka wazi ni Mungu yupi ambaye hata ukimuamini haita kugharimu?
 
Tunachohitaji is the cause of every cause.
Aliyekwambia kila kitu kina chanzo nani? Umeitoa wapi hii?
Mungu ametuumba kama ni hivyo yeye ameumbwa na nani?
Huyo "mungu" anayeumbwa ni feki. Kwanza una assumption zisizo za kweli kwamba kila kitu kina mwanzo. Hii nadharia umeitoa wapi?
Kisayansi na kifalsafa ni kitu chenye mwanzo pekee ndio kina sababu ya chanzo. Sasa Mungu hana mwanzo wala mwisho unataka chanzo kianzie wapi?

Na kama hajaumbwa kwa nini sisi iwe lazima tumeumbwa!?
Kwa sababu tuna mwanzo. Hahitaji kuumbwa kwa sababu hana mwanzo. Ulitaka aumbwe lini sana?
 
Nilipata kusimuliwa kisa kimoja,

Kuna bwana mmoja alikua akitembea ufukweni huku akitafakari juu imani ya kikristo ya utatu mtakatifu yaani Mungu baba,Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu,huyu bwana aliona kwamba anapigwa haiwezikani Mungu mmoja nafsi tatu.

Ghafla akakutana na katoto kadogo pake yake kakiwa kanafukua mchanga wa ufukweni akavutwa kuongea nacho kwani kalikuwa peke yake pasipo wazazi.

Huyu bwana akakauliza kanafanya nini pale kakiwa peke yake?

Kale katoto kakamjibu kanachimba shimo ili kahamishe maji yote ya bahari kwenye kishimo anachochimba na bahari itakauka kabisa.

Yule bwana akakaambia kale katoto karudi nyumbani kwani haiwezekani kuhamisha maji ya bahari yaenee kwenye kale kashimo.

Kale katoto kakamjibu kwamba uwezo wa kichwa chake ni mdogo Sana kulielewa fumbo la imani la utatu mtakatifu linalo msumbua kulitafakari,vivyo hivyo ataendelea kuona haiwezekani maji ya bahari kuyahamishia kwenye kale kashimo kwani uwezo wa kichwa chake ni mdogo.

Yule bwana akaingiwa hofu dogo amejuaje kwamba yeye anatafakari juu ya utatu mtakatifu.

Kwa bahati mbaya kale katoto kalitoweka kwenye mazingira yakutatanisha.

Kwa mafano huu ni dhahiri uwezo wa vichwa vyetu ni mdogo Sana kutafakari na kuelewa habari za uwepo wa Mungu.

Samahani kwakujibu kwa hadithi ndefu chief.
So interested, but it has nothing to do with existence of God
 
wewe mzindakaya acha upuuzi,, History yenyewe ya form two inakubali uwepo wa mwana wa MUNGU. Before Christ BC
 
Aliyekwambia kila kitu kina chanzo nani? Umeitoa wapi hii?

Huyo "mungu" anayeumbwa ni feki. Kwanza una assumption zisizo za kweli kwamba kila kitu kina mwanzo. Hii nadharia umeitoa wapi?
Kisayansi na kifalsafa ni kitu chenye mwanzo pekee ndio kina sababu ya chanzo. Sasa Mungu hana mwanzo wala mwisho unataka chanzo kianzie wapi?


Kwa sababu tuna mwanzo. Hahitaji kuumbwa kwa sababu hana mwanzo. Ulitaka aumbwe lini sana?
Kama kuna baadhi ya vitu havina mwanzo.
Kwa nini unalazimisha binadamu anamwanzo?
 
Shida ukiamini haya Mambo unakuwa chizi sadaka zinaliwa tu na wajanja
Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.

Huwezi kuiamini na kuifuata Biblia na bado ukatapeliwa na hao wahuni. Unless "haya mambo" unamaanisha kitu kingine!
 
Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.

Huwezi kuiamini na kuifuata Biblia na bado ukatapeliwa na hao wahuni. Unless "haya mambo" unamaanisha kitu kingine!
Hahaha!!! Nyakati za mwisho zimeimbwa sana na hazifiki..
Biblia imeandikwa vatican, unaitumiaje kama reliable source yako?
 
Kama kuna baadhi ya vitu havina mwanzo.
Kwa nini unalazimisha binadamu anamwanzo?
Khaa! How absurd is your question. Kwa hiyo birthday yako kwa mfano ina maana gani?
Na Scientifically ulimwengu wote kwa pamoja una mwanzo. Tunatofautiana tu ulianza lini na ulianzaje. Lakini kuwa una mwanzo hilo swali lilishakuwa settled long ago!
 
Haya mambo ni yapi? Biblia imesema kuwa nyakati hizi za mwisho kutakuwa na matapeli wengi na watakuja kwa jina la Yesu. Na kwamba wazipime kila roho, ili kuona kama zimetoka kwa Mungu. Na ya kuwa watawajua kwa matendo yao.

Huwezi kuiamini na kuifuata Biblia na bado ukatapeliwa na hao wahuni. Unless "haya mambo" unamaanisha kitu kingine!
Yani siku biblia ikisema hakuna moto wafia dini hawataimba tena hizi nyimbo za kumpenda Mungu,
mnaongozwa na hofu wala sio mapenzi ya dhati na Mungu wenu.
 
Hahaha!!! Nyakati za mwisho zimeimbwa sana na hazifiki..
Unaelewa hata ya maana ya nyakati za mwisho?
Naamini hujui kwa sababu wakosoaji wa Biblia wengi wao hawaijui!
Biblia imeandikwa vatican, unaitumiaje kama reliable source yako?
Nilijua tu hujui. Biblia imeandikwa na Vatican lini?
Hivi hauoni hata aibu kuandika stori za vijiweni unapoongea kwenye mijadala serious kama huu? Kwamba Vatican iliandika Biblia ambayo imekuwepo kabla ya Vatican? Eeh, kuna eneo jingine ambalo umeamua kuwa kilaza kama hivi? Yaani ukilaza wa hiyari?
 
Mpagani ni mpwgani ata ukilemba vipi.Tupo waislamu wenye hofu ya allah lakini hatufanyi ibada ya kutosha kwa sababu ya udhaifu wetu lakini hatujawahi kubisha uwepo wa Allah.
Mpagani ni mpagani tuu
Unahaki ya kusema walio kinyume na imani yako ni wapagani na kwa ulivyo jinasibu kua wewe ni muislamu wala sishangai

Kwasababu maneno ya namna hiyo yameanzia ndani humo humo kabla hyajawafikia wengine wasio husika na imani yao

Hata humu JF kuna member anajita Mubarridi aliwahi kumtamkia Mokaze kua ni kaffir

Na wote humu tunajua huyo jamaa aliyeitwa kaffir ni muislamu pia, ila nilichokuja kugundua ni kwamba yupo dhehebu tofauti na mdau, lakini hiyo pekee ya kuwa muislamu haikutosha kumfanya aepukane jina hilo ambalo absolutely hakulifurahia hata yeye

Sasa sembuse mimi ambaye sina asilimia yeyote nayo kubaliana naye?

Wewe ukiniita mimi mpagani unakuwa umesalimika kwa upande wangu nikiwa na maana siwezi kukuita mpagani kwasababu siamini katika dini, ila watu walio kinyume na dini yako lazima wakuhesabu kama mpagani, ni hivyo tu.
 
Back
Top Bottom